Profesa Wangwe: Afrika iongeze thamani ya rasilimali zake

Profesa Wangwe: Afrika iongeze thamani ya rasilimali zake

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,974
Reaction score
6,721
Profesa wa Uchumi, Samuel Wangwe, amesema nchi za Afrika zinapaswa kuweka kipaumbele katika kuongeza thamani ya rasilimali zake ili kunufaika ipasavyo na utajiri uliopo barani humo. Amesema miongoni mwa njia muhimu ni kuwekeza kwa vijana kwa kuwapeleka kujifunza katika mataifa yaliyopiga hatua kiteknolojia, ili warudi na kutumia ujuzi huo kuendeleza nchi zao.

Ameeleza hayo leo Januari 21, 2026, kupitia kipindi cha Mizani cha TBC 1, wakati akichangia mada inayohusu nafasi ya Afrika katika muktadha wa siasa za kikanda na maendeleo ya kiuchumi.

 
Kwanza, yeye binafsi ameongeza thamani kwenye rasilimali ipi? Kama mfano
 
Back
Top Bottom