Profesa Muhongo amekengeuka!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,897
Reaction score
25,238
Jana tumeshuhudia Profesa Muhongo akimchana Dr Ole Sendeka bungeni kwa kumkejeli na kumdhalilisha hadharani huku akifikia hatua ya kutaka kuweka hadharani matokeo yake (Ole Sendeka) ya mtihani wa kidato cha nne aliokaa mwaka 1984 katika Shule ya Sekondari Monduli.

Isingekuwa busara za Spika Makinda ni dhahiri kwamba Muhongo angeanika matokeo ya Ole Sendeka hadharani.

Badala ya kujibu tuhuma za ufisadi wa fedha za umma unaomkabili yeye (Profesa Muhongo) na mshirika wake (Maswi), Muhongo alitumia muda wa umma vibaya kwa kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi na kumdhalilisha vya kutosha.

Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, ushahidi ukishatolewa bungeni, kama alivyofanya Dr Kafulila na Dr Ole Sendeka, ni jukumu la tume ya maadili ya bunge kuuchunguza na kuona kama unakidhi haja na kisha kuwapelekea TAKUKURU na mahakama waufanyie kazi.

Sasa inakuwaje Madam Spika akamruhusu Prof Muhongo apoteze muda wa umma kwa kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi huku akikwepa tuhuma za ufisadi zinazomwandama yeye na Maswi? Hili suala sio sawawa hata kidogo.

Aidha, inaonekana kwamba Prof Muhongo ni mtu wa ajabu sana kwa jinsi anavyojisifu kwa usomi wake bila kuzingatia kwamba sisi watanzania tumemtuma akatuwashie umeme sio kututangazia usomi wake! Mh Mbowe aliomba muda uongezwe ili kila mbunge apate nafasi ya kuhoji namna mambo yanavyokwenda ovyo kwenye wizara hii lakini Prof Muhongo akambeza na kumdharau.

Majisifu ya kila siku ya profesa Muhongo na kuringia usomi wake sio tija kwa watanzania. Watanzania tunataka umeme na tunataka mafisadi wanaokula fedha za umma washughulikiwe.

Sisi hatuna haja na usomi wa Muhongo. Hata kama Wizara hii ikiongozwa na mtu aisiyekwenda shule kama vile Kapteni Komba au Prof Majimarefu, sisi hatuna shida na hilo. Shida na taabu yetu ni kuona kila mtanzania anapata huduma ya umeme wa uhakika.

Profesa Muhongo anatakiwa ajiandikishe kwenye chuo siasa cha CCM Kivukoni, akajifunze taaluma ya siasa na namna ya kuheshimu watu na mawazo yao, tofauti na jinsi anavyotenda mambo kwa sasa. Kutaja matokeo ya mtihani ya Ole Sendeka bungeni haikuwa hoja ya msingi. Hoja ya msingi ilikuwa ajibu tuhuma zinazomkabili yeye na msaidizi wake wa karibu (Maswi). Vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na watu wa chama na serikali haviwafurahishi wananchi hata kidogo. Wananchi wanataka mawaziri wachapakazi watakaowaletea maendeleao endelevu. Hawataki mawaziri domo kaya wanaoringia usomi wao wakati wanashindwa kutumia usomi huo kuwaletea wananchi maendeleo. Kutamba kwamba amewahi kuwa Rais wa wanajioljia Afrika hakutuongezei shibe na wala hakutupunguzii njaa. Muhongo anapaswa kupima kila neno linalotoka kinywani mwake na kutathimini madhara yake kabla ya kuropoka.

Kutaja hadharani matokeo ya mtihani ya mtu anayetetea wananchi, ni utovu wa maadili ya uongozi na nidhamu kwa kiongozi mkubwa kama Muhongo ambaye anategemewa kuwaletea watanzania maendeleo. Matokeo ya mtihani ya mtu ni SIRI, hayatakiwi kutajwa hadharani-hii ni NYARA ya serikali. Muhongo na hao watumishi kengeufu wa Baraza la Mitihani (NECTA) waliomchapia matokeo ya Ole Sendeka yafaa wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka miiko ya utumishi wa umma.

Nawasilisha.
:yield:
 
Muacheni Pamoja na usomi wake lakini akumbuke Siasa inaweza kumfanya akaonekana Bule kabisa na hafai we subili.
 
Kuna thread ndani humu ilimchambua Prof na nakumbuka aliyeandika alidai ya kuwa Prof anaugua ugonjwa wa grandios,nahisi unahusu majisifu.
Tatizo kubwa ni kuwa ameamini anamshambulia Sendeka lakini asijue (pamoja na usomi wake) ya kuwa anamshambulia mpaka spika na hata baadhi ya mawaziri.
Mambo haya ya kufanya vitu bila kutafakari repurcussion yake inaelekea yanajengeka kwani hata Mwigulu nae ameingia katika mkumbo huyo akitamani kuwa Rais ili awakomeshe (Rais aliyemteua kashindwa????).
Muhongo amezoea kufundisha wanafunzi wa chuo kikuu na anaona wote ni wanafunzi lakini akumbuke bunge hilo hilo lilimtoa EL (strong person) na naamini yeye hana killo kama za EL katika siasa.
 
Muhongo na Mwigulu huwa nawaona kama mapacha wa fikra, hawakustahili hata kuwa wenyeviti wa kijiji lakini Mkuu ndio kawaona wanafaa.
 
Hivi hujawahi kuambiwa kuwa sio kila aliesoma na kupewa vyeti kama alivyo Muhongo haina maana kuwa ameelimika unless anathibitisha uelevu wake kwa namna atakavyokuwa anaishi na kuhusiana na jamii. Pamoja na kuwa Mhongo anaonekana kuwa na kasoro ya kuzaliwa, elimu yake haijamsadia kuiepuka kasoro hiyo. Kitendo cha kuamini kuwa hakuna mtanzania mwelevu kuliko yeye bila shaka ni ushahidi wa ulemavu na kukosa adabu alikonako.
 
Pambafu ww: Hatuwezi kama nchi kila siku tunaimba ufisadi wa karatasi na magazeti ya Mengi. Vita na fitina kwa Prof hazina msingi wowote.
 

Longo longo pro muhongo siyo asili yake. kumshauri aende kivukoni kusoma siasa ni kumwambia aende kusoma longo longo. Mzee huyu haangalii sura wala chama. Ulivyokuja ndivyo atakavyokujibu. Kutaka kuonyesha matokeo ya mh Sendeka nayo ni sawa maana alitaka kuonyosha uelewa wa mtu huyo. tuwe wakweli hivi hatuoni mabadiliko ktk sekta ya umeme tangu pro muhongo awe waziri? kwa nn tusione kwamba huyu pro ameziba liziki za watu ndiyo maana anasakamwa? Hatukumbuki dili la mafuta mazito? Nani asiyeelewa Dr mengi anavyopenda kuabudiwa lkn pro hamuabudu na ndiyo chanzo cha wawili hawa kutoelewana? Mnataka serikali iwekwe mfukoni na watu wa aina ya Dr mengi? Watz bw angekuwa mpole mngemsodoa!! Anaonyesha makucha mnalalamika! kwani amezuia asichunguzwe km kuna tuhuma za kweli dhidi yake? Bila aibu unashauri wizara iongozwe na vihiyo mikataba ya kimataifa wataipambanuaje. Unasemaje matokeo ya mtu ni siri wakati hubandikwa ktk mbao za matangazo na sasa unayaona kiganjani? Huyu ni mzee wa makavu kavu. SHIKAMOO PRO MUHONGO.
 

ile transfoma ya mabilion imenunuliwa na kusafirishwa ktk uongozi wa nani
 
ile transfoma ya mabilion imenunuliwa na kusafirishwa ktk uongozi wa nani

kama utakuwa umehudhuria shule nadhani umesoma kwa miaka saba tu. Soma vzr post yangu nimesema kwani prof amezuia asichunguzwe?
 
Ila nilikuwa namheshimu jana nimemdharau totally,maprofesa wa bongo wanamuangusha sana kikwete kwa kweli.
 

Mshamba kama wewe hutaweza kuacha kushabikia kisa ni Prof na anatokea Musoma , tembea uone ma Prof wenzaje Duniani ni wa aina gani kaka .
 
Ole wao wenye kuifisidi nchi hii! Waombe kifo kiwapate kabla hawa watoto walioko sekondari za kata hawajakamata nchi! Wallah nawathibitishia watajuta kufanya ufisadi! Ni wakati tu unaosubiliwa, utafika!! Hivi watz mnafahamu ufisadi mwingine unaofanyika kupitia makato ya asilimia tatu wanayokatwa kila mwezi wateja wa tanesco kwa kisingizio cha kuchangia upelekaji umeme vijijini (rea) ni wizi mtupu, chunguzeni!
 
Duh m aliniaha hoi alipo muelezea mnyika aseeee,(aliuliza Mnyika kipeo cha 4+4 ni sawa 4... Tafuta mnyika.m. Aseee nlipofanya nakapata 0)
 
Cha ajabu ni pale wote wenye sifa kama za Ole Sendeka au wasio na sifa za usomi Kama Muhongo mwenyewe wanamshangilia kwa nguvu wakifikiri anawakomesha au ni kiboko cha wapinzani. Baada ya muda watagundua kuwa anawatukana na kuwadharau hata wao! Na pia wananchi wengine wote wasio soma kama yeye! Time will tell.
 
Watu wengi waliosoma Kwa shida ie kukariri Kwa kiwango cha juu ndivyo walivyo haimaanishi kuwa profesa ndio ana akili sana rais wa USA Lincoln alikuwa na Elimu ya kawaida sana lakini aliongoza kwa busara taiga kubwa muhongo aweke matokeo yake ya F4 na F6 tuone unaweza kuta alifaulu kawaida sana hamfikii hata mnyika mwenye matokeo ya muhongo yatupie javini tuchangie asije kuwa anatubabaisha hapa
 
mtoa mada kama nawe hujasoma usilalame. siku hz kuna opportune ya kusoma zaidi kuliko zamani. mwacheni prof ukalumekenge basi tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…