Elections 2010 Profesa Msolla aipa somo CCM kura za maoni......................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174


Profesa Msolla aipa somo CCM kura za maoni

Imeandikwa na Frank Leonard, Kilolo; Tarehe: 26th December 2010 @ 23:44

MBUNGE wa Kilolo mkoani Iringa, Profesa Peter Msolla ameomba mfumo wa kura za maoni unaotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata wagombea wake katika nafasi za ubunge na udiwani kuangaliwa upya kwa sababu unachochea makundi ndani ya CCM yanayozidisha hatari ya kushindwa katika chaguzi.

Profesa Msolla ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alisema kama mfumo huo hautafanyiwa marekebisho upo uwezekano kwa chama hicho kuendelea kupoteza ushindi katika maeneo yatakayokuwa na wagombea wengi kwenye kura hizo.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ruaha Mbuyuni juzi, Profesa Msolla aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa awamu ya kwanza ya Rais Jakaya Kikwete, alipendekeza kamati maalumu ya Kitaifa katika chama hicho iundwe ili kushughulikia suala hilo.

Akikumbushia maagizo ya Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Profesa Msolla alikita chama katika ngazi zote kufanya tathimini ya Uchaguzi Mkuu uliopita ili kubaini mambo yaliyosababisha chama kifanye vibaya kwenye baadhi ya maeneo.

"Pamoja na kufanya vibaya katika maeneo fulani fulani, ni vizuri pia tukajiuliza kwa nini wananchi hawakupiga kura kama ilivyotarajiwa na tuzitumie changamoto tutakazozibaini kuimarisha chama vinginevyo vyama vya upinzani vinaweza kuutumia mwanya huo kujiimarisha zaidi," alisema.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo, Profesa Msolla alisema vipaumbele vyake vikubwa vitakuwa katika maeneo makubwa manne ambayo ni pamoja na elimu, afya, miundombinu na shughuli za kiuchumi.

Hata hivyo, alisema katika kutekeleza Ilani ya CCM miaka mitano iliyopita, alikumbana na ushirikiano mdogo kutoka kwa madiwani na akawataka madiwani wapya wa Halmashauri ya

Wilaya ya Kilolo, kutimiza wajibu wao kwa wananchi kama walivyoahidi wakati wa kampeni. “Miaka mitano iliyopita kwangu mimi ilikuwa ni miaka ya mpito kwa sababu hata zile kazi zilizopaswa kufanywa na madiwani katika kata zao, bado zilionekana zinatakiwa kufanywa na mbunge na kwa kweli nilijitahidi nikazifanya, lakini sasa muda umefika kwa madiwani wapya kutekeleza wajibu wao,” alisema.

Kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Joseph Muhumba alisema wanaendelea kujipanga kikamilifu ili kumpa ushirikiano wa kutosha mbunge huyo katika kutekeleza ahadi mbalimbali alizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Muhumba anayekuwa mwanaCCM wa pili kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, aliikwaa nafasi hiyo hivi karibuni baada ya kumuangusha dada wa Profesa Msolla, aliyekuwa mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).
 
Hata hivyo, alisema katika kutekeleza Ilani ya CCM miaka mitano iliyopita, alikumbana na ushirikiano mdogo kutoka kwa madiwani na akawataka madiwani wapya wa Halmashauri ya

Wilaya ya Kilolo, kutimiza wajibu wao kwa wananchi kama walivyoahidi wakati wa kampeni. "Miaka mitano iliyopita kwangu mimi ilikuwa ni miaka ya mpito kwa sababu hata zile kazi zilizopaswa kufanywa na madiwani katika kata zao, bado zilionekana zinatakiwa kufanywa na mbunge na kwa kweli nilijitahidi nikazifanya, lakini sasa muda umefika kwa madiwani wapya kutekeleza wajibu wao," alisema.
Profesa msola anajua ya kuwa makundi ndani ya CCM hayasababishwi na kura za maoni bali jinsi CCM inavyoshindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.....ikiwemo raia kupandikiziwa viongozi wasiowataka......na vikao vya juu...........................makundi ni dalili ya kuwa CCM siyo chama cha wote ila kina wenyewe.........................................

CCM has shifted ground from a mass party to a vanguard one.........................who does not know this................angalia jinsi wanamtandao walivyoula ndani ya himaya ya JK........na wengine wametelekezwa....................kwa nini sasa yasiwepo makundi ya walaji na waangaliaji ulaji unavyoendelea..................
 
kwa hiyo Msolla yeye kufanya mkutano ni tiki lakini wenje,lema na Mbilinyi wao wanaleta fujo jamani hii nchi sijui tunaenda wapi
 
Rudi chuoni kakate nyanga...siasa sio kitu yako!Unapoteza muda tu Mh. Msolla...
 
Inaonekana CCM Wamechanagnyikiwa Hawajui Kwanini Wanashindwa Kuchaguliwa na Kushinda Viti Mbalimabali Nchini. The Saga Continue, Wananchi Wameshakua Kisiasa na Ngumu Kuwadanganya Tena na Tena.
 
kama kaongea na wananchi (wapiga kura wake) kwenye mkutano wa hadhara maana yake alitoa taarifa masaa 48 kabla na kuelezea ni nini anataka kuongea pia nakala polisi ya kiitelejensia kwamba amani itakuwepo....wenye uwezo wa kutunyofelea nakala za maombi hayo watuanikie! maana haiwezekani wabunge wa CDM wawe na matatizo wao tu kila siku!
 
kama kaongea na wananchi (wapiga kura wake) kwenye mkutano wa hadhara maana yake alitoa taarifa masaa 48 kabla na kuelezea ni nini anataka kuongea pia nakala polisi ya kiitelejensia kwamba amani itakuwepo....wenye uwezo wa kutunyofelea nakala za maombi hayo watuanikie! maana haiwezekani wabunge wa CDM wawe na matatizo wao tu kila siku!
Isipokuwa Zitto tu! hahaaaa. (Angalia kwenye thread ingine, (Zitto ampa waziri siku7)
 
Back
Top Bottom