Hata ingekuwa wewe huwezi kuachia ngazi maana kila mtu sasa anapenda pesa na maisha mazuri na kingine serikali yetu ni ya usanii maana haioni aibu hata kukana maamuzi yake yenyewe! Hivi unadhani jamaa ni mjinga kiasi hicho hapo walipokuwa wanajibu ni sehemu ya siasa ila ukweli serikali inao maana hii ingepita wangemsifu sana kwa ubunifu wa kuiokoa serikali ya chama tawala dhidi ya maafa ya wanaofeli kila mwaka.
Kwa vile wawakilishi wa wananchi wamejitahidi kuona kwa kiasi chao basi serikali inasema ni uongo kwa hiyo yenyewe inafanyia kazi taarifa za mfanyakazi moja kwa moja! Je baraza la mawaziri halikuwa na taarifa hii? Huu ni usanii tu maana hawawezi kumwajibisha kwa vile ukweli wanaujua maana huenda kuna barua ya kuruhusiwa kufanya hivyo na waziri husika!