JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524

Tumeshuhudia siku chache zilizopita mauaji ya kinyama ya rubani Capt. Roger yaliyofanywa na majangili .Ujangili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla badala ya kupungua ndio kwanza unashika kasi,na kufikia hatua ya kutungua hata vyombo vya anga.

Kitu kibaya zaidi majangili wameungana na magaidi.Ushauri wangu kwa Mh. Maghembe..kama tumeshindwa Kupambana na majangili basi ni wakati muafaka Tanzania ianze kuwapa mafunzo wanyama pori ,wajilinde wenyewe. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kufundisha wanyama .Wengi tunaufahamu mradi wa panya wa kutegua mabomu.Mradi huu umesaidia sana katika nchi zilizo tumbukia katika vita na kubaki na maelfu ya mabomu ardhini.
Kama inavyoonekana katika picha ya nyani hapo juu aliepewa mafunzo ya kuwalinda nyani wenzie pamoja na faru dhidi ya maadui .. hususan binadamu..Tunaweza tukaanza na battalion moja ya nyani wenye IQ ya kushika mafunzo...kama nyani huyu wa South Africa aliepewa kazi ya kulinda faru na kampuni iliyompa mafunzo na kumuajiri... na sasa kampuni hii inalipwa fedha nyingi.