Profesa Lipumba amshambulia Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Lipumba amshambulia Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshume Kiyate, Mar 15, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba, amemshambulia Rais Jakaya Kikwete kuwa hajali matatizo ya wananchi pindi yanapojitokeza mazito ya Kitaifa.
  Akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Mwanga Centre mkoani Kigoma juzi, Profesa Lipumba alisema rais anapaswa kuwa makini na kuonyesha misingi bora ya uongozi.
  Rais wetu amekuwa akichezewa ovyo na watu na kutukanwa bila sababu za msingi, hali hii inasababishwa na rais kutokuwa makini. kwa bahati mbaya sana, ana udhaifu wa kutokuwa makini, jambo linalofanya baadhi ya watu kupoteza imani naye na kumuona kama mfano mbaya wa kiongozi wa nchi.
  Rais amekuwa hajali matatizo ya wananchi na kutoa mfano wa milipuko ya makombora ya Gongo la Mboto.
  Baada ya kutokea milipuko Rais aliondoka zake kwenda Ulaya, kama rais anafanya safari kipindi kigumu kama hicho, ni wazi wananchi watapoteza imani naye, Profesa alisema Rais Kikwete alikimbia wageni kutoka nchi mbalimbali kutazama fursa za uwekezaji, lakini Rais aliondoka kwenda nje.
  Mwananchi Machi 15 2011
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Huyu muheshimiwa nimeshindwa kumuelewa. Kwasasa wapo pamoja na CCM, hivyo ndiyo wanaoendesha serikali hii mbovu. Na tumeshuhudia akiwakandia CDM tukamuelewa kuwa wao si wapinzani tena. Sasa inakuwaje tena kumshambulia JK? Sasa tuwaweke kundi gani?
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,620
  Trophy Points: 280
  mbatia,lipumba na kikwete lao moja kuipoteza CHADEMA. lipumba,kile kitbu cha sera za cuf mlichompa alisha fanya kazi?
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,411
  Likes Received: 1,865
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu hayumo kwenye serekali ya umoja wa kitaifa?
   
 5. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Lipumba hana Jipya la kuwaeleza watanzania, yeye ni mvurugaji na ni ndumila kuwili anajaribu kujionyesha kwa wananchi kwamba yeye ni mpinzani wa kweli ilihali yeye ni CCM B, ameishiwa sera apishe na wengine sasa, Miaka 20 ya kugombea urais na sera zile zile, mawazo yale yale na maneno ni hayo hayo.

  Hawa wanaona wivu Jinsi wenzao Chadema walivyojipanga na kuteka watu wengi, nafikiri wanajaribu kuwagawa wananchi kwa maslahi ya CCM, kama kweli wao yani Lipumba na Mbatia ni watu wanaoitakia mema nchi hii waachane na kila kitu nao wakifuate chama cha ukombozi Chadema. na sio kwenda kwa wanachi wakilaumu JK and CCM na wakati wanawatuma wabunge wao kupinga kila kitu cha Chadema Bungeni.

  Watu wa namna hii ni wakuogopa kama Ukoma!
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mi sidhani kama lipumba anamshambulia Kikwete, ni wazi kaona kapoteza mvuto kwa wananchi. Ni wazi lipumba na CUF wamepoteza hadhi yao kama chama cha upinzani kwa liason yao na sisiem.
  Anatafuta namna ya kurudi kwenye siasa. His days are gone.
   
 7. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu Prof vipi? Anasema watu wanamtukana JK halafu yeye anasema rais ana udhaifu wa kutokuwa makini. Je hili sio tusi? Au tusi mpaka liweje? Au tusi ni mpaka mtu aseme kuwa mtu huyu ni mp****vu. CDM wamekuwa wakisema hayohayo wao wanaambiwa wanamtukana rais. Wamekuwa wanasema serikali siyo makini wanaambiwa wanikejeli serikali. Je, kwa hili la Profesa limekaaje?
   
 8. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hapana jamani tusimjaji Prof wa Uchumi kwa ndoa yake na ccm,ingawaje wapo ubia na ccm lakini zaidi ni zanzibar na sio hapa bara kwani kama ingekuwa na bara basi tungeona ndani ya uongozi wa serikali ya sasa pia wana cuf wangekuwepo
  kwa hiyo yupo huru na ana haki ya kusema kama katiba inavyo mruhusu mtu yeyote kutoa maoni,

  sema Prof wa ukweli ipo siku tu watakusikia
  Tatizo letu wana jf tunataka waseme CDM hapo ndipo tunapo pishana,akisema wa chama kingine kaishiwa sera,kweli tutafika kweli?

  tuwaache wana siasa wafanye kazi zao sisi sio majaji bana ama waaaaaaaaamuzi wa nani aseme na nani asiseme
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Amenukuliwa vibaya au?? Anasema kikwete anadharauliwa na kutukanwa BILA SABABU ZA MSINGI, wakati huohuo anataja mapungufu ya kikwete ambayo ndiyo yanamfanya adharauliwe!! Anataka nini sasa, watu waache kumkosoa kikwete au wafanyeje???
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Soon bara itakuwa kama ZNZ CDM watakuwa pamoja na CCM kwa ajili ya kuleta tija na kuondoa uhasama anza kutafuta chama cha kuendeleza ligi mapemaaaaa...............
   
 11. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Katumwa na maaskofu huyo, LOL!!!!!!!!!!!!!????
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tuombeane maisha bwana Mohammed kulidhihirisha hili, ingawa sikuchangia mada husika kwa ajili ya kuendeleza ligi. Lakini nataka nikujulishe (nikujuze), sehemu nyingi walipoafikiana kuendesha serikali ya mseto hapajakuwa na mafanikio na wala makubaliano ya kweli. Mfano wa Karibu ni majirani zetu Kenya ama Zimbabwe.
   
 13. G

  Godwine JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi CUF na CCM hazijaungana kabisa? lakini seif shalifu kwanini kamtosa lipumba kiasi cha kutokuwa na kazi ya kufanya
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Unajua kutetea kitu cha uongo ni kazi kwelikweli inahitaji uwe na akili sana.

  Lipumba anasema rais anatukanwa bila sababu za msingi baada ya dk1 anasema rais hayuko makini huyohuyo anasema tena rais hajali matatizo ya wananchi kwa hiyo kutojali matatizo ya wananchi siyo sababu za msingi.
   
 15. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  mbona hata mke na mume cku nyingine utofautiana katika mitazamo na vipaumbele mama anaweza kuongea ila mume atabak kua mume na fianal say. hao c wameoana
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  aaaaaaaaaah!! na mke na mme.....lol
   
 17. M

  Mtaalaamuna Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusema ule ukweli ni kwamba CUF bara wamewekwa njia panda, wanajaribu kubembeleza serikari na wakati huo huo wasionekane kama ccm B mbele ya wapinzani wenzao, kwa namna hii kauli zitokazo zina ashiria anawabeza wanaotoa maneno ya kejeli kwa prezda na wakati huo kutaka kumshauri awe makini. Hapa anajichanganya. Tunamtaka Lipumba awe wa MOTO au wa BARIDI ili tujue yuko upande gani.
   
 18. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  huyu jamaa ni ndumi la kuwili anataka JK amkubali at the same time wananchi wamkubali.. tumuogope kama ukoma.
   
 19. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ngangari +
  jino kwa jino
  = CCM B
   
 20. G

  Gathii Senior Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huo ndio ukweli ulivyo;CUF wamejiweka katika hali ngumu sana kwa kukubali kushirikiana na CCM Zanzibar wakati huo huo wao ni wapinzani
  ..kwa binadamu yeyote aliye timamu hii inakuwa ngumu kuelewa,maana itafika kipindi watahitaji kuwa pande zote mbili katika kufanya maamuzi,kwangu ni kichekesho kidogo.
   
Loading...