Profesa Lipumba amshambulia Rais Kikwete

Unajua kutetea kitu cha uongo ni kazi kwelikweli inahitaji uwe na akili sana.

Lipumba anasema rais anatukanwa bila sababu za msingi baada ya dk1 anasema rais hayuko makini huyohuyo anasema tena rais hajali matatizo ya wananchi kwa hiyo kutojali matatizo ya wananchi siyo sababu za msingi.

Mkuu
Wenzako huwa wanafanya Quote kwenye posts lakini wewe kwenye hii post umefanya Quotability na Quothe
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba, amemshambulia Rais Jakaya Kikwete kuwa hajali matatizo ya wananchi pindi yanapojitokeza mazito ya Kitaifa.
Akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Mwanga Centre mkoani Kigoma juzi, Profesa Lipumba alisema rais anapaswa kuwa makini na kuonyesha misingi bora ya uongozi.
Rais wetu amekuwa akichezewa ovyo na watu na kutukanwa bila sababu za msingi, hali hii inasababishwa na rais kutokuwa makini. kwa bahati mbaya sana, ana udhaifu wa kutokuwa makini, jambo linalofanya baadhi ya watu kupoteza imani naye na kumuona kama mfano mbaya wa kiongozi wa nchi.
Rais amekuwa hajali matatizo ya wananchi na kutoa mfano wa milipuko ya makombora ya Gongo la Mboto.
Baada ya kutokea milipuko Rais aliondoka zake kwenda Ulaya, kama rais anafanya safari kipindi kigumu kama hicho, ni wazi wananchi watapoteza imani naye, Profesa alisema Rais Kikwete alikimbia wageni kutoka nchi mbalimbali kutazama fursa za uwekezaji, lakini Rais aliondoka kwenda nje.
Mwananchi Machi 15 2011

Yes, aaah samahani ndiyo!. Unajua Mh. Lipumba ni mchumi makini anapokuja kusema hadharani ili kutoa maoni yake kwa kweli tumuache aseme kile ambacho kina maslahi kwa Taifa bila kujali kama yuko kwenye serikali ya UMOJA WA KITAIFA au lah.

Lipumba ni mtanzania mwenzetu na ni mchumi makini na alichokisema naomba kiingie akilini mwa watawala wetu ambao wanapenda matanuzi kuliko kujali utaifa wetu na hasa raia wa Taifa hili.

Mimi binafsi kutokana na kauli ya Profesa Lipumba najifunza kitu kifuatacho nacho ni kimoja tu;
TANZANIA NI NCHI RAHISI ZAIDI KUITAWALA KULIKO NCHI ZOTE DUNIANI!!!.

Kwa nini nasema hivi?. Hebu tazama tulivyo sasa;
1. Kulitokea milipuko ya mabomu ya mbagala - wote tulisema tulichoweza mpaka tukapitiliza japo hadi leo kuna baadhi ya ndugu zetu hawana mahali pa kulala, hawajui hatma yao na hakuna wa kuwasemea tena!. JE WATANZANIA TUMESAHAU HILI???.

2. Baada ya Mbagalla ukatokea wimbo mpya wa RICHMOND, DOWANS, IPTL, TANGOLD, MEREMETA, KIWILA, BOMOA BOMOA YA KIPAWA NK.- Hapa tukasahau ya Mbagala wote kwa umoja wetu tukaimba wimbo huu RICHMOND, RICHMOND, RICHMOND mpaka Bunge likaunda tume ya MWAKYEMBE ikafanyakazi yake hatimaye Mh. Lowasa akajiuzulu pamoja na Mh. Msabaha na yule Mh. Karamagi. Kazi ikawa inaendelea ya kumsaka huyu RICHMOND ambaye hadi sasa hajapatikana na nchi iko gizani, mgao wa umeme kila siku, umaskini unaongezeka na mfumuko wa bei hausemeki tena. JE HATA HILI NALO TUMESAHAU TAYARI????.

Wakati tunaendelea na kutafuta suluhisho hili la kupata umeme na watu wengine wakiwa bado wana vidonda vya RICHMOND bado vibich havijapona kabisa na tukiwa tunavutana JE DOWANS ALIPWE AU ASILIPWE!!!!, ghafla tu mambo yanageuka tunaingia katika wimbo wa tatu yaaani,
3. Milipuko ya Mabomu ya GONGO LA MBOTO ambayo bado hata machozi ya kuwalilia ndugu zetu hayajakauka, hawana pa kulala na hata baadhi ya waliopotea hatujawapata, kila TV, REDIO, MAGAZETI, NK yaliandika habari hii hivyo kutusahaulisha kila kitu kama MBAGALA, RICHMOND/DOWANS NK. na wimbo ukawa GONGO LA MBOTO, GONGO LA MBOTO, GONGO LA MBOTO ambao kabla hata watu hawajawajibika na kupewa tathimini ya kina juu ya upotevu wa ndugu zetu na mali zao, ghafla tu!!

4. BABU WA LOLIONDO kaja kwa kasi ya ajabu hata mimi natamani kwenda loliondo kibaya zaidi hata GONGO LA MBOTO tumeshasau mara hii tu!! jamani amka Watanzania nchi yetu haitajengwa tukilala fofofo namna hii!!.

MIMI SIJUI KESHO KITATOKEA NINI BAADA YA LOLIONDO???. BIG UP PROF. LIPUMBA JAPO WEWE SI MWANA CDM LAKINI UMETUKUMBUSHA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
huyu muheshimiwa nimeshindwa kumuelewa. Kwasasa wapo pamoja na ccm, hivyo ndiyo wanaoendesha serikali hii mbovu. Na tumeshuhudia akiwakandia cdm tukamuelewa kuwa wao si wapinzani tena. Sasa inakuwaje tena kumshambulia jk? Sasa tuwaweke kundi gani?

huyo ndie prof lipumba kama jina lake. Hajui yuko wapi, anaishi oxygen ipo basi inatosha
 
Ndoa nyingine ngumu sana, cuf bara hakina nguvu ni kama kimemezwa kwani wanashindwa kujielewa wawajibike wapi ndyo maana wanahangaika kutafuta ushirika na vyama vingine na ninakuhakikishia mapenzi ya cuf na nccr hayatadumu
 
Yes, aaah samahani ndiyo!. Unajua Mh. Lipumba ni mchumi makini anapokuja kusema hadharani ili kutoa maoni yake kwa kweli tumuache aseme kile ambacho kina maslahi kwa Taifa bila kujali kama yuko kwenye serikali ya UMOJA WA KITAIFA au lah.

Lipumba ni mtanzania mwenzetu na ni mchumi makini na alichokisema naomba kiingie akilini mwa watawala wetu ambao wanapenda matanuzi kuliko kujali utaifa wetu na hasa raia wa Taifa hili.

Mimi binafsi kutokana na kauli ya Profesa Lipumba najifunza kitu kifuatacho nacho ni kimoja tu;
TANZANIA NI NCHI RAHISI ZAIDI KUITAWALA KULIKO NCHI ZOTE DUNIANI!!!.

Kwa nini nasema hivi?. Hebu tazama tulivyo sasa;
1. Kulitokea milipuko ya mabomu ya mbagala - wote tulisema tulichoweza mpaka tukapitiliza japo hadi leo kuna baadhi ya ndugu zetu hawana mahali pa kulala, hawajui hatma yao na hakuna wa kuwasemea tena!. JE WATANZANIA TUMESAHAU HILI???.

2. Baada ya Mbagalla ukatokea wimbo mpya wa RICHMOND, DOWANS, IPTL, TANGOLD, MEREMETA, KIWILA, BOMOA BOMOA YA KIPAWA NK.- Hapa tukasahau ya Mbagala wote kwa umoja wetu tukaimba wimbo huu RICHMOND, RICHMOND, RICHMOND mpaka Bunge likaunda tume ya MWAKYEMBE ikafanyakazi yake hatimaye Mh. Lowasa akajiuzulu pamoja na Mh. Msabaha na yule Mh. Karamagi. Kazi ikawa inaendelea ya kumsaka huyu RICHMOND ambaye hadi sasa hajapatikana na nchi iko gizani, mgao wa umeme kila siku, umaskini unaongezeka na mfumuko wa bei hausemeki tena. JE HATA HILI NALO TUMESAHAU TAYARI????.

Wakati tunaendelea na kutafuta suluhisho hili la kupata umeme na watu wengine wakiwa bado wana vidonda vya RICHMOND bado vibich havijapona kabisa na tukiwa tunavutana JE DOWANS ALIPWE AU ASILIPWE!!!!, ghafla tu mambo yanageuka tunaingia katika wimbo wa tatu yaaani,
3. Milipuko ya Mabomu ya GONGO LA MBOTO ambayo bado hata machozi ya kuwalilia ndugu zetu hayajakauka, hawana pa kulala na hata baadhi ya waliopotea hatujawapata, kila TV, REDIO, MAGAZETI, NK yaliandika habari hii

Hujaeleka mwanzo mwisho na font uliyotumia inatia uvivu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba, amemshambulia Rais Jakaya Kikwete kuwa hajali matatizo ya wananchi pindi yanapojitokeza mazito ya Kitaifa.
Akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Mwanga Centre mkoani Kigoma juzi, Profesa Lipumba alisema rais anapaswa kuwa makini na kuonyesha misingi bora ya uongozi.
Rais wetu amekuwa akichezewa ovyo na watu na kutukanwa bila sababu za msingi, hali hii inasababishwa na rais kutokuwa makini. kwa bahati mbaya sana, ana udhaifu wa kutokuwa makini, jambo linalofanya baadhi ya watu kupoteza imani naye na kumuona kama mfano mbaya wa kiongozi wa nchi.
Rais amekuwa hajali matatizo ya wananchi na kutoa mfano wa milipuko ya makombora ya Gongo la Mboto.
Baada ya kutokea milipuko Rais aliondoka zake kwenda Ulaya, kama rais anafanya safari kipindi kigumu kama hicho, ni wazi wananchi watapoteza imani naye, Profesa alisema Rais Kikwete alikimbia wageni kutoka nchi mbalimbali kutazama fursa za uwekezaji, lakini Rais aliondoka kwenda nje.
Mwananchi Machi 15 2011

nzuri sana ..ila anapokuwa anamkanusha rais wake awe anawaambia kabisa watanzania kubwa suluhu ni DR.SLAA
 
@ Iyimo kwani unatumia kipimo gani kujua kama serikali ya mseto imefanikiwa au la? Nahisi kipimo chako ni kibovu na hakiko standard. Kwani kama si mseto kenya wakikuyu si wangalitoweka ktk ramani ya dunia? Kama si mseto zimbabwe walemavu leo si wangali zidi? Kama si mseto znz watu si wangali uliwa kwenye uchaguzi?

Tulia nyie chadema watoto wadogo tu ktk siasa, muacheni hamad rashid awafundishe siasa. Et the end mnatamani muwemo ktk serikali ya mseto lkn hamumo. Wananchi ndio wanaoamua ni mfumo gani wa utawala wanataka na znz kura ya maoni ilipita kwa 64% mbona chadema muna wivu wa kike nyie.
 
Huyu na alolaumiwa tofauti zao ni majina tu na si tabia wala msimamo!
 
Achaneni na huyo profesa asiyejua chochote. Subirini msomi mwenyewe anayejua mambo Padri Slaa aseme nasi tumeze kama dodoki au sponji!!
 
Back
Top Bottom