Profesa Kitila Mkumbo amchana Humphrey Polepole

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,779
Reaction score
29,351
‪Kijana wangu Humphrey Polepole anapaswa kuelewa kuwa kazi ya chini kabisa (minimum responsibility)ya upinzani katika nchi ya kidemokrasia ni kuikosoa na kuizodoa serikali na chama kilichopo madarakani.

Mengine yote yanajengwa katika msingi huu.Kwa upinzani kuisifia serikali ni hiari lakini sio wajibu.

‬Sasa yeye kama Katibu wa Uenezi wa chama tawala kuitisha press conference kwa lengo la kulaumu upinzani kwa sababu unaikosoa na kuizodoa serikali ni kosa la kimantiki.

Yeye ajikite kujenga hoja za kutetea chama na maamuzi na matendo ya serikali pale bila kuzuia upinzani kufanya kazi yake ya kuzodoa kwa sababu hawezi kuzuia.

Naamini kijana wetu huyu hatapoteza umahiri wa kujenga hoja kama tumjuavyo.

Bado naendelea kuamini kuwa katika teuzi ambazo Mwenyekiti na Rais Magufuli alipatia sana ni pamoja na kumteua Ndugu Polepole kwa nafasi hii.

Abaki tu katika mstari wa kujenga hoja.

My take : Huenda Polepole ametishwa mzigo unaomlemea. Siyo makosa yake bali ya aliyemtwisha.
 
Ngoja ninywe bia kwanza nipate sitimu nitakuja
Unajua maaana ya kuchanwa ww mpunga wa ufipa kinondoni
 


Kama ni kweli haya ni maneno ya huyo Kitila Mkumbo basi na yeye namshangaa pia, kwani cheo cha H. Polepole ni kipi? Na kazi yake ni ipi, ndani ya CCM?
 
Siku zote mpinzan ni sawa na leso, na kazi ya leso ni kufuta uchafu,sasa slow slow anataka leso isifute uchafu itunzwe tu mfukoni hata kama unaonekana kwa macho?.
 
Kama ni kweli haya ni maneno ya huyo Kitila Mkumbo basi na yeye namshangaa pia, kwani cheo cha H. Polepole ni kipi? Na kazi yake ni ipi, ndani ya CCM?
Unamshangaa kwa lipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…