Profesa Kabudi, Tanzania imewahi kushindwa vita nyingi tu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Nilimsikiliza Profesa Kabudi akijimwambafy, akizungumza kwa kujitapa kabisa kuwaambia wahisani wetu kuwa Tanzania iko imara, haibabaishwi na misaada yao na kwamba sisi kama Taifa tunaweza kushinda vita zetu maana hatujawahi kushindwa vita!.

Kabudi ameongea hayo aakijaribu kutuma meseji kwa jumuia ya Ulaya kuwa serikali ya Magufuli haikufurahishwa na hatua yao kuukosoa vikali uchaguzi uliofanyika majuzi ambao uligubikwa na dosari nyingi sana.

Kabudi anajaribu kucheza karata ya uzalendo ili kulifanya Taifa liungane nao katika kikaango hiki ambacho wao serikali wamekikalia baada ya kumess up kwa kuendesha zoezi lilojaa kila aina ya udanganyifu (fraud) na kufuatiwa na uvunjifu wa kutisha wa haki za binadamu hususan huko Zanzibar ambapo kuna wananchi wameuawa, kuteswa, na kuumizwa vibaya katika zoezi zima la uchafuzi lilioendeshwa kibabe kabisa bila kujali wala kuheshimu wananchi.

Hata hivyo nataka nimkumbushe Kabudi kuwa siyo kweli kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita, tena vita kubwa tu na kila awamu Tangu ya Nyerere hadi Magufuli zimeshindwa vita nyingi tu. Labda Kabudi anafikiri vita ni ya kubeba bunduki tu, hiyo ni aina moja ya vita lakini zipo nyingine nyingi tu!

Hizi zifuatazo ni baadhi ya vita tulizoshindwa

1. Tumeshindwa vita ya kuondoa umasikini
Mpaka hivi sasa zaidi ya Asilimia 50 ya wananchi wanaishi chini ya dola mbili kwa siku, Idadi ya masikini imeongezeka kutoka watu milion 13 mwaka 2007 hadi milioni 14 mwaka 2019, na kwa kila Watanzania wanne wanaotoka katika umasikini kuna wengine watatu wanaingia katika umasikini!

Kwa vigezo vyote huku siyo kushinda vita, ni kushindwa vita maana kwa standard zote tukilinganisha na nchi nyingine za Asia kama vile Singapore ambazo tulikuwa katika viwango vinavyokaribiana mwaka 1964 ni dhahiri wenzetu wameshinda vita ya umasikini wakati Sisi Umasikini unaendelea kutugalagaza, Sasa Kabudi unaposema Tanzania haijawahi kushindwa vita yoyote unamaanisha nini?. Leo bado tuna mamilioni ya watoto waliodumaa kwa kukosa lishe bora. Nchi ya miaka 70 ina mamilioni ya watoto wadumavu kwa ukosefu wa lishe

2. Tulishindwa vita ya kujenga ujamaa nchini
Mwaka 1967 hadi 1989 tulipambana kujenga Taifa la Kijamaa, tulisema tunapambana na unyonyaji, ukabaila , ubwanyenye, n.k lakini tukasanda

Leo wale waliokuwa Mabingwa wa kuvaa suti za cho-enlai na kubeba vijitabu vya mwalimu vya "Ujamaa na kujitegemea", "Tujisahihishe", "Azimio la Arusha" n.k ndiyo leo hii ni watu wazima, wengine wanamiliki maelfu na maelfu ya ekari za ardhi hata kwenye mikoa ambayo wananchi wanapigana wakulima na wafugaji kwa sababu ya uhaba wa ardhi.

Leo tunaishi katika nchi wastaafu wenye miaka 95 na 70 wanajengewa majumba mithili ya mahekalu na makasri halafu tukiuliza tunaambiwa eti ni haki ya maraisi wastaafu kujengewa nyumb!. Hivi Ali alipostaafu hakuwa na nyumba?, aliishi wapi miaka yote hiyo 25 ya kustaafu kwake mpaka eti John Msamaria amuonee huruma na kumjengea hekalu leo hii.

Hivi Jakaya huko Msoga anaishi kwenye kichuguu?, iweje leo John msamaria mwema atwae pesa za wananchi na kumjengea kasri kubwa. Ujamaa tulishindwa sasa tunaishi kibepari huku kwenye katiba yetu tukijidanganya kwa kusema eti hii ni nchi ya kijamaa!

3. Tumeshindwa vita ya kuondoa dhulma katika nchi na kujenga Taifa la taasisi imara na la kidemokrasia
Leo wapinzani wanavamiwa na kupigwa mapanga na kuuawa (Kamanda Mawazo), kupigwa risasi(Lissu), kupotea mazima(Ben Saanane), hakuna uchunguzi wala ripoti za serikali kuhusu matukio hayo. Hatuoni Jitihada za serikali katika kudeal na masuala hayo.

Tumeona vita ya kujenga demokrasia katika nchi ikifeli vibaya, genge la watu wachache wenye kushika madaraka ya kidola hayataki demokrasia katika nchi, linavuruga chaguzi, linakwamisha jitihada za kupatikana kwa katiba bora ya kuendeshea nchi, limeteka taasisi za kidola kwa manufaa yake binafsi badala ya manufaa ya nchi kiujumla. Vita ya kujenga demokrasia imefeli na sasa tunarudisha nyuma saa kuelekea kule tulipokuwa kwenye utawala wa mtu mmoja na chama chake kushika hatamu badala ya taasisi imara.

Ukiachilia mbali na hapo, hata vita ya kupambana na ufisadi nayo inatuelemea. Leo hii tuna wabunge waliopita kwenye kura za maoni za chama chao kwa kutoa rushwa, kisha wakashindishwa kibabe baada ya kupora maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura.

Katika mazingira hayo ambapo una bunge la watu corrupt, litawezaje kupambana kuondoa corruption nchini wakati lenyewe lina mzizi kwenye corruption?. Hii vita ya kuondoa dhulma na kujenga taifa la haki imetushinda. Tumegeuka Taifa la watu wadogowadogo tu kwa sababu ya kuweka pembeni nyingi ya values zinazofanya mataifa yawe imara na yaheshimike duniani!

WATU GANI WAMETUFIKISHA HAPA?
1. Ni wasomi wa dizaini ya akina Kabudi

Wasomi wa aina ya Kabudi wanaangalia maslahi yao kwanza huku wakijificha kwenye kichaka cha uzalendo. Ni miaka michache tu huyu Kabudi alikuwa akipigia chapuo katiba mpya, na kwa ustadi mkubwa alichambua na kuelezea namna katiba ya sasa ilivyombaya na kwamba haisaidii kujenga muungano imara, lakini leo hii ni upi msimamo wake kwenye katiba?, ni flip-floping.

Wakati ule alitwambia raisi wa Muungano hana authority yoyote huko Zanzibar, alivyoingia serikalini anasema raisi wa Muungano ana mamlaka sehemu zote za Muungano

Kuna huyu msomi mwingine anaitwa Bashiru Ally, yeye kwenye TV alisikika akisema kuwa Katiba hii haikidhi haja ya muafaka wa kitaifa wa vyama vingi, lakini leo hii ni katibu mkuu wa chama aliyeshindwa kuisemea haja ya uwepo wa katiba nchini.

Mifano hii miwili ya aina ya wasomi, ndiyo tatizo kubwa la nchi hii, ndiyo maana tunafeli kwenye vita nyingi nilizoziorodhesha huko juu

2. Mahakama na Taasisi za usalama
Unapokuwa na Mahakama ambayo inatoa maamuzi ambayo ni dhahiri unayaona ni ya kuilinda serikali na watu wake, mfano kesi zote za kikatiba dhidi ya watawala wa sasa mahakama imekuwa ndiyo kinara wa kuziminya kwa ajili ya maslahi ya wanasiasa wachache (rejea ishu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi, kesi dhidi y utenguzi wa CAG, Kesi ya Mgombea binafsi na nyinginezo nyingi), mahakama imekuwa ikisiamama na watawala badala ya haki na maslahi ya taifa. Ni as if mahakama nayo imekuwa tawi la genge fulani hivi la wanasiasa.

Katika nchi yenye mahakama isiyotambua jukumu lake la kujenga Taifa lenye haki, ni dhahiri vita nilizozisema huko juu zitafeli big time.
Kadhalika ukija kwenye Taasisi ya usalama ambayo utendaji wake wa kazi uko biased kwa kupendelea chama tawala, au watawala, ni dhahiri ni vigumu sana kujenga taifa lenye haki, na kwa matokeo yake tutaendelea kupata viongozi "waliowezeshwa kuwa hapo" badala ya Taifa la watu huru wenye utashi na mamlaka ya kuweka madarakani vyama na watu kutokana na merits zao.

Uchaguzi wa mwaka huu ni kioo cha kuangalia namna taasisi za serikali na usalama zinavyoweza kuteam up kuibaka demokrasia, kuwadhulumu wananchi chaguzi zao.

Sasa Kabudi anataka kutwambia nini?
Huenda Kabudi yeye binafsi ameshinda vita yake ya njaa, basi anaamini Taifa limeshida vita ya umasikini, maradhi na Ujinga!
 
Halafu neno MABEBERU ni hatari sana kulitumia ni sawa wewe mpangaji unamtukana mwenye nyumba
1. Muna mbuga kama Serengeti mtaenda kutalii wewe na mkeo?
2. Muna mazao ya biashara kama korosho mtanunua wewe na mkeo?
3. Muna madini mtayanunua wewe na mkeo?

Mzee Nyerere aliwaita MABEBERU. wakaiporomosha bei ya Mkonge (katani) haijapanda hadi leo.
Nyerere Mabeberu
Mwinyi Wahisani au wafadhili
Mkapa wawekezaji
Kikwete Wadau wa maendeleo
Magufuli Mabeberu?????????
Ni nani alimtukana BEBERU akasalimika?
Kwame Nkurumah
Patrick Lumumba
Muamar Gaddafi
Sadam Hussein
Mgabe- mashamba wanarudisha kwa wenyewe na fidia juu
Pia wamo Mapank wa korea kaskazini
Pia yupo Hugo ShAVEZ wa Venezuela
Walijitahidi kidogo Fidel CASRO CUBA na Yasser Arafat - hawa wawili waliwawatukana tukana mabeberu kiasi

Nyie nyie nyie chungeni midomo yenu. Kabla hujavuka mto usitukane mamba wakale walisema
 
Kwa ujumla Kabudi nikimsikikiza, ni vigumu sana kufikiria kama ana hata shahada moja. Ni mtu anayeamini kuwa anajua sana lakini ni zero thinking brain. Kikubwa anachokijua ni kukariri matukio ya kihistoria na unafiki wa kujipendekeza.

Yaliyoorodheshwa ni mchache, nina uhakika kama Taifa tumeshindwa mengi kuliko tuliyoshinda.

Miaka ya 1960 tulikuwa sawa na Singapore, Malaysia na Thailand. Angalia waliko wenzetu leo na sisi tuliko! Halafu mtu anayejiita eti msomi, bila aibu anasimama na kuropoka eti hatujawahi kushindwa.

Kabudi, kwa vile anapenda historia, akatazame mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka 5, ambao tulishindwa kuutekeleza kwa 75%. Kilimo kwanza cha Pinda kilifanikiwa kwa asilimia ngapi? Magufuli na Tanzania ya viwanda, ameshinda nini?
 
Halafu kingine ni nani aliowaambia wawajibu wazungu wakati bado hata hawajaulizwa!?
Bunge la eu limeulizana wao kwa wao lakini kwa kiherehere cha kutojua kitu wameanza kujibu huku kila mmoja anajibu kivyake
Hivi kabudi ameongea kwa kuwawakilisha akina nani?
Taifa au chama chake cha sisiemu?
 
Hata vita ya Uganda bila kuwakuta Tito okelo na museveni Msituni wameasi wakawasaidia jwtzccm kupigana kuwaonyesha njia wasingeshinda kamwe, Kule msumbiji walishindwa vita na waasi wa msumbiji wakauawa kwa wingi mpaka ikabidi warejeshe jeshi Tanzania, vita zote hushindwa hata uchaguzi mkuu wameshindwa lakini NECCCM Tumeccm wakurugenziccm na Polisiccm wameulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani
 
Nilimsikiliza Profesa Kabudi akijimwambafy, akizungumza kwa kujitapa kabisa kuwaambia wahisani wetu kuwa Tanzania iko imara, haibabaishwi na misaada yao na kwamba sisi kama Taifa tunaweza kushinda vita zetu maana hatujawahi kushindwa vita!...
Sio CCM imeshindwa?
 
Huyu si kabudi ni Kibudu maiti kwenenda ni jipu kubwa sana tena lishaiva lispotumbuliwa litawatumbukia.
 
Halafu kingine ni nani aliowaambia wawajibu wazungu wakati bado hata hawajaulizwa!?
Bunge la eu limeulizana wao kwa wao lakini kwa kiherehere cha kutojua kitu wameanza kujibu huku kila mmoja anajibu kivyake
Hivi kabudi ameongea kwa kuwawakilisha akina nani?
Taifa au chama chake cha sisiemu?
Waligawana pesa za corona pasipo kujipanga kujua kuwa ipo siku kitanuka na watoa pesa kudai rist, mda huu wapo busy kutengeneza visingizio na matumizi feki mojawapo lazima watasema zilitumika mwananyamala ilala na mloganzila , CCM kwenye ufisadi unaowagusa hawaoni tatu kutengeneza matumizi hewa ili kuharalisha wizi wao.
 
Huyu si kabudi ni Kibudu maiti kwenenda ni jipu kubwa sana tena lishaiva lispotumbuliwa litawatumbukia.
Kumtumbua anaona Aibu kwani pesa zote wamegawana zikiwemo pesa za msaada wa uchakachuaji tokea Serikali ya China
 
Nilimsikiliza Profesa Kabudi akijimwambafy, akizungumza kwa kujitapa kabisa kuwaambia wahisani wetu kuwa Tanzania iko imara, haibabaishwi na misaada yao na kwamba sisi kama Taifa tunaweza kushinda vita zetu maana hatujawahi kushindwa vita!.

Kabudi ameongea hayo aakijaribu kutuma meseji kwa jumuia ya Ulaya kuwa serikali ya Magufuli haikufurahishwa na hatua yao kuukosoa vikali uchaguzi uliofanyika majuzi ambao uligubikwa na dosari nyingi sana.

Kabudi anajaribu kucheza karata ya uzalendo ili kulifanya Taifa liungane nao katika kikaango hiki ambacho wao serikali wamekikalia baada ya kumess up kwa kuendesha zoezi lilojaa kila aina ya udanganyifu (fraud) na kufuatiwa na uvunjifu wa kutisha wa haki za binadamu hususan huko Zanzibar ambapo kuna wananchi wameuawa, kuteswa, na kuumizwa vibaya katika zoezi zima la uchafuzi lilioendeshwa kibabe kabisa bila kujali wala kuheshimu wananchi.

Hata hivyo nataka nimkumbushe Kabudi kuwa siyo kweli kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita, tena vita kubwa tu na kila awamu Tangu ya Nyerere hadi Magufuli zimeshindwa vita nyingi tu. Labda Kabudi anafikiri vita ni ya kubeba bunduki tu, hiyo ni aina moja ya vita lakini zipo nyingine nyingi tu!

Hizi zifuatazo ni baadhi ya vita tulizoshindwa

1. Tumeshindwa vita ya kuondoa umasikini
Mpaka hivi sasa zaidi ya Asilimia 50 ya wananchi wanaishi chini ya dola mbili kwa siku, Idadi ya masikini imeongezeka kutoka watu milion 13 mwaka 2007 hadi milioni 14 mwaka 2014, na kwa kila Watanzania wanne wanaotoka katika umasikini kuna wengine watatu wanaingia katika umasikini!

Kwa vigezo vyote huku siyo kushinda vita, ni kushindwa vita maana kwa standard zote tukilinganisha na nchi nyingine za Asia kama vile Singapore ambazo tulikuwa katika viwango vinavyokaribiana mwaka 1964 ni dhahiri wenzetu wameshinda vita ya umasikini wakati Sisi Umasikini unaendelea kutugalagaza, Sasa Kabudi unaposema Tanzania haijawahi kushindwa vita yoyote unamaanisha nini?. Leo bado tuna mamilioni ya watoto waliodumaa kwa kukosa lishe bora. Nchi ya miaka 70 ina mamilioni ya watoto wadumavu kwa ukosefu wa lishe

2. Tulishindwa vita ya kujenga ujamaa nchini
Mwaka 1967 hadi 1989 tulipambana kujenga Taifa la Kijamaa, tulisema tunapambana na unyonyaji, ukabaila , ubwanyenye, n.k lakini tukasanda

Leo wale waliokuwa Mabingwa wa kuvaa suti za cho-enlai na kubeba vijitabu vya mwalimu vya "Ujamaa na kujitegemea", "Tujisahihishe", "Azimio la Arusha" n.k ndiyo leo hii ni watu wazima, wengine wanamiliki maelfu na maelfu ya ekari za ardhi hata kwenye mikoa ambayo wananchi wanapigana wakulima na wafugaji kwa sababu ya uhaba wa ardhi.

Leo tunaishi katika nchi wastaafu wenye miaka 95 na 70 wanajengewa majumba mithili ya mahekalu na makasri halafu tukiuliza tunaambiwa eti ni haki ya maraisi wastaafu kujengewa nyumb!. Hivi Ali alipostaafu hakuwa na nyumba?, aliishi wapi miaka yote hiyo 25 ya kustaafu kwake mpaka eti John Msamaria amuonee huruma na kumjengea hekalu leo hii.

Hivi Jakaya huko Msoga anaishi kwenye kichuguu?, iweje leo John msamaria mwema atwae pesa za wananchi na kumjengea kasri kubwa. Ujamaa tulishindwa sasa tunaishi kibepari huku kwenye katiba yetu tukijidanganya kwa kusema eti hii ni nchi ya kijamaa!

3. Tumeshindwa vita ya kuondoa dhulma katika nchi na kujenga Taifa la taasisi imara na kidemokrasia
Leo wapinzani wanavamiwa na kupigwa mapanga na kuuawa (Kamanda Mawazo), kupigwa risasi(Lissu), kupotea mazima(Ben Saanane), hakuna uchunguzi wala ripoti za serikali kuhusu matukio hayo. Hatuoni Jitihada za serikali katika kudeal na masuala hayo.

Tumeona vita ya kujenga demokrasia katika nchi ikifeli vibaya, genge la watu wachache wenye kushika madaraka ya kidola hayataki demokrasia katika nchi, linavuruga chaguzi, linakwamisha jitihada za kupatikana kwa katiba bora ya kuendeshea nchi, limeteka taasisi za kidola kwa manufaa yake binafsi badala ya manufaa ya nchi kiujumla. Vita ya kujenga demokrasia imefeli na sasa tunarudisha nyuma saa kuelekea kule tulipokuwa kwenye utawala wa mtu mmoja na chama chake kushika hatamu badala ya taasisi imara.

Ukiachilia mbali na hapo, hata vita ya kupambana na ufisadi nayo inatuelemea. Leo hii tuna wabunge waliopita kwenye kura za maoni za chama chao kwa kutoa rushwa, kisha wakashindishwa kibabe baada ya kupora maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura.

Katika mazingira hayo ambapo una bunge la watu corrupt, litawezaje kupambana kuondoa corruption nchini wakati lenyewe lina mzizi kwenye corruption?. Hii vita ya kuondoa dhulma na kujenga taifa la haki imetushinda. Tumegeuka Taifa la watu wadogowadogo tu kwa sababu ya kuweka pembeni nyingi ya values zinazofanya mataifa yawe imara na yaheshimike duniani!

WATU GANI WAMETUFIKISHA HAPA?
1. Ni wasomi kama Kabudi

Wasomi wa aina ya Kabudi wanaangalia maslahi yao kwanza huku wakijificha kwenye kichaka cha uzalendo. Ni miaka michache tu huyu Kabudi alikuwa akipigia chapuo katiba mpya, na kwa ustadi mkubwa alichambua na kuelezea namna katiba ya sasa ilivyombaya na kwamba haisaidii kujenga muungano imara, lakini leo hii ni upi msimamo wake kwenye katiba?, ni flip-floping.

Wakati ule alitwambia raisi wa Muungano hana authority yoyote huko Zanzibar, alivyoingia serikalini anasema raisi wa Muungano ana mamlaka sehemu zote za Muungano

Kuna huyu msomi mwingine anaitwa Bashiru Ally, yeye kwenye TV alisikika akisema kuwa Katiba hii haikidhi haja ya muafaka wa kitaifa wa vyama vingi, lakini leo hii ni katibu mkuu wa chama aliyeshindwa kuisemea haja ya uwepo wa katiba nchini.

Mifano hii miwili ya aina ya wasomi, ndiyo tatizo kubwa la nchi hii, ndiyo maana tunafeli kwenye vita nyingi nilizoziorodhesha huko juu

2. Mahakama na Taasisi za usalama
Unapokuwa na Mahakama ambayo inatoa maamuzi ambayo ni dhahiri unayaona ni ya kuilinda serikali na watu wake, mfano kesi zote za kikatiba dhidi ya watawala wa sasa mahakama imekuwa ndiyo kinara wa kuziminya kwa ajili ya maslahi ya wanasiasa wachache (rejea ishu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi, kesi dhidi y utenguzi wa CAG, Kesi ya Mgombea binafsi na nyinginezo nyingi), mahakama imekuwa ikisiamama na watawala badala ya wananchi. Ni as if mahakama nayo imekuwa tawi la genge fulani hivi la wanasiasa.

Katika nchi yenye mahakama isiyotambua jukumu lake la kujenga Taifa lenye haki, ni dhahiri vita nilizozisema huko juu zitafeli big time.
Kadhalika ukija kwenye Taasisi ya usalama ambayo utendaji wake wa kazi uko biased kwa kupendelea chama tawala, au watawala, ni dhahiri ni vigumu sana kujenga taifa lenye haki, na kwa matokeo yake tutaendelea kupata viongozi "waliowezeshwa kuwa hapo" badala ya Taifa la watu huru wenye utashi na mamlaka ya kuweka madarakani vyama na watu kutokana na merits zao.

Uchaguzi wa mwaka huu ni kioo cha kuangalia namna taasisi za serikali na usalama zinavyoweza kuteam up kuibaka demokrasia, kuwadhulumu wananchi chaguzi zao.

Sasa Kabudi anataka kutwambia nini?
Huenda Kabudi yeye binafsi ameshinda vita yake ya njaa, basi anaamini Taifa limeshida vita ya umasikini, maradhi na Ujinga!

Serekali isiyo badilika uwezi kubadili ikipitia chama kimoja chenye wana kabudi
 
Kwa ujumla Kabudi nikimsikikiza, ni vigumu sana kufikiria kama ana hata shahada moja. Ni mtu anayeamini kuwa anajua sana lakini ni zero thinking brain. Kikubwa anachokijua ni kukariri matukio ya kihistoria na unafiki wa kujipendekeza.

Yaliyoorodheshwa ni mchache, nina uhakika kama Taifa tumeshindwa mengi kuliko tuliyoshinda.

Miaka ya 1960 tulikuwa sawa na Singapore, Malaysia na Thailand. Angalia waliko wenzetu leo na sisi tuliko! Halafu mtu anayejiita eti msomi, bila aibu anasimama na kuropoka eti hatujawahi kushindwa.

Kabudi, kwa vile anapenda historia, akatazame mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka 5, ambao tulishindwa kuutekeleza kwa 75%. Kilimo kwanza cha Pinda kilifanikiwa kwa asilimia ngapi? Magufuli na Tanzania ya viwanda, ameshinda nini?
Kabudi kichwani kasalia na darasa la nne tu, alichosoma chote kimefutika sasa ni mtu anayeitwa aliwahi kuwa Msomi lakini alichokisoma kimefutika kichwani kabakia kuwa mbumbumbu juha zuzu kilaza wa kutupwa
 
Serekali isiyo badilika uwezi kubadili ikipitia chama kimoja chenye wana kabudi
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani kwa sababu ya CCM kutumia pesa za walipa kodi kwa mambo ya hovyo hovyo yasiyo na tija kwa Taifa
 
RAIS MSTAAFU INGILIA JAHAZI WE BELIEVE IN YOU JMK WANA WANATAKA KUZAMISHA JAHAZI KWELI IVO SISI NI WAKUTUNISHIANA MISULI NA HAWA KWELI KWELI
 
Vema mkuu Bonge la Analysis.

kabudi anashindwa kujibu maswali anabaki kujimwambafai...

AMENISHANGAZA SANA.

PROFESA MZIMA ANASHINDWA KUJIBU FEDHA IMETUMIKA KWENYE NINI ANAJIBU UPUMBAVU MTUPU!
Waziri wa Afya na wajanja janja wanufaika wa mgao wa pesa za corona wapo busy tokea juzi kutengeneza matumizi hewa feki ya kuwahadaa watu wakiamini watu ni wajinga kama wao wakiona hayo matumizi feki wataamini walicholishwa kwa njia haramu za kishetani
 
RAIS MSTAAFU INGILIA JAHAZI WE BELIEVE IN YOU JMK WANA WANATAKA KUZAMISHA JAHAZI KWELI IVO SISI NI WAKUTUNISHIANA MISULI NA HAWA KWELI KWELI
Tayari wametengeneza matumizi hewa ya kuwahadaa wazungu ili waone pesa zao zilitumika vizuri ingawa pesa zote waligawana kifisadi
 
Mimi nina mashaka kuwa Kabudi ametumwa kusema hayo na John! Ukisikiliza kwa makini unaona matamko kama haya yaliyojaa jaziba mara nyingi hutolewa na John kabisa! Lakin kama Wazungu wata ghadhabika kwa kauri za Kabudi,usishangae John akimtumbua ili ionekane kauri za Kabudi siyo msimamo wa serikali ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom