Dr. uko sahihi. Kabudii Ni Waziri wa ushrikiano wa kimataifa. Anaongea ndani ya bunge kwa Kiswahili. Akili zake zimamtuma kuwa kesho akienda huko Ulaya na Amerika hawatamwekea mkanda wa ujinga alioongea.
Anazungumza habari za Spika mwanamke wa Ujerumani ya miaka ya 47, wakati Mkuu wa Ujerumani ya sasa ni mwanamke. Anadai aliwazidi darasani kwa kukariri wakati wenzake wakifanya mavumbuzi ya anga za juu.
Maajabu zaidi Ni kuitetea serikali inayoteka na kupoteza watu, halafu akatumia mifano ya akina Hitler huku akijua dunia nzima hadi leo inayalaani matendo maovu ya akina Hitler.
Kabudi amwambie boss wake wazi kuwa Ni lazima serikali yake iheshimu uhai wa watanzania. Afanye miradi Hadi mawinguni lakini asitumie uzalendo feki kuwaumiza raia na kuvuruga Uhuru wa watu na demokrasia.
Kabudi asisahau kuwa tunawajibika kwa ulimwengu kama ambavyo ulimwengu unavyowajibika kwetu Anaposema: "they have no moral authority to condemn us" ana maana gani kama si ujinga tu.
Yaani dunia ya Leo uwatese raia wa nchi yako kwa dhana za ujima halafu utarajie dunia isikusakame!!!! Ujinga wa kiwango Cha PhD!!!