Niliona jina la Prof. J angeperform jana kwenye Kongamano/Tamasha la Mwalimu pale UD, ila jana sikuuliza kama aliperform au la. Kwa source ni Global, as usual huwa wana sensenalize ili wauze magazeti, kwa Prof. ninayemjua mimi, hawezi kutaka kunyang'anya silaha polis,
Ila polisi nao wana yao, niliwahi kukamatwa usiku wa kawaida tuu toka kwenye starehe zangu, nikaulizwa kitambulisho, nikasema sina, nikaulizwa ninafanya wapi kazi, nikasema sifanyi kazi popote, wakaniambia niko chini ya ulinzi, nikawauliza kwa kosa gani?, wakasema kwa nini huna kitambulisho, kwa nini huna kazi, nikawauliza hivi kukosa kitambulisho ni kosa?, au kokosa kazi ni kosa?, jamaa wakakasirika, wakasemezana, hiri rijamaa rinatuuriza maswali sisi polisi, risweke ndani lirajiereza mbele ya safari. Nikaamriwa kukaa chini, mikono kichwani, ilinibidi nitii tuu.
Jamaa wakaita defender, kwa redio, wakati wakiripoti, wakasema kuna rijambazi wamerikamata rikiwa kwenye harakati za kwenda kutenda uhalirifu. Nilipelekwa kituoni O/Bay kama majira ya Saa Nne usiku. Thanks God, ile kufikishwa kituoni, Mkuu wa Kituo Afande Kalinga, akauliza huyu jamaa amefanya nini, jamaa wakadai, huyu jamaa tumemhoji akatutukana. Afande Kalinga akaniuliza mbele yao, wewe umewatukana vijana wangu?, mimi nikamjibu Sitamtukana mtu Afande, nikamwambia labda wasema nimewatukana nini, kabla hawajajibu, afande akawaambia wanipeleke chumba cha pili kuchukua maelezo yangu, huku nyuma wakasemezana, Afande Kalinga akaja akamwambia askari anayechukua maelezo, aache, akaniambia ondoka yamekwisha. Mimi nikamwambia afande kumbe huu ndio utendaji wa vijana wake, hivi ni wanachi wangapi wa kawaida wanatendewa isivyo na polisi?.
Hii ndio nchi yetu na hawa ndio polisi wetu.