Profesa Baregu: CCM hamna haki miliki ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Baregu: CCM hamna haki miliki ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 13, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Date::10/13/2008
  Profesa Baregu: CCM hamna haki miliki ya nchi
  Na Claud Mshana
  Mwananchi

  MHADHIRI katika Idara ya Siasa na Uongozi wa Umma kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwisega Baregu amekitaka Chama cha Mapinduzi, (CCM) kitambue kuwa hakina haki miliki ya uongozi wa nchi hii, hivyo kinapaswa kusoma alama za nyakati baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa wilayani Tarime.

  Profesa Baregu alisema wananchi walishaamua kufanya mabadiliko katika jimbo hilo tangu mwaka 2005 na kwamba matokeo hayo yanadhihirisha kuwa nia yao ya kutaka mabadiliko ipo palepale.

  ''Pamoja na vitisho na hofu kubwa ya kuwepo kwa askari wa kutiliza ghasia wenye silaha nzito, bado wananchi walijitokeza kwa wingi na kupiga kura kuchagua kiongozi wananyemtaka,'' alisema Baregu.


  Katika uchaguzi huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kiliibuka kidedea baada ya mgombea wake, Charles Mwera kushinda kwa kura nyingi dhidi ya mgombea wa CCM, Christopher Kangoye, aliyekuwa wa pili.

  Prof. Baregu alisema matokeo ya uchaguzi huo na matukio mengine hasa la hivi karibuni mjini Mbeya, ambako Rais Jakaya Kikwete alisimamishwa na wananchi katika msafara wake wakilalamikia kuchoshwa na maisha magumu na kero za mafisadi, ni somo tosha kwa CCM kuanza kujirekebisha.

  ''Zama za michezo michafu na kutumia nguvu katika siasa zimepitwa na wakati, hivi sasa ni wakati wa kushindana kwenye uwanja sawa wa kidemokrasia na si kutumia nguvu ya dola,'' alisisitiza Prof. Baregu.

  Kuhusu suala la ushirikiano wa vyama vya upinzani unaoonekana kulegalega, mhadhiri huyo alisema kinachotakiwa kwa vyama vya upinzani ni kuweka maslahi ya taifa mbele na si maslahi binafsi.

  ''Ni laziama vyama vya upinzani viwe na nia moja na viwe vimekomaa kisiasa kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbeleĀ… na nadhani hapa suala la strategic alliance (ushirikiano wa kimikakati) ndilo linalotakiwa zaidi,'' alifafanua.

  Alisema pia sera iliyopo sasa ni tatizo kwani hata vyama vikiunganisha nguvu bado chama kitakachotambulika ni kile ambacho mgombea huyo amesimama kugombea, hali ambayo alisema inasababisha vyama vingine kuogopa kupotea katika medani ya siasa.

  Wakati huohuo, Mussa Juma kutoka Tarime anaripoti kuwa mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe na naibu katibu mkuu wake, Zitto Kabwe ushindi wa wilayani humo ni zawadi tosha ambayo wakazi wa Tarime wametoa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika vita dhidi ya ufisadi.

  Wakizungumza kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ambao ulifanyika jana katika uwanja wa michezo Sabasaba, viongozi hao walisema ushindi wa Chadema katika jimbo hilo ni ushindi wa Watanzania wote wanaopinga mafisadi.

  ''Ndugu zangu leo mmeandika historia ya nchi hii na tunawahakikisha Mwera na Hecha kuwa watakuwa ni chachu ya maendeleo yenu na tutawapa msaada wote wanaohitaji,'' alisema Mbowe.

  Mwenyekiti huyo alisema uchaguzi wa Tarime ulikuwa ni kipimo kikubwa kwa watanzania wote kama jitihada za wabunge wa upinzani bungeni zimezaa matunda au la na sasa imeonekana somo limeeleka.

  ''Leo mmewapa zawadi kubwa Watanzania ambao wanajiandaa na siku ya kumuenzi Rais Nyerere ambaye ni mzaliwa wa mkoa huu wa Mara hapo Oktoba 14 na tunawapongeza sana,'' alisema Mbowe.
   
Loading...