Prof. Sospeter Muhongo VS Dr. Peter Slaa 2015!!

nafikiri tunahitaji Mtu na sio chama,tukiangalia Zambia walipata mtu anaitwa Sata,kila kitu kimebadilika

Zambia kuna kitu gani kilichobadilika? je, Zambia imetoka kwenye list ya nchi masikini duniani? Je, huduma za kijamii vijijini zimebadilika? Tuambie objectively mabadiliko aliyoleta Sata kwa Zambia.
 
Watu wanaokataa kuuliza maswali ndiyo hutawaliwa kijinga na mafashisti huku wakiwaimbia nyimbo za kuwasifia. wewe kama ungekuwa na uwezo ungejibu maswali yaliyoko kwenye hili bandiko!!

Sioni swali lolote kwenye bandiko hilo zaidi ya wewe kuendelea kupigia mistari majibu ya watanzania walio wengi,amka ndugu,
 
Mimi Prof Muhongo namheshimu, ni mtanzania, ni mtu wa mkoani kwangu, shule aliyosoma msingi ndiyo niliyosoma mimi. Ni mwana taaluma mzuri. Lakini linapokuja suala la uongozi wa nchi yangu. Hasa ikiwa imevurugwa kabisa na ccm kiasi cha kutofikia uwezo wa nchi kiuchumi, huku watanzania hata wale wa mtaani kwao Prof Muhongo wakihangaika na umaskini wa kutisha. Hata angeniambia poti wewe utakuwa waziri mkuu nikipata uongozi kuwa rais kupitia ccm sitamuunga mkono hata kwa robo ya kura yangu.
Kwa kifupi hakuna atakayekuja kutoka ccm atupeleke kwenye nchi tunayotaka watanzania. Hiyo ni kama ndoto ya 2005 wakati watanzania hawa wasiofikiria mbali walipodhani Jakaya Mrisho Kikwete, mwanasiasa mwenye haiba angewapeleka kaanani wanayoitaka. Hapo watanzania tutakuwa na akili za samaki wanaoponyoka kwenye mtego wa samaki na kuendelea kuwa hapohapo mpaka wakanaswa na mtego. Hata tukimchagua kijana asiyetulia kama Zito, Lema, Julius Mtatiro au Sugu lakini wasitoke ccm nchi yetu inaweza kufanya vizuri kuliko kuwa na mtu kutoka ccm.
Kitakachofanya mfano wa hao niliowataja kufanya vizuri kuliko mwanataaluma kama Prof Muhongo kutoka ccm ni kwamba wataweka mfumo wa utawala tunaoutaka. Tutawapa utawala ili watupe mfumo wa utawala tunaoutaka ambao utawabana hata wao kwa udhaifu walionao wafanye vizuri kuliko kichwa kizuri cha Prof Muhongo kwa mfumo mbovu wa utawala uliopo sasa hivi unaolindwa kwa nguvu zote na ccm. Prof Muhongo hawezi kubadilisha mfumo mbovu wa ccm. Hawezi hawezi hawezi hawezi hawezi hawezi hawezi mpaka milele na utabaki hivyo mpaka milele.
Kwa maana hiyo ukija kuangalia ccm na Prof Muhongo ulinganishe na Dr. Slaa na na CDM. Dr Slaa anaweza kufanya vyema mara 10 zaidi. Kwanza kwa kutuwekea mfumo mpya wa utawala na yeye mwenyewe akiwa kiongozi shupavu kama tunavyomjua tutakuwa tumeanza kuondoa nchi yetu kwenye gurudumu la umaskini tunaozunguka nao kila siku, kuweka matumaini ya siku zijazo na kuanza enzi mpya ya maendeleo ya nchi yetu. Usihadaike na katiba mpya ya Jaji Waryoba. Hiyo ni funika kombe mwanaharamu apite ya ccm tu. Haiwezi kuleta mabadiliko makubwa tunayoyataka. Italeta tu cream ya mabadiliko na kuacha misingi ya mfumo mbovu ili ccm iendelee kutawala. Huo ndio ukweli wa mambo.
 
Thesi
asante kwa mawazo yako ya kikamanda,
mods tunaomba muweke polls ya hii thread ili tumtoe wasi wasi mkuu Kigarama
 
Last edited by a moderator:
Mr. Makanyaga
kwanza kabisa huwa sina ushabiki, kwetu umeme unakatika hovyo hovyo tu, wala sija ona tofauti yoyote hivyo nikianza kumsifia itakuwa unafiki. alafu tatizo la huyu bwana...magao wa umeme utakuwa historia...mgao ukaendelea...ohooo tunaweka miundo mbinu mipya mgao ukaendelea....ohooo huyu jamaa wana muhujumu mgao ukaendelea mwisho akaja kuseme ili tanesco ifanikiwe inabidi ifumuliwe upya...jamaa hajafanya chochote cha maana..sijalianakwamishwa na nini
 
Labda Prof ahame chama lasivyo hawezi akampata Dr ata kwa robo kura aiseee
 
Ndiyo kwa asilimia 100 CCM ndiyo tatizo . Kwa sababu ni chama kilichoacha kuongoza kwa maadili yaliyotokana na azimio la Arusha. Na sasa kinaongoza kkwa mfumo wa rushwa na ufisadi tupu. Kimepoteza imani kwa watu wake.
 

WG;
Tatizo la kukatika umeme kumbe unalijua ni miundo mbinu, siyo mgawo. Ulimsikiliza kwenye Kitimoto cha dakika 45 Jumatatu wiki hii lakini?
 
Porojo tupu, narudia tena hii thread ni ya kijinga kabisa.

Tatizo sio profesa wala dk wala suluhisho la matatizo ya watanzania sio chadema suluhisho ni watu gan ama viongozi ambao tutawapata ambao tunawaamini kwa dhati na tunawajua kua wanajua matatizo ya watanzania na wako tayari kutusaidia kuondoa matatizo yanayotukabili na sisi tuwe tayari kuwapokea na kushirikiana nao.Tunahitaji viongozi watendaji zaidi wala sio siasa wala malumbano kwenye mambo ya kiutendaji.Tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Mtawaleta wengi ili mpime kama wanaweza kupambana na Dr.Slaa lakini ukweli ni kwamba he is the best to lead the nation.
 
Uhovyo wangu ni kwa kulitaja jina la Muhongo? Muhongo majibu yake kuhusu Gesi uliyasikia?
Mkuu, majibu ya Muhongo niliyasikia na niliyaona ni mepesi tu.

1. Wananchi wa Mtwara ilibidi washirikishwe kupitia wawakilishi wao (Wabunge na Madiwani) katika hatua ya kwanza kabisa ya kutayarisha mradi. Katika kushirikishwa huko, ilikuwa ni muhimu wajue sababu za kujengwa kwa bomba, na hasara kwao ni nini, na manufaa ya bomba kwao na kwa taifa pia ni nini. Hilo halikufanyika na ni blunder kubwa sana.

2. Wananchi wa Mtwara wana makovu mengi ya kuwekwa pembeni katika fursa mbalimbali za kiuchumi:
a. Reli iling'olewa
b. Barabara bado haijakamilika hadi leo licha ya kusemwa muda mrefu. Miradi iliyokuja nyuma kama ya barabara ya Chato kwenda Mwanza, Nzega Shelui, Shelui Igunga, Nzega Isaka n.k. imekamilika kwa nini wao?
c. Ahadi za wazi za Kikwete juu ya maendeleo ya viwanda ya Mtwara.
d. Dharau ya kudhani kuwa watu wa Mtwara hawawezi kufikiri. Hata katika maswala yanayoathiri afya na shibe yao wakisema eti wanatumiwa na wapinzani.

3. Makubaliano ya Mradi yalitiwa saini Dar, na sherehe ya kukabidhi mradi ilifanyika Dar. Kwa nini?

4. Majibu ya sasa ya serikali ni kuonea aibu mkataba na wawekezaji, ambao tayari umesainiwa.

Muhongo alipoongea hakugusia haya. CCM watakuja kukumbuka mradi huu wa gesi ya Mtwara kama kosa kubwa sana kwao kisiasa. Kigarama siku moja tutarudi hapa na ntakwambia: Didn't I tell you so?
 
Hata CCM Mtwara wanatofautiana na msimamo wa serikali Narudia tena. Serikali ya CCM makao makuu imefanya kosa la kisiasa ambalo watalijutia sana baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…