Prof. Shayo (RIP): Na aina saba za watu

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
Tujikumbushe Prof. Shayo mwanasiasa na mwenyekiti wa demokrasia makini,aliwahi kusema kuna aina saba za watu katika moja za makalla zake katika gazeti la mwananchi enzi za uhai wake....
Aina za watu kutoka kwa mtu mwenye umuhimu sana kwenda kwa mwenye umuhimu mdogo kabisa kwa jamii, je wewe uko wapi???
1. Highest level ya mtu: ni yule anayefikiri pamoja na familia yake pia anajishughulisha kwa manufaa ya binadamu wote, mazingira yake bila kujali mwanadamu huyu anaishi wapi, dini yake au rangi yake. mfano ni watu wahaojihusisha na global economy, global warming etc
2. Second level ya mtu: Ni yule anayefikiri pamoja na familia yake pia anajishughulisha kwa manufaa ya taifa lake na watu wake wote bila kujali dini na rangi zao. mfano ni watu waliojihusisha kupigania uhuru, kina mandela, nyerere, kawawa, etc
3. Third level ya mtu: Ni yule anayefikiri pamoja na familia yake pia anajishughulisha kwa manufaa ya chama chake cha siasa, dini yake, tu. mfano wao ni watu ambao ni pro-religion, pro-ccm etc husaidia pale tu unapokuwa member kikundi chao.
4. Fourth level ya mtu: Ni yule anayefikiri pamoja na familia yake anajishughulisha kwa manufaa ya kabila lake tu, watu ambao si kabila lake hana habari nao. mfano wao ni watu ambao wakipata nafasi hutoa upendeleo kwa kabila lao tu...inasemekana tanzania yako makabila fulani yana haka katabia...
5. Fifth level ya mtu: Ni yule anayefikiria familia yake na ndugu zake tu, hana muda na watu ambao si familia yake wala ndugu (relatives zake). mfano ni watu ambao hupendelea sana ndugu zao pindi wapatapo nafasi.
6. Least but one level ya mtu: Ni yule anayefikiria familia yake tu yaani mke na watoto wake. Mfano wao ni watu wasio hitaji sana marafiki, wala undugu kila jambo hufanya kwa faida ya watoto na mke/mume wake tu finito!
7. Lowest ya mtu: Ni yule anayejifikiria yeye mwenyewe tu!...mfano watu hawa ni wale ambao hawataki familia au hawana familia kabisaa!. watu hawana wanawake/wanaume. ni watu wapweke sana. hujifikiria kujishughulisha kwa faida yao wao wenyewe no more! (No marriage, no family)
 
Kumtaja mtu na kumwongelea tabia yake bila kujua umri wake na mazingira ambayo amekulia kwa namna moja au nyingine ni kutomtendea haki yake. Sioni hapo juu hizo aina za watu zimeongelea watu katika umri gani. Mtoto , vijana katika makumi yao (teens), vijana, watu wa makamo, wazee na vikongwe wote ni watu na tabia zao katika maisha yao zitategemea sana umri walionao. Does that hypothesis of his equate in the age factor?!
 
Kumtaja mtu na kumwongelea tabia yake bila kujua umri wake na mazingira ambayo amekulia kwa namna moja au nyingine ni kutomtendea haki yake. Sioni hapo juu hizo aina za watu zimeongelea watu katika umri gani. Mtoto, vijana katika makumi, watu wa makamo, wazee na vikongwe wote ni watu na tabia zao katika maisha yao zitategemea sana umri walionao. Does that hypothesis of his equate in the age factor?!
Hypothesis in equate character za mtu... kama anajishughulisha na xyz nafikiri prof. ame-hold constant issue ya age.
 
Back
Top Bottom