Prof. Patrick makungu: Katibu Mkuu W. Sayansi na Mawasiliano

Mantissa

JF-Expert Member
Jul 24, 2010
876
166
Ndugu wana JF,

Nimejaribu kumfuatilia sana huyu mzee, ambaye ni katibu mkuu wizara ya Mawasiliano, sayansi na Technolojia, ni moja ya watendaji bora katika Tanzania yetu. Huyu mzee ana maadili ya kazi sijapata kuona. Damu yake naona imejaa element za Nyerere, hana makuu kabisa huyu mzee, hana hata chembe ya ufisadi, kama angekuwa mtu wa kupenda siasa, basi huyu Prof, angefaa kutuongoza. wanaofanya wizara hii nadhani mwaweza kukubaliana na mimi jinsi huyu mzee alivyo mtulivu katika kazi yake na hasa maadili katika kazi ya umma. Hata kama akiwa na safari, akibakiza chenji ya nauli lazima irudi ofsini, kitu ambacho viongozi wengi wa TZ hawana huo uzalendo. Utakuta anaenda kutafuta ticket za kuforge ili mradi tu ionekane hiyo pesa ilitumika kihalali. Tukiiga maadili ya kiongozi kama huyu, basi taifa lazima litabadilika.

Tuige mfano wa kiongozi kama huyu. Angekuwa anapenda siasa, ningemshawishi aingie kwenye kinyang'anyiro, but yeye na siasa, mbali mbali, kwake kazi tu.

Nawasilisha
 
Kwa sifa hizo japo simfaham ila nampongeza namuombea aendelee ivo ivo na msimamo.
 
Good thinking approch. Inauzi kilasiku watu kujifunga na majina fulani fulani tu. Ninaamini Tanzania tuna watu wanaoweza kulirudisha taifa la Tanzania kwenye mstari wa maendelea, nidhamu, uadilifu na uzalendo. Tatizo kubwa ni kuwa tumeacha baadhi ya makundi ya watu yasiyo na fikra huru kuteka mijadala yote kwa kuongelea watu wale wale wenye mawazo yale yale na nia zile zile ambazo zimeshindwa kuleta neema kwa watanzania. Watu wanatumwa tu nenda kaandike hivi leo, unaeda na unatetea upuuzi usioujua madhara yake hadi yatakapokufika.
 
Huyo Prof. ni mchapakazi we acha tu alafu ni kichwa sana, hata alipokuwa mwalimu pale sua uwezo wake wa kufundisha ulikuwa upo juu sana.
 
Huyo Prof. ni mchapakazi we acha tu alafu ni kichwa sana, hata alipokuwa mwalimu pale sua uwezo wake wa kufundisha ulikuwa upo juu sana.
Akiwa CAMARTEC Arusha alifanya makubwa ikiwemo kutengeneza trekta yenye mfumo rahisi. Akiwa SUA pia alishiriki kutengeneza trekta iliyoitwa GRADUATE FARMER ambayo bahati mbaya sifa hiyo ilimuendea asiyehusika.
 
Back
Top Bottom