Prof. Ndalichako, kiatu kishampwaya!

Ikumbukwe moja ya wizara ngumu nchi hiii ni wizara ya elimu
Kama huamini taja waziri mmja ambaye hajawahi kuteleza katika kipindi chake tangu enzi zile
 
macho yangu na hicho kiatu je kitaendelea kupwaya au...?


Obviously Mkuu, kiatu kitaendelea kupwaya coz inasemekana Mtukufu hajaribiwi, hashauriki, na wateule wake wanamuogopa!

-Kaveli-
 
Ikumbukwe moja ya wizara ngumu nchi hiii ni wizara ya elimu
Kama huamini taja waziri mmja ambaye hajawahi kuteleza katika kipindi chake tangu enzi zile
yule padri aliekuwa waziri wa elimu enzi zile hakuteleza?
 
Ikumbukwe moja ya wizara ngumu nchi hiii ni wizara ya elimu
Kama huamini taja waziri mmja ambaye hajawahi kuteleza katika kipindi chake tangu enzi zile


Nchi hii, moja ya mambo ya hovyo yanayotukwamisha sana, ni poor prioritization.

Mifano michache:

1. Kutenga bajeti ya kujenga Airport huko porini, wakati bado hakuna madawa ya kutosha kwenye hospitali wala vifaa tiba.

2. Kutenga bajeti ya kujenga ocean-crossing bridge from Coco beach to Aga Khan, wakati kuna wilaya ambazo bado hazina lami, ama kuna vijiji ambavyo bado havina umeme!

-Kaveli-
 
Tena ni hakika kuwa wote wawili walisoma bure wakati wa Mwl
 
Hii kauli sitaisahau kabisaa, kweli siasa waachie wanasiasa..!

Ni bora niwe unpopular president ili nitimize vitu nilivyoahidi..! by JPM
 
Huyu mama pale yupo kama remote control
Inawezekana kuna ukweli kwa sababu kuna vitu katika hotuba za mkulu huwa anaviongea kiasi ya kwamba unashangaa kwa level yake amejuaje (kawaida tungeona afsa mtendaji,mwenyekiti mtaa/kijiji,meneja,muhandisi avitolee ufafanuzi) and then unaona kabisa kwamba alitoa maelekezo kukataza na hapohapo anatoa uamuzi ambao una lengo la kufurahisha mkutano(anaruhusu).Infact professionalim na ujuzi sio deal bali agizo na mtazamo wa viongozi ndio unao-matter awamu hii
 
Binadamu kwa hulka yetu ni ngumu sana kubaini uzuri wa kitu/mtu mpaka kitu/mtu huyo awe hayupo tena kwenye jambo husika,mfano mzuri ni mke au mume anayemuona mwenzi wake ndani ya nyumba si lolote si chochote lakini muda mfupi baada ya kutenganishwa na kifo au talaka ndipo uzuri wa mwenzake huanza kudhihirika kwenye ubongo wake uliokosa hekma...kama utakumbuka vizuri hata JK alipokuwa kitini wapo ambao hawakubaini uzuri wake lakini kwa sasa wanamuona alikuwa mzuri,likewise mnaobeza utendaji wa JPM siku moja mtakuja kumkubali tena kwa utendaji uliotukuka,JUST A MATTER OF TIME.
 
Wadanganyika tupunguze kulalamika na kulialia, tatizo letu kila mtu anajifanya anajua zaidi, tumekuwa wakwanza kujikosoa na tumekuwa wakwanza kuwasifia wenzetu eti wanaweza. Tumebaki kuwa wakwanza kutojikubali hadharani na piya Tumebaki kuwa wakwanza kujikubali MIOYONI.
 
Huyu mama nilitegemea atatusaidia kwenye hii sekta ya elimu lakin nachokiona ndo anaua zaid

Hivi ni vigezo zipi zinatumika ili mtu upewe uprofesa???

Kama profesa yupo hivi je wengine na mm itakuwaje???
 
Huyu mama nilitegemea atatusaidia kwenye hii sekta ya elimu lakin nachokiona ndo anaua zaid

Hivi ni vigezo zipi zinatumika ili mtu upewe uprofesa???

Kama profesa yupo hivi je wengine na mm itakuwaje???
Hujui unachokisema. Watumishi hawa kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira ya woga wa katumbuliwa wakati wo wote na hawawezi kufanya maamuzi yao binafsi. Kama mimi ningeweza hata kujiuzulu ili kutoendelea kuburuzwa. Lakini again kuna shangingi la Wizara, mshahara mnono na marupurupu mengine kibao.

Kuwa full profesa inabidi uchapishe machapisho yasiyopungua 25 katika reputable peer reviewed journals za ndani na nje. Pengine academic books mbili hivi pia zinatakiwa. Kisha baraza la chuo unachofundisha (only the professors) linakaa na kukujadili kisha linapiga kura baada ya kujiridhisha kuwa machapisho yako yana hadhi ya kimataifa. Ni process ndefu ndiyo maana maprofesa ni wachache na wengine huwa wanakaribia kustaafu ndiyo wanaupata.

Maprofesa wetu, in principle, wanaweza kwenda chuo cho chote duniani kufundisha na kufanya utafiti. Please usichanganye uprofesa wao na mazingira ya kisiasa wanamofanyia kazi. Hata kama ungekuwa wewe ungefanyeje?
 
Nilisema ivi muliomubeza Kikwete na Kawambwa , siku moja mutarudi hapa kuwaomba radhi. Full stop
 
Hapana Mkuu
Huyu kaisha shindwa
Kama hotuba yake ya leo madudu kabisa
Rais anajiaifu kunyima watoto wetu mikopo sababu tu wamesema private schools?
Why hasemi tu ukweli kama HAZINA ni nyeupe?
 

Ok nimekupata kwa hiyo tatizo ni uwoga wa kutumbuliwa pale ambapo itaonekana umeenda kinyume na Mshuwa siyo!

Anyway all in all,hali ni mbaya kwenye hii sekta ya elimu but tukiendelea hivi hivi cjui itakuwaje huko mbeleni

Kama ulivyosema kuwa ni bora mtu ukajiuzulu kuliko kuburuzwa tena profesa mzima,Naamini kuwa profesa una uwezo mkubwa sana wa kuchanganua mambo yapi ni mazuri na kupewa kipaombele,una uwezo mkubwa sana wa kujisimamia na kujiamini

Sioni haja Profesa Ndalichako kuburuzwa kwenye hii sekta muhimu sana
 
Aliyemteua anaamini kama waaminivyo Waafrika wengi kuwa anayeitwa "Professor" au "Doctor" ndiye mwenye akili na uwezo wa hali ya juu wa kufanya mambo.
Nadhani hali halisi inajieleza.
Yuko professor mwingine waziri wa utalii bure kabisa.
kama 'maprofesa' na 'madaktari' wenyewe ndo hawa dizaini ya kina jeipiem,ndalichako na lipumba ooopppssss kazi tunayo....
 
Ukiuliza unaambiwa unatumika kisiasa. Duuuh!!!!! Ata kama umebanwa kuwa mpole tu
 
Mkuu kila profesa wanne mmoja ni kichaa,hata kila mawaziri wanne mmoja ni kichaa,hii wizara bora angepewa profesa Gallabawa,ameonesha kwa vitendo angalia shule yake ya St Thomas More iko njema.huyu mama alinifundisha chuo kozi flani hivi,ni mkurupukaji tuu na hajiamini.
 


Kumbe unamjua vyema eeh.

Watu wengi tulikuwa na imani naye aiweke kwenye mstari Elimu ya Bongo. Lakini dooh sarakasi tupu!

-Kaveli-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…