Prof. Ndalichako awatupia lawama Bodi ya Mikopo kufanya kazi kwa mazoea, arejesha posho ya 8,500

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof. Ndalichako amewatupia lawama bodi ya mkopo elimu ya juu kuwa wanafanya kazi kwa mazoea. Amesema pamoja na kutumia jitiada za kusafisha watumishi bodi hiyo amesema wapo watumishi bado wanafanya kazi kwa mazoea.

Prof. Ndalichako amesema ameyasikia malalamiko kutoka kwa wananchi na anayafanyia kazi na amesema wanafunzi wapewe mikopo semista hii kwa mwaka wa kwanza na wote bila kufuata mean tested.

Amesema lengo la serikali ni kuwapa wote wahitaji. Ameiagiza bodi ya mikopo kuwapa kama mfumo wa zamani na amesema bodi ya mkopo imekosea kuwapa wanafunzi shilingi elfu tano kwa miezi, kama pesa za kujikimu amesema bora kutompa.

Chanzo: TBC
Ninamuunga mkono Prof Ndalichako, HESLB wamefanya kazi kwa mazoea, according to my experience kwa fani ya IT(old is gold or rather experience is the best teacher) kilichotokea pale HESLB ni IT software problem, they should have done a dry run(sample of few students) so as to ensure accuracy and correctness in computing.
 
hatimae ndalichako kasisitiza bodi irudishe 8500 per day kupitia tbc asema hayo....tunakushukuru kwa kutusikiliza pia utusamehe kwa matusi yooote
 

Attachments

  • IMG-20161020-WA0024.jpg
    IMG-20161020-WA0024.jpg
    76.2 KB · Views: 40
Ikiwa hii taarifa ni yakweli, basi naliona tatizo hapa la kiuongozi kwa mawaziri wetu hawa wa awamu hii. Na tatizo hili ni;

1. Ima kila waziri analinda nafasi yake (asitumbuliwe) na hivyo kutoa matamko yenye kupingana au

2. Hakuna mawasiliano kati baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wao. Hii ni kwasababu chache zifuatazo;

Imekuwa ni kawaida kusikia matamko kinzani kati ya waziri na naibu wake ndani ya wizara moja, ama taarifa kinzani kati ya Waziri Mkuu na waziri katika mifano ifuatayo:

A) Kulikuwa na taarifa kinzani katika kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa watumishi kati ya Waziri Mkuu na Mh. Kairuki. Mmoja alisema zoezi limekwisha na huku mwingine akasema zoezi bado halijaisha.

B) Tulipokea taarifa kinzani kati ya Waziri wa Afya na Naibu waziri wake juu ya upungufu wa madawa nchini katika hospitali za umma huku MSD wakipigilia msumari ukinzani huu.

C) Ni taarifa kinzani kati ya Waziri wa Elimu na naibu wake juu ya suala zima la mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu. Huku Bodi ya Mikopo ikipigilia msumari katika taarifa hizi.

Bodi wanasema tusiliganishe mwaka huu na mwaka jana kwenye idadi ya wanafunzi watakaopata mikopo kwakuwa 'priorities' za Waheshimiwa hazifanani. Huku Aibu waziri akidai eti wanafunzi hutumia Boom kununulia TV na 'kupiga ulabu' na hivyo hakuna haja kuwafadhili.

Huku Waziri mwenye dhamana anasema Bodi inafanya kazi kwa mazoea, anaishagaa!

Sasa hapa mwananchi mie wa kawaida ninajiuliza, hivi hawa waheshimiwa hawawasiliani?? au danganya toto kwa sisi wenye kuwasikiliza??

Basi ndio maana kila jambo hata kama ni dogo wananchi wanataka Rais aingilie kati kuondoa sintofahamu . Wakati mambo kama haya yanapaswa kushughulikiwa kikamilifu na ninyi mawaziri aliowateua.

Kazi hizi mkimuachia yeye pekee, mzee mtamzeesha haraka na hali tunahitaji ainyooshe 'inji' hii kona zote zilizopinda.
 
Ndalichako ni mama jasiri. Anaweza kusimamia. Tumuunge mkono
kwani alkua hajawasiliana na naibu wake? mbona yeye kasema watanywea pombe na kununua TV.au hayo maneno alijitungia mwenyewe!
Tuanze na huyo naibu wazir kutumbuliwa maana atakua anaongea upotoshaji wakat mkubwa wake hajui kitu.!!
 
hivi na yule aliesema kua wameangalia vigezo ktk kutoa mikopo na kua sio lazima mikopo itolewe km zamani,kwani kwa sasa kipaumbele ni viwanda. et hii ni serikali nyingine,hiv kwani nae alikurupuka?!!.
 
kwani yule naibu wazir wa elimu, ni wa rwanda au nje ya bara hili la giza?
 
Waislamu walivyoandamana kumkataa yule mama alirudishwa kwa sympathy kwa kudhani eti kaonewa.
Alifanya negligence ya matokeo ya mtoto mmoja ikazuka outcry nchi nzima, sasa anamess up na elimu ya nchi nzima maelfu ya watoto wetu lakini bado anadhani kiti kinamtosha?

Sasa ona anaipinduapindua elimu ya vijana wetu kama chapati.
yule mama anapwaya, Ajiuzulu tu au ang'olewe!
Ukiingiza dini ndo unapo oneshe wewe ki kilaza kiasi gani
 
Board wamekata mishahara yetu hata kwa ambao tumeshamaliza kurejesha mikopo mwezi wa 9 wamepeleka wapi hizo pesaaa walizotukana???
 
Lawama wanatupiwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu tu, je yule Naibu Waziri wa Elimu Eng.(Injinia) Stella Manyanya aliyesema fedha zinatumika kununulia TV na kunywa pombe je kauli yake haikuhusika kwa bodi kupunguza mikopo?
 
4m4 walimlilia huyu mama kuwachanganyia habari Ku change gia angani
 
Back
Top Bottom