Prof Ndalichako asipokuwa makini kuna vyuo vimejiandaa kupiga dili kwa wanaotuma maombi ya vyuo

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,858
5,101
Hivi karibuni serikali imetangaza rasmi kuwa kuanzia mwaka huu maombi yote yanayohusu kutaka kudahiliwa kujiunga na vyuo kwa kozi yoyote yatatumwa Moja kwa Moja kwenye vyuo husika

Katika hili kuna vyuo vimejiandaa kufaidi kupitia ada ya waombaji Wa vyuo. kama Waziri Wa elimu hatoliona hili na kutoa mwongozo mapema juu ya kiwango maalum cha ada ya maombi watu wategemee kulizwa kwani kuna vyuo vimekata tamaa hivyo wanategemea kupitia ada hii.

Nawasilisha
 
Ila jaman vyuo private kwa ada kubwa na michango mshtukizo vimezidi, ingawa ckupata mkopo ila kwa hili namsifu magu kwa maana hawa tcu walikuwa wametupanda kichwan mtu umekesha kutafuta CCC zako then wanakufanya fala huu ni ujinga bora mtu afanye application direct chuo, ila kuna baadhi ya vyuo vitakosa watu watajikuta wanasajili hata watu wasio na sifa... Yangu macho
 
Nafikiri anamaanisha Application fees ( Ada ya maombi ya kujiunga na chuo) hiyo ipo ni Tsh 20000/= na isizidi Tsh 30000/= unapewa na Risiti maalumu
 
Ila jaman vyuo private kwa ada kubwa na michango mshtukizo vimezidi, ingawa ckupata mkopo ila kwa hili namsifu magu kwa maana hawa tcu walikuwa wametupanda kichwan mtu umekesha kutafuta CCC zako then wanakufanya fala huu ni ujinga bora mtu afanye application direct chuo, ila kuna baadhi ya vyuo vitakosa watu watajikuta wanasajili hata watu wasio na sifa... Yangu macho

lakini kumbuka kuwa unaweza kuomba vyuo vyote vya serikali ukatemwa na hapo utalazimika kutumia hela nyingine tena kuomba hivyohivyo vyuo vya private. hivyo kikubwa ni serikali kuweka kiwango kidogo cha ada ya maombi vinginevyo watu watashindwa kupata vyuo mwaka huu
 
Hivi karibuni serikali imetangaza rasmi kuwa kuanzia mwaka huu maombi yote yanayohusu kutaka kudahiliwa kujiunga na vyuo kwa kozi yoyote yatatumwa Moja kwa Moja kwenye vyuo husika
katika hili kuna vyuo vimejiandaa kufaidi kupitia ada ya waombaji Wa vyuo. kama Waziri Wa elimu hatoliona hili na kutoa mwongozo mapema juu ya kiwango maalum cha ada ya maombi watu wategemee kulizwa kwani kuna vyuo vimekata tamaa hivyo wanategemea kupitia ada hii.

nawasilisha
Unataka Fomu zitolewe bure?
 
lakini kumbuka kuwa unaweza kuomba vyuo vyote vya serikali ukatemwa na hapo utalazimika kutumia hela nyingine tena kuomba hivyohivyo vyuo vya private. hivyo kikubwa ni serikali kuweka kiwango kidogo cha ada ya maombi vinginevyo watu watashindwa kupata vyuo mwaka huu
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom