TANZIA Prof. Mwesiga Baregu afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,579
6,558
IMG_20210613_095423_972.jpg

Ni habari mbaya ambayo imetokea muda si mrefu.

Aliyekuwa Mhadhiri wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, Prof. Mwesiga Baregu amefariki dunia mapema leo.

Prof. Baregu alikuwa pia Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA.

Pia Soma: Prof. Baregu alifukuzwa UDSM kwa sababu za kisiasa, huku Bashiru akiachwa kwakuwa ni CCM

1623650580786.png

Dar es Salaam. Mwanachama wa Chadema na mwanazuoni, Profesa Mwesiga Baregu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema, “amefariki saa tano usiku wa kuamkia leo akiwa ICU (chumba cha uangalizi maalum) na alikuwa hapo kwa takribani siku 15.”

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Mkurugenzi wa Itikadi na Uhusiano wa kimataifa wa Chadema, John Mrema amesema chama kitatoa taarifa rasmi taarifa baada ya kikao na wanafamilia.

"Tunaelekea hospitali ya Muhimbili kukutana na wanafamilia halafu tutatoa taarifa rasmi," amesema Mrema.

Katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema, "pumzika kwa amani Profesa Baregu. Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao.’”

Mwingine aliyeandika ujumbe Twitter ni kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akimtakia mapumziko mema Profesa Baregu.

Profesa Baregu aliyekuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa na utawala wa umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baadaye alisitishiwa mkataba wake kwa kile kilichoelezwa kuchanganya utumishi na siasa.

Baadaye alihamia Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema hadi mwaka 2019.
20210613_200804.jpg
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
4,097
11,031
1 Wakorintho :15:26
Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.

Mpk wakati huo ufike hatuna budi kuwa wanyonge kwa huyu adui wetu kifo. Kwa wale wanaolala wakiwa na tumaini kwa mwokozi wao Bwana Yesu kifo ni usingizi tu maana siku akirudi atawaamsha. Bwana atupe moyo wa hekima tuzihesabu siku zetu hizi chache za ubatili. Pole kwa familia ya mpigania demokrasia huyu nguli
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,451
Uzima wetu aujuae Mungu pekee, Duniani tupo kwa muda kitambo tu, na tena haijulikani ni lini Mungu atautaka uhai wetu, Tunalojukumumoja tu, Ni kusema Asante Mungu kwa maisha ya mja wako,

Pumzika kwa amani na kwa hakika umeacha alama

Poleni wafiwa, R.I.P prof Baregu
 
36 Reactions
Reply
Top Bottom