Prof. Mwandosya amchana Mkapa

Prof. Mwandosya amchana Mkapa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
MWANASIASA mashuhuri nchini, Prof. Mark Mwandosya, amemtolea uvivu, Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Mwandosya ambaye alikuwa mmoja wa wagombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye jina lake liliondolewa katika hatua za awali za kinyang'anyiro hicho anasema, "ni muhimu kama viongozi, kuvumiliana na kuheshimiana," ili taifa lisiingie katika machufuko.

Akiandika katika ukurasa wake wa facebook, Prof. Mwandosya amesema, taifa linapita katika kipindi kigumu, hivyo ni vema wanasiasa na wananchi wengine wakajenga utamaduni wa kuvumiliana.


Amesema, "katika kipindi hiki muhimu, kama taifa, inatupasa tuzingatie; kuvumiliana, kuheshimiana, kukubaliana, kukubali kutokubaliana, kushindana kwa hoja, na kutumia lugha yenye staha."


Prof. Mwandosya anasema, "Msaafu Mtakatifu unatukumbusha '…vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao huvuna majivuno makuu."


Andishi la Prof. Mwandosya limekuja siku tatu baada ya Mkapa kufungulia bomba la matusi kwa kuwaita viongozi wakuu wa upinzani nchini na wafuasi wao, kuwa marofa na wapumbavu.


Mkapa alisema wapinzani wanaosema vyao vyao ni vya ukombozi ni wapumbavu na malofa kwa kuwa Tanzania ilishakombolewa na vyama vya Tanganyika National Union (Tanu) na Afro Shirazi Party (ASP).


Bila kutaja jina la Mkapa, Prof. Mwandosya aandika kwa njia ya kuonya, "…angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana…"


Anasema, "Msaafu Mtakatifu unatuonya pia "…kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa…."


Tangu Edward Lowassa, kujiunga na upinzani na baadaye Fredrick Sumaye, kumfuata kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuondoa CCM madarakani, kumekuwa na mihamko ya viongozi wakuu wa chama hicho na serikali kuzuia upinzani kushika dola.


Taarifa zinasema, mihamko hiyo, ndiyo iliyomsukuma Mkapa kutukana baada ya kuona kitumbua chake kinaingia mchanga.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
hiyo ndo busara,sio akili za kijinga tena za kipuuzi za mkapa jangwani,kikwetu tunamfananisha mkapa na IFUVE
 
Mwandosya nimeamini ni Profesa halali Tanzania akifuatiwa na mwenzie waliosoma pamoja pale Ud Prof Mayo mjasiriamali wa Real Estate kule Changanyikeni.
 
Well done prof Mwandosya tunakusubiri pale bahari beach hotel tuunganishe nguvu waporomosha matusi wasiendelee kutawala wastaarabu.
 
Msameheni bure Mkapa! Mkapa anajulikana ni mtu wa mwenye MIHEMKO na JAZIBA

Aliwahi kutupa microphone mbele ya Tim Sebastian wa kipindi cha hard talk cha BBC, wakati huo kikiwa hewani (LIVE) na kugoma kuendelea na mahojiano.

Hiyo ilitokea wakati alipobanwa na Tim kuhusu mauaji ya Wapemba huko Zanzibar.

Kutokana na JAZIBA na MIHEMKO ndio maana hata baada ya kuwa Rais, hakuacha kumpiga/kugombana na mke wake hata alipokuwa IKULU (Ref kuvunjika mkono na kutembelea magongo saga)
 
Mkapa amejidhalilisha sana ameonekana ni kama jitu lisilo na heshima mbele ya jamii.
 
nngu007

kumbe ni nyie, subiri sheria ya mtandao ianze bado siku tano za uropokaji
 
Last edited by a moderator:
Hapa najua kuna wanafiki kibao, sasa hivi WANAMKUBALI Prof. Mwandosya sababu kasema wanachotaka kusikia, siku akisema kitu ambacho hawataki kusikia na kukikubali licha ya kwamba chaweza kuwa na ukweli ndani yake atageukwa na kuwa mchumia tumbo!
 
Back
Top Bottom