PRof. Mutakyahwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PRof. Mutakyahwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee wa Usafi, Apr 10, 2012.

 1. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Leo wanataaluma na wataalamu wa sayansi ya dunia (Earth Scientists-Geologists et al) tumemzika mwanataaluma mahiri Prof.Mutakyahwa. Prof.Muta ni mmoja wa wataalamu waliotoa mageo karibia wote walioko migodini na nje ya nchi ambayo ndo wanaaingizia mifuko ya hifadhi ya jamii mabilioni ya shilingi. Amesaidia kuongeza namba ya wahitimu wa shahada mbalimbali. Cha ajabu serikali nzima imeishia kwa Kanumba, TBC1 wameacha kutangaza mambo mengine isipokuwa maziko ya Kanumba....Je wazalishagi hawaonekani isipokuwa wasanii wa luninga tu, au kwakuwa Prof.Muta sio maarufu kwa wanasiasa.


  Sisi wasome wachache tulioko Tanzania tunasema RIP Prof.Muta kazi yako na mchango kwa Taifa ni kubwa kuliko wasanii wa tasnia ya filamu. Tutakukumbuka daima kwa jinsi ulivyo saidia taifa hili....mara ya mwisho kukuona nilikupakiza kwa gari na tuliongea mengi mmojawapo ulisema ulipewa nafasi ya kufundisha nje ila ukaweka uzalendo mbele ukaamua kurudi nyumabani ili kuanzisha Geology department pale Mlimani.. Watawala hawaoni hilo isipokuwa umaarufu wao kwa kwenda kwa marehemu Kanumba.......daima tutakukumbuka
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Wakongwe wa Geology wanazidi kwish tu
  Dr Mnali, Dr Kapilima, Dr Msindai na Sasa Prof. Muta,

  RIP Prof. Muta
   
 3. T

  TwendeSasa Senior Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mungu ailaze mahala pema roho ya Prof Muta... nawasikitia waliobaki chuo watakosa mafundisho yake na furaha yake ya kufundisha
   
 4. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  So sad, R.I.P Prof, kweli nilifurahia sana course zako, kwa wale wote waliosoma CoET uhandisi wa madini kamwe hawatamsahau.
   
 5. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vipi kikwete alikuwepo?
   
Loading...