Prof. Muhongo na jitihada za kutokomeza umaskini na unyonge

Prof. Muhongo na jitihada za kutokomeza umaskini na unyonge

Upanga Mkali

Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
96
Reaction score
83
PROFESA Sospeter Muhongo, ni mmoja wa wanasayansi bobezi na mahiri katika sayansi ya madini (geologists), anayetambuliwa na kuheshimika na mashirika mbalimbali ya kisayansi na utafiti ulimwenguni.

Miongoni mwa taasisi zinazoaminika kimataifa zinazomtambua na kumtumia Profesa Muhongo katika uwezo wake wa utendaji wa kazi ni pamoja na FGSA la Marekani, FGS la London, Uingereza; HonFCAGS la China, na Chuo cha kuendeleza Sayansi ya dunia (FTWAS).
Taasisi nyingine zinazomtambua na kuheshimu uwezo wa Profesa Muhongo ni Rais wa Taasisi ya Wataalamu wa Jiolojia wa Afrika (FGSAF), Taasisi ya Chuo cha Sayansi Afrika (FAAS), Taasisi ya Sayansi Tanzania (FTAAS).

Ukitazama taasisi ambazo amezifanyia kazi na kujipatia heshima na kuaminika ni za nje ya nchi na hasa za nje ya Afrika. Ni profesa wa vitendo, tofauti kabisa na maprofesa waliozoeleka humu nchini ambao hupenda kusikika wao ni wasomi lakini usomi wao ni wa tafiti na midhara ya kisomi, kusubiri wananchi waibuke na mambo yao mitaani wao waifanyie uchambuzi kama wamepatia au wamekosea basi.

Maprofesa hawa mara nyingi wamekuwa wakisubiri vipindi vya majadiliano kwenye redio na luninga ili kushiriki majadiliano na kuikosoa serikali ama kuwakejeli watanzania wakiwa na lengo la kuonyesha kwamba wao ni wasomi.

Uwemo wake katika orodha ya wanasayansi wa fani yake wanaoaminiwa duniani, umemsaidia kupata tuzo mbalimbali zenye heshima kimataifa.

Mwaka 2004, alitunukiwa tuzo ya Profesa Robert Shakleton ya nchini Uingereza kutokana na mchango wake katika utafiti wa kisayansi barani Afrika.

Uwezo wake huo, umewafanya wataalamu wa Jiolojia duniani wampe hadhi ya umakamu wa rais katika Kamisheni ya Wataalamu wa Jiolojia duniani (CGMW). Ni profesa katika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Tanzania na chuo kikuu cha Sayansi cha Pretoria nchini Afrika Kusini.

Heshima nyingine iliyo katika kumbukumbu yake ni kuwahi kuwa mwenyekiti wa kamati inayotoa Tuzo ya Sayansi na Teknolojia (AIPF-STI) ya Kwame Nkrumah inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU), tuzo iliyotolewa mwaka 2011.

Hii ilitokana na yeye kuwa miongoni mwa wanasayansi wa jiolojia anayeheshimika na kutambuliwa ulimwenguni katika kupanga sera zinazohusu sayansi na Teknolojia sambamba na utafiti. Mwaka 2009, Tanzania kwa kutambua uwezo wake, ilimpendekeza kugombea nafasi ya kuwa mkurugenzi mkuu wa UNESCO.

Prof Muhongo alikuwa rais wa wataalamu wa Jiolojia Afrika mwaka 1995-2001, mwaka 2005-2010 akawa mkurugenzi wa kanda wa ICSU kwa upande wa Afrika ofisi yake ikiwa Pretoria nchini Afrika Kusini.

Mwaka 2004-2008 alikuwa mwenyekiti wa tume ya sayansi ya UNESCO-IUGS-IGCP na pia akafanikiwa kuwa mwenyekiti wa program ya kamati ya sayansi. Mwaka 2007-2010

Miongoni mwa sifa zake za hivi karibuni, Prof. Sospeter Muhongo ameendelea kuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, huku akiwa profesa wa FGSAf, FAAS, FASI, FASSAf, FGIGE, FTWAS, HonFCAGS, HonFGS, CGeol, EurGeol na ni mwanachama wa heshima katika Taasisi ya Jiolojia ya London (Honorary Fellow of the Geological Society of London (HonFGS).

Ni mtafiti wa heshima wa Taasisi ya Jiolojia ya nchini China (HonFCAGS), Mwanachama wa Taasisi ya Sayansi ya Nchi zinazoendelea (Fellow of the Academy of Sciences for the Developing World (FTWAS). Ni mwanachama wa Taasisi ya Jiolojia ya Afrika (Fellow of the Geological Society of Africa (FGSAf)) na mwanachama wa Taasisi ya Sayansi ya Afrika (Fellow of the African Academy of Sciences (FAAS).

Ni mwanachama anayeaminika kwenye vyama na taasisi nane za wanasayansi wenye elimu ya juu katika sayansi duniani akiwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya Robert Shackleton ya ufanisi katika utafiti wa jiolojia barani Afrika.

Ni Makamu wa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa ramani za kijiolojia duniani (Commission of the Geological Map of the World (CGMW). Ni mhariri Mkuu wa Jarida la Sayansi za Dunia barani Afrika (Journal of African Earth Sciences), Mhariri mwenza wa jarida la taasisi ya Precambrian (Precambrian Research) na yumo katika bodi kadhaa za uhariri wa majarida ya sayansi.

Prof. Muhongo ni mhariri mwandamizi wa kitabu kilichochapishwa mwaka (2009) kiitwacho; Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika maendeleo ya Jamii habari za mafanikio kutoka Afrika (Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa.)

Alikuwa Rais wa Chama cha wanajiolojia barani Afrika (Geological Society of Africa (1995 - 2001). Ni mkurugenzi muasisi wa kanda ya Afrika wa Chama cha wanajiolojia Afrika katika wa ICSU katika ofisi ya kanda iliyoko mjini Pretoria, Afrika Kusini (2005 - 2010).

Alikuwa mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya Bodi ya Kimataifa ya Sayansi za kijiolojia, iliyo chini ya UNESCO (UNESCO-IUGS-IGCP (UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of International Geoscience) mwaka 2004 - 2008, na Mwenyekiti (2007 - 2010) wa Kamati Umoja wa Mataifa ya Mwaka wa Sayansi ya Sayari Dunia.

Ni mjumbe wa kikundi cha wataalamu wa kimataifa wa Sayansi ya Dunia (Member of the International Experts Group (Global Science Forum) ya taasisi ya OECD.

Alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO mwaka 1999 mpaka 2005. Alikuwa mkuu wa idara ya Jiologia ya Chuo Kikuu cha Dar e salaam (1997 - 2000), Mwenyekiti wa Kamati ya serikali ya kuchunguza maafa kwenye mgodi wa Tanzanite wa Mererani (2002).

Ni mwandishi wa taarifa za utafiti zaidi ya 200 zinazotumika katika ufundishaji duniani kote kuhusiana na jiolojia na madini. Amewahi kualikwa ili kutoa mada kwenye mikutano zaidi 300 ya kimataifa ya wataalamu duniani.

Amefanya tafiti zaidi ya 100, kutoa machapisho zaidi ya 200 katika majarida ya kisomi kimataifa na kufanya kazi ya ushauri katika sekta ya madini, na mazingira na katika masuala ya sera za mazingira. Amekuwa kwenye kamati, kamisheni na bodi mbalimbali za ushauri kuhusu jiolojia na mazingira akishiriki kupitia kupitia na kuboresha sera nyingi katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.

Mbali ya kuwa mhadhiri Mwandamizi katika idara ya sayansi ya Jiolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia ni mtahini kutoka nje na mwamuzi (Examiner/Referee) kwa vyuo vikuu kadhaa duniani akishiriki kama msahihishaji. Msimamizi wa mitihani na mthaminishaji wa mitihani kwa watahiniwa wa ueledi kama vile watahiniwa wa nafasi za kieledi.

Kwa miongoni miwili iliyopita, Profesa Muhongo amekuwa akitumika na kutayarisha zaidi ya mikutano 100 ya kimataifa ya wanataaluma wa sayansi ya dunia, na sera za sayasi ikiwemo ile iliyohusu sayansi na Afrika, inayoendeshwa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (United Nations Economic Commission for Africa (UNECA), the African Union Commission (AUC) na washirika wake.

Kama ilivyoelezwa kwa ufupi hapo juu, Profesa Muhongo amewahi kushika nafasi kadhaa muhimu za juu katika taaluma za kitaifa, Afrika na za kimatifa akiwa anajishughulisha na sayansi, teknolojia, rasilimali ya dunia, sera za sayansi na diplomasia ya sayansi.

Prof. Muhongo ameshiriki katika kuwafuatilia na kuwasaidia wanasayansi vijana akiwa amejiegemeza zaidi katika matumizi na uendelezaji wa sayansi kwa manufaa ya maendeleo ya kiuchumi katika jamii yote duniani.

Alijifunza jiolojia kwenye vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Goettingen (Ujerumani). Anayo pia shahada kutoka Chuo Kikuu cha Berlin nchini Ujerumani. Ana uwezo mkubwa wa kuzungumza lugha za kiingereza, kijerumani na ana uwezo pia wakiasi fulani kifaransa.

Anafahamika kama muumini thabiti wa matumizi ya sayansi kwa faida ya jamii ya dunia na maendeleo. Anaamini kwamba sera za maendeleo ya dunia zinatakiwa kuwa na mwelekeo wa kisayansi na wa kiasiasa baadaye.

Anaamini kwamba usalama wa chakula, mabadiliko ya hali ya hewa, afya ya binadamu kama mambo ya muhimu kuliko yote yanayotakiwa kushughulikiwa na dunia, dhidi ya yale yanayojitokeza hivi sasa kama kupunguza idadi ya watu (inatarajiwa kufikia bilioni 10 mwaka 2050).

Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni alikuwa waziri wa Nishati na Madini, kwa muda wa miaka miwili na nusu aliyotumikia wizara hiyo, ameonyesha uzalendo na uchapakazi wa hali ya juu.

Kwa kipindi kifupi aliweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye wizara hiyo na kuboresha utendaji kazi wa mashirika na idara zilizo chini ya wizara hiyo. Ameweza kusimamia vema mradi wa umeme vijijini (REA) ambapo mpaka sasa zaidi ya asilimia 40 ya vijiji vya Tanzania vina umeme. Ameiwezesha Tanzania kuwa Taifa linaloongoza barani Afrika kwa wananchi wa vijijini kuwa na umeme.

Waliofanya kazi naye au kufanyakazi chini yake wanakiri Prof. Muhongo ni mwadilifu, mzalendo na mwaminifu anayeguswa na kuhuzunishwa na umasikini uliowatia unyonge waafrika hasa wa nchi yake Tanzania na mara kadhaa amekuwa akisisitiza baada ya miaka kadhaa Tanzania itapiga hatua na kuondokana na umaskini iwapo raslimali zilizopo zitasimamiwa vizuri.

Prof Muhongo, kwa muda wote, amekuwa akisisitiza watanzania wamechoshwa na umasikini kwa kuwa wanazo rasilimali za kufuta umasikini. Anasema haki, amani, utulivu, uadilifu na uaminifu ni nguzo za ustawi wa Taifa letu. Elimu, utaalamu, uchapakazi kwa bidii, ubunifu, mipango na miradi inayotekeleza ni nguzo za uchumi imara wenye kutoa ajira mpya na kufuta umasikini hivyo tusikate tamaa na kwamba tutavuka tukiwa na ushindi wa masikini na wanyonge.

“Ni jukumu la Wasomi na Wataalamu Watanzania kuongoza jitihada za kutokomeza umaskini na unyonge tulionao nchini mwetu. Gesi asilia tuliyonayo na tunayoendelea kugundua (na huenda mafuta) ndiyo injini nambari wani ya kutokomeza umaskini wetu. Umeme wa bei nafuu utapatikana, viwanda vitapanuka na vipya vitajengwa. Kilimo chetu kitabadilika na kufanywa cha kisasa chenye kutumia sayansi na teknolojia. Ajira mpya zitakuwa nyingi” anasema Prof. Sospeter Muhongo.
 
kushiriki uchotwaji wa billion 321 kwenye account ya ESCROW inatosha kabisa kusema Prof. Muhongo ni muongo hana nia ya kutokomeza umasikini TZ.
 
aaaaaaaaarrrrrrggggggggghhhhhhhhh ndefu sana hii, plz atakayeisoma yote aisummarize
 
Back
Top Bottom