Prof. Muhongo: Subirini maamuzi magumu TANESCO

Status
Not open for further replies.

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospiter Muhongo, amewataka wananchi kuvuta subira wakati akishughulikia orodha ya watumishi wanaolihujumu Shirika la Umeme (Tanesco) kwani yeye si mtu wa kukurupuka.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na NIPASHE mjini hapa juzi.

“Vuta subira…unajua mimi nimelelewa katika sayansi, si mtu wa kukurupuka tu, ni lazima tufanye uchunguzi kwanza suala si kuyataja tu,” alisema.
Alisema hataki kumuonea wala kumpendelea mtu, hivyo watafanya uchunguzi wa kina, kuyaanisha matatizo na kisha kuja na njia za utatuzi kabla ya kutoa taarifa kwa umma.

Profesa Muhongo, alisema hayuko tayari kusema mambo nusu nusu katika vyombo vya habari na kutaka wananchi kuvuta subira.

Hivi karibuni, Profesa Muhongo, alikwenda kutembelea Tanesco na kuwataka watumishi kuwataja watu wanaolihujumu shirika hilo kwa kutumia kura za siri.

sosi: Ippmedia.com
 
Ukisikia maamuzi magumu nchini Tanzania ujue mkuu wa kaya amelindwa. na ndio maana wanakuwa wagumu kuamua ili wapate watu wa kuwatoa kafara kwa ajili ya mkuu wa kaya.
 
Mi hofu yangu ni kuzimwa kwa watu hao kutokana na nguvu kubwa waliyonayo Mafisadi, baadae tutaanza kusikia siasa ama anaweza asichukue tena maamuzi magumu ni muda toka ametajiwa wahujumu hao wa tanesco
 
tunasubiri,ila tusije kusubiri kwa karne!maana wote aliotupa ahadi pamoja na yeye tutakuwa hatupo duniani!
 
:llama:Anatia matumaini tunakuombea usibadirike kama wenzio wengine. Kumbuka cheo ni dhamana. Siku ya mwisho utakuja kuulizwa ulikifanyia nini.
 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospiter Muhongo, amewataka wananchi kuvuta subira wakati akishughulikia orodha ya watumishi wanaolihujumu Shirika la Umeme (Tanesco) kwani yeye si mtu wa kukurupuka.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na NIPASHE mjini hapa juzi.

"Vuta subira…unajua mimi nimelelewa katika sayansi, si mtu wa kukurupuka tu, ni lazima tufanye uchunguzi kwanza suala si kuyataja tu," alisema.
Alisema hataki kumuonea wala kumpendelea mtu, hivyo watafanya uchunguzi wa kina, kuyaanisha matatizo na kisha kuja na njia za utatuzi kabla ya kutoa taarifa kwa umma.

Profesa Muhongo, alisema hayuko tayari kusema mambo nusu nusu katika vyombo vya habari na kutaka wananchi kuvuta subira.

Hivi karibuni, Profesa Muhongo, alikwenda kutembelea Tanesco na kuwataka watumishi kuwataja watu wanaolihujumu shirika hilo kwa kutumia kura za siri.

sosi: Ippmedia.com

Aanze na mafundi wote kwani wao ndio vishoka wakubwa
 
limeanzishwa 1930 mpaka leo just 20% ndio wenye umeme!hataki mambo ya tume ni upuuzi!PUBLIC HEARING ITAANZA
 
box la spear ya tanesco toka uk imelipiwa pound 50000 kumbe ni misumari

Kuu ni kweli ? Kama ni hivyo huyo aliyefanya hivyo anastahili china style. risasi tu tena anazinunua kwa hela yake mwenyewe.
 
Wamejiunganishia umeme kinyume cha sheria, hawaripi bils, imebainishwa na Waziri wa nishati na madini leo bungeni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom