Nitatumbua majipu tofauti na wengine- Prof. Muhongo
Friday, February 19 2016, 0 : 0
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema kazi ya kutumbua majibu inayofanywa na viongozi
wenzake serikalini, itakuwa tofauti na ile ambayo ataifanya yeye kwa kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi.
Prof. Muhongo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Wawekezaji wa Nishati ya Umeme nchini.
Alisema kila mtu anastahili yake ya kufanya kazi ambapo hamu ya wananchi ni kuona Wizara yake ikitumbua majibu kama wafanyavyo viongozi wenzake lakini yeye atatumbua majipu hayo kwa staili tofauti.
"Itanichukua miaka 100 kutumbua majibu kama wafanyavyo viongozi wenzangu...mimi utumbuaji wangu ni kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi.
"Mtendaji mzuri si lazima aonekane sana katika vyombo vya habari, Watanzania tunapaswa kuwa makini katika hili, lazima
viongozi wawe waangalifu tunapovitumia vyombo vya habari, jambo la msingi ni kutoa huduma," alisema.
Aliongeza kuwa, atahakikisha mikataba mipya ambayo Wizara itaingia na wawekezaji, haitakuwa na makosa na ile ya zamani, itaanza kupitiwa upya.
Prof. Muhongo alisema mikataba ambayo wameikuta ni mingi ambapo kwa mujibu wa taratibu kisheria, ipo mikataba ambayo wataipitia na kuirekebisha, mingine haitawezekana kutokana na kuheshimu mikataba hiyo.
Akizungumzia tozo za kampuni kutokana na sera mpya ya umeme, alisema Shirika la Umeme nchini (TANESCO) halitazalisha umeme pekee bali litashindana na kampuni nyingine katika uzalishaji.
"Sera mpya inasema, mtu kuzalisha umeme si lazima auziwe na TANESCO, hivi sasa kampuni zinazozalisha umeme zinaruhusiwa kumuuzia mtu yeyote bila kupitia TANESCO," alisema.
Aliongeza kuwa, TANESCO mpya itapata washindani katika uzalishaji umeme na usambazaji ili kuhakikisha Watanzania wanapata umeme kwa bei nafuu na kuwafikia kwa urahisi.
Alisema hadi sasa Watanzania asilimia 40 wanapata umeme ambapo Tanzania ikiwa nchi ya kipato cha kati, huduma hizo lazima isambae kwa asilimia 75 ambapo mpango huo utafanikiwa kutokana na kasi iliyopo katika Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA).
Kuhusu upunguzaji bei ya umeme, Prof. Muhongo alisema Serikali imewapa jukumu la TANESCO, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), waone uwezekano wa kupunguza bei ya umeme.
"Watanzania wavumilie, kazi ya kupiga hesabu inaendelea iweze kuletwa wizarani nasi tutawaeleza maana upunguzaji bei hauwezi kufanyika kwenye jukwaa, lazima kuwepo hesabu," alisema.
Alisema tathmini inaonesha hali ya umeme nchini imeimarika ambapo TANESCO wamejitahidi na wanazidi kuimarisha upatikanaji umeme wa uhakika.