Waziri Muhongo...
Umeonyesha umahiri mkubwa wa kuongea na kuonyesha kwamba unayoyawasilisha una uhakika nayo. Lakini kumbuka wizara unayoiongoza ni sensitive zaidi ya unavyofikiria.
Kumbuka kauli yako uliyotoa miezi kadhaa iliyopita 'kuwatukana' watu wa Mtwara kuwa ni wapumbavu na wabinafsi ni mojawapo ya kauli zililolifikisha taifa hapa lilipo juu ya ishu ya Mtwara.
Umekuwa mwepesi sana wa kukosoa kwa kejeli na majivuno makubwa na kuonyesha kwamba unayoyawaza wewe tu ndiyo sahihi. Pengine ni kweli maana wewe ni profesa... msomi na hakuna msomi kama wewe hapa Tanzania. Lakini kumbuka tu kitu kimoja,... hao unaowadharau na kuwaona wapumbavu kuna siku utahitaji kuungwa nao mkono ili hiyo mipango yako ya kiprofesa itekelezwe
Waziri Muhongo, nimesikitishwa zaidi na namna unavyolishughulikia suala la Mtwara kwa kuita mawazo yeyote mbadala kuwa ni "porojo". Lakini umesahau kuwa hawa unaowaambia wanapiga porojo wana ushawishi mkubwa katika jamii, wanakubalika na wengi katika jamii na wana nafasi kubwa sana katika jamii. Kama profesa nilitarajia kuwa majibu yako kwa maoni ya kambi ya upinzani yawe ya kidiplomasia zaidi. Nilitarajia useme 'maoni ya kambi ya upinzani tumeyasikia, tutajitahidi kuyafanyika kazi yale yenye manufaa kwa wananchi'... kisha ukaendelea na hotuba yako. Si ndivyo mnavyotufundisha hata huko vyuo vikuu profesa? Kwamba unapotakiwa kutetea hoja yako katika jambo lililo tense basi uwe diplomatically neutral?
iHivi profesa unadhani wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine walioshika kalamu na karatasi jana walikuwa wangapi?
Hivi profesa unadhani kwa kutengeneza unnecessary "bifu" na wapinzani ndio utakuwa umeshinda mchezo?
Pinda anaenda Mtwara sasa, kujadiliana na "wapiga porojo", na watamuuliza umekuja kusikiliza porojo zetu?
Mheshimiwa profesa, mimi sina ueledi wowote wa kukushauri, lakini nakuomba kuanzia sasa kabla hujaja kutusomea hotuba zako za takwimu, walau zipitishe kwa "afisa mahusiano ya jamii" wa wizara yako apitishe hapo macho...