Prof. Muhongo, Maswi watajwa kuiua TANESCO

Prof. Muhongo, Maswi watajwa kuiua TANESCO

Aina hiyo ya ubanaji wa matumizi wala hakuna anayesema kwamba ndio suluhisho la TANESCO hivyo ni upuuzi kudai hata kama watafanya yote hayo bado TANESCO itapata hasara tu! Hii ni weak justification.

The only thing wanachotakiwa ni kuongeza mapato...since sometime it's bit hard to control cost, then the best option is to increase sales! Nitakubaliana na madai yao endapo tu watathibitisha kwamba wanakusanya bili kwa at least 90%....! Je, wote waliounganishiwa na kutumia umeme wanalipa bili zao? Kama wateja walipao bili hawafiki hiyo 90%, na si ajabu hata 60% hawafiki; then wao(akina TANESCO) ndio wanaotakiwa kuacha longo longo!! It's only the failure executive ndie ambae anaona the best way ya kuongeza mapato ni kuongeza bei!!

So, kama Muhongo anafanya siasa, basi TANESCO waje hadharani na data za kisomi za kuonesha ni asilimia ngapi ya mapato wanakusanya! Kama walitakiwa kukusanya sh.100 na sasa wanakusanya 70 and above, then Muhongo aache siasa na awaache TANESCO wafanye kazi yao. Lakini kama out of TZS 100, wao wanakusanya less or equal to TZS 40, then wao ndio waache professionalism politics!!
you are right.inawezekana hawakusanyi pesa sawasawa au wanazifakamia.Agekuwepo mtaalam wa hesabu hapa atuambie wanazalishe umeme kiasi gani,umeme unatumika kiasi gani?je hizo bilion 2.3 wanazokusanya ni sawa na MW ngapi?maana wasiwe wanawakilisha pesa za MW 50 ofisini afu wanadai wanakusanya za megawat 900.
 
Kazi ya Muhando na wenzake hii ili Muhongo ashindwe
 
Ni sahihi kwa kuwa unahisi Tanzania Daima wana smear campaign against Muhongo kwa kuwa mmiliki wake anahusishwa na chama cha upinzani. Na nyie masalia huwa hamuoni kizuri kutoka Tanzania Daima.

Pia huyo Muhongo unayesema sio malaika hana uwezo wa kumaliza matatizo ya sekta ya umeme Tanzania ambayo chanzo chake ni Kikwete kuileta IPTL wakati waziri enzi za Mwinyi na alipokuwa Rais ameileta Richmond.

Tatizo la umeme linasababisha umaskini na maisha duni kwa vijana wengi wa kitanzania na msipoangalia siku wakiingia mtaani nchi itashindwa kutawalika. Mnawanyima elimu bora hadi wanapata sifuri kwa wingi na mnawanyima umeme ambao wangeutumia hata kujiajiri kwa welding au ukinyozi
Mkuu funguka kwanza kimawazo na fikra badala ya kuanza kuniwekea fikra ambazo hata sina. Swala la Mmiliki wa Tanzania Daima na chama cha upinzani linaingiaje kwenye bandiko langu.

Nimeweke fikra zangu kutokana na maudhui ya habari na historia ya matatizo ya TANESCO na hakuna sehemu ambayo nimesema Mh Profesa Muhongo ni maraika. Tanzania Daima wao walichofanya ni cherry picking ili kutaka kutuaminisha kama matatizo ya TANESCO yanasababiswa na yeye.

Kama uko fair na unaweza kufungua mboni kuangalia historia, Matatizo ya TANESCO hayajaanza kipindi cha utawala wa Rais Mwinyi bali yamekuwepo tokea utawala wa Mwl Nyerere. Kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kumechangia tatizo kuwa ni kubwa kwa sababu ya mabadiliko ya hali hewa na hakukuwepo juhudi au plan za kuboresha sekta kukabiliana na hizo changamoto.

Kama ulipata elimu ya biashara utajua kama Kuna njia nyingi za kuongeza mapato siyo katika kupandisha bei tu.

Swala la kuwa kuna watu walikuwa wananufaika na TANESCO hilo halina ubishi, bali Tanzania Daima inapokuja na habari chokonozi bila hata ya kusema watu ambao imeongea nao badala yake inasema MANAGEMENT ni kutaka kutuaminisha kwa habari ambayo haijakamilika.
 
Kisingizio kuwa matatizo ya Tanesco yamekuja baada ya kuongezeka matumizi hakikubali hata kidogo. Ni sawa na mzazi anayezaa watoto wengi halafu anashindwa kuwalisha anasingizia wako wengi, au wanafika umri wa kwenda shule anakosa ada anasingizia watoto wengi wakati amewazaa yeye mwenyewe. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere amekufa hajui hata maana ya Capacity Charge, na serikali yake haijawahi kuingia mkataba wa kuzalisha umeme kwa bei kubwa kuliko ya kuuzia. Alijenga mabwawa na nchi ilikuwa inatumia umeme wa maji na majenereta baadhi ya wilaya. Tanesco wana MASTER PLAN yao ya miaka toka ya 70 imeainisha miradi na namna ya kuitekeleza na time frame yake. Sasa MaCCM mafisadi yalipoingia madarakani yametelekeza master plan na kuingiza miradi yao ya wizi ambayo wanufaikaji wakubwa ni akina Kikwete.

Hivi unajua kuwa hawa jamaa wanajenga Mtambo wa kuzalisha umeme Nyakato Mwanza kwa kutumia mafuta mazito yatakayokuwa yanatoka Dar kuja Mwanza kwa malory yao wakati miundombinu ya kusafirisha umeme toka Dar kuja Mwanza ipo. Wangezalisha umeme huko Dar na kusafirisha kwa miundombinu iliyopo, lakini kwa vile Ngeleja ndio alikuwa anaanzisha kampuni ya usafirishaji akajua kuwa ndio wakati muafaka wa kuibebesha nchi mzigo ili anufaike. Madhambi haya MaCCM mliyoitendea Tanesco kuna siku mtaumbuka vibaya sana.
 
Nani kakwambia mimi ni CCM?. Huwezi kuishi kwa hisia, tafuta ukweli kwanza ili ukufungue kimawazo na kimtazamo.

Hivi ni lini TANESCO ilijiendesha bila kutegemea mgongo wa serikali?. Na kwa kuwa iliishi kwa utegemezi ndiyo maana kuna watu wabaya (mafisadi) waliingilia kwa urahisi utendaji wake na matokeo yake ndiyo haya ambayo kuna mikataba mingine iliingia ambayo haina manufaa kwa mwananchi.

Majibu yako ya hoja kisiasa, ndiyo maana hutaki kuona madudu ya utendaji wa TANESCO ambayo yamepelekea kuwepo ufisadi katika utendaji.

Ndiyo wale wale, Baba wa Taifa hakufanya makosa!

anyway, endelea kuamini hivyo na tukubali kutokubaliana.
 
Wengi mnaochangia thread hii mnashindwa kuelewa undani wa matatizo ya TANESCO. Wachache wamechangia vizuri sana wakielezea ubovu wa mikataba, udhaifu wa uongozi ndani ya TANESCO kupanga na kusimamia utekelezaji wa mipango hiyo, na shirika kwenda na wakati.

Mimi ningepewa nafasi ya kuongoza shirika hilo watu wangeshangaa mafanikio yake ndani ya kipindi kifupi. Kinachopungua katika uongozi wa shirika hilo ni uadilifu na kutofuatilia mambo kwa karibu.

Anachofanya Maswi na Muhongo ni kuingilia kati masuala ya TANESCO pale wanapoona inabidi iwe hivyo kwa maslahi ya Taifa. Ni hakika, suala la nchi kuingia gizani halikubaliki kwa sababu yoyote ile.

Watu wanahitaji umeme, vyanzo vya umeme vipo, kwa nini viongozi wa shirika hilo wanashindwa kuwezesha upatikanaji wa uhakika wa huduma hiyo?

Ndio maana nimesema, nikipewa mwaka 1 tu wa kuongoza TANESCO nitafanya wonders chini ya viongozi hao makini Maswi na Prof. Muhongo.
 
Back
Top Bottom