Prof. Muhongo, Maswi watajwa kuiua TANESCO

Prof. Muhongo, Maswi watajwa kuiua TANESCO

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,892
WAKATI hali ya Shirika la Ugavi Tanzania (TANESCO) ni mbaya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakimu Maswi, wanatajwa kuwa chanzo cha kulidhoofisha kiuchumi shirika hilo, Tanzania Daima Jumatano, limedokezwa.

Vigogo hao wanadaiwa kuingilia shughuli za kiutendaji za shirika hilo kisiasa na kwa maslahi ya watu binafsi.

Vyanzo vya habari toka serikalini na TANESCO vinasema Muhongo na Maswi wamekuwa wakiliendesha shirika hilo kama taasisi binafsi kinyume na taratibu, jambo ambalo limesababisha hasara ya mabilioni ya shilingi kwa shirika hilo tangu waingie madarakani.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya shirika hilo, zinasema kuwa kumekuwa na msigano wa kimaamuzi kati ya shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini.

Inaelezwa kuwa wakati Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Felchesmi Mramba, akianzisha mchakato wa kuomba maoni ya wadau kupandisha bei, Waziri Muhongo aliibuka kupinga mawazo ya kupandisha bei kwa maelezo kuwa shirika lina pesa nyingi na serikali inalipatia ruzuku.

Mramba katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, alisema kuwa kwa hali ilivyo sasa, hata kama TANESCO ikiamua kutolipa mishahara wala isifanye matengenezo ya mitambo, isinunue vifaa vya kuunganishia wateja, au isiingie gharama nyingine zozote, bado ingepata hasara ya karibu sh bilioni 90 kila mwezi, hivyo lazima bei ya nishati hiyo ipande ili liweze kujiendesha.

Taarifa zaidi zinasema, menejimenti ya TANESCO haina mamlaka ya kuendesha kitaalamu shughuli zake isipokuwa Maswi na Muhongo ambao hawana sifa za utaalamu wa kuendesha shirika, huingilia utendaji.

“Maswi na Muhongo wamekuwa wakiingilia utendaji wa kila siku wa TANESCO kwa sababu za kisiasa na sasa shirika hilo linaelekea kufilisika kabisa kwani kwa sasa linatumia sh bilioni 5.4 kwa siku huku likikusanya sh bilioni 2.3 tu, hali hiyo imetokana na maamuzi ya kisaiasa yanayofanywa na viongozi hao,” alisema mtoa habari wetu.

Habari kutoka ndani ya TANESCO, zinasema kuwa Maswi na Muhongo hawataki bei ya umeme ipande kwani wamekuwa wakisema serikali ndiyo yenye shirika, menejimenti ya TANESCO ni chombo cha kuelekezwa namna ya kuiendesha tu.

Hivi majuzi, baada ya TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme Katibu Mkuu Maswi aliingilia kati kumshauri Mkurugenzi wa Ewura Haruna Masebu kuwa asikubali uamuzi wa TANESCO kwani ungeiaibisha serikali na walipofanikiwa Maswi alinukuliwa katika andiko moja akimwandikia Masebu kumpongeza:

“Bwana Masebu, naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa uungwana wako na kuamua kazi kwa kuilinda heshima ya serikali yetu. Heshima haina duka. Nakushukuru sana na naomba tuendelee kuisaidia serikali yetu pamoja na matatizo yaliyo mbele yetu. Kwa aina hii ya kushirikiana tutafika tu wala haina gogoro”

Wiki hii vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa nchi iko hatarini kuingia gizani wakati wowote kutokana na hali ya uzalishaji umeme kuwa tete TANESCO.

Inaelezwa kuwa hali ya shirika kifedha ni mbaya licha ya serikali kukwepa kukiri uwepo kwa mgawo ikihofia kubanwa kwa ahadi yake kuwa mgawo ungelikuwa historia.

Julai 28 mwaka jana, wakati wa kuhitimisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Muhongo na Naibu wake, George Simbachawene, walilihakikishia Bunge kuwa mgawo wa umeme ungelikuwa historia.

Lakini kwa takriban wiki nzima sasa, umeme umekuwa ukikatika hovyo kwa muda mrefu katika maeneo mengi nchini huku TANESCO ikitoa sababu za kawaida kuwa hali hiyo inatokana na matengenezo madogo kwenye miundombinu yake.

Habari zaidi za uchunguzi toka ndani ya TANESCO zinasema, hata mikopo ambayo shirika linapata sasa ni kwa ajili ya kulipa madeni tu wala sio kwa ajili ya kusaidia shirika hilo lisifilisike.

Ofisa habari wa TANESCO Badra Masudi alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alijibu kwa kifupi kuwa mchanganuo wa pesa za TANESCO uko wazi.

Waziri Muhongo alipoulizwa kupitia simu yake ya mkononi kuhusu suala hilo, alijibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye mkutano.

Baadaye alipoandikiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake ya mkononi, hakuweza kujibu.

Ujumbe alioandikiwa na gazeti hili ulisomeka hivi: “Mheshimiwa Waziri, jana Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO amesema shirika linaendeshwa kwa hasara na wewe ulisema wanakusanya pesa nyingi, sana, taarifa ipi ni sahihi? Pia tumepata taarifa kuwa unaiendesha TANESCO kisiasa; hufuati ushauri wa wataalamu nini maoni yako?”

Waziri alijibu tena kwa kifupi kwamba yuko kwenye mkutano. Jioni alipopigiwa simu, hakuweza kupokea.

Tanzania Daima pia ilimuandikia ujumbe wa simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini: “Mheshimiwa Maswi, unatuhumiwa kuingilia utendaji wa kila siku wa TANESCO, je ni kweli? Au una taarifa zozote kuhusu hili?” Katibu Mkuu hakujibu ujumbe wala kupokea simu.
 
Niliweka uzi hapa jamvini na kuhoji kati ya Muhongo na Ngeleja yupi bora?Ukweli huyu Muhongo anau hilo shirika kwasababu tofauti na Ngeleja yeye hataki kukubaliana na ukweli wa mambo.Hataki challenges na anapenda sifa za kijjinga.Mwenzake licha ya mapungufu yake alikubali lawama na kujikongoja na alikuwa muwazi kuhusu mgao wa umeme.Alikubali kushambuliwa ila sio huyu anaetaka kuonekana kidume wakati maji yamemfika shingoni.
 
Watanzania walivyo wanafiki,wanaoongoza kumshambulia Muongo sasa ni wale waliojipambanua kumpongeza wakati wa porojo zake bungeni just bcoz alimtuhumu mtu wanayepambana kumwangusha(Zitto).ilinishangaza hata wabunge wa upinzani kumpamba vile ktk mazingira tuliyonayo.ni upuuzi kuamini bila kuhoji itawezekana vipi kutokuwa na mgao wakati tunategemea mitambo inayolipiwa mabilioni kila mwezi pesa zinapatikana vipi.mtu kama Mnyika au Nasari wanakosa uhalali wa kumshambulia mtu waliyempamba kwa mbwembwe wakati ule.
 
Duru za kisiasa kutoka ndani ya shirika hilo, zinasema kuwa kumekuwa na msigano wa kimaamuzi kati ya shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini

Hapa ndo tunapokosea kuingiza siasa hadi kwenye masuala ya msingi.
 
Ni kawaida kabisa ya binadamu anapokuwa kwenye "confort zone", hatopenda kupata changamoto zinakazo hatarisha mazingira aliyonayo.

Waziri Profesa Muhongo anapambana na mtandao wa watu ndani ya TANESCO ambao wanadhani/wanaamini yuko pale kuhatarisha mazingira na maslahi waliyonayo. Kelele kama hizi siyo ajabu kuzisikia kutoka kwao kwa vile wanatumaini zitapata wateja ambao wako tayari ku-emplifier kama Tanzania Daima ili zipokelewe na watu waliobarikiwa fikra finyu.

Ni cha kushangaza kama siyo kuchekesha kufahamu kama kuna watu wanaamini TANESCO kabla ya profesa Muhongo ilikuwa kama maraika na kwa sasa imeingiliwa na jinamizi ( shetani) na linataka kuiua.
 
Mramba katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, alisema kuwa kwa hali ilivyo sasa, hata kama TANESCO ikiamua kutolipa mishahara wala isifanye matengenezo ya mitambo, isinunue vifaa vya kuunganishia wateja, au isiingie gharama nyingine zozote, bado ingepata hasara ya karibu sh bilioni 90 kila mwezi, hivyo lazima bei ya nishati hiyo ipande ili liweze kujiendesha.
Aina hiyo ya ubanaji wa matumizi wala hakuna anayesema kwamba ndio suluhisho la TANESCO hivyo ni upuuzi kudai hata kama watafanya yote hayo bado TANESCO itapata hasara tu! Hii ni weak justification.

The only thing wanachotakiwa ni kuongeza mapato...since sometime it's bit hard to control cost, then the best option is to increase sales! Nitakubaliana na madai yao endapo tu watathibitisha kwamba wanakusanya bili kwa at least 90%....! Je, wote waliounganishiwa na kutumia umeme wanalipa bili zao? Kama wateja walipao bili hawafiki hiyo 90%, na si ajabu hata 60% hawafiki; then wao(akina TANESCO) ndio wanaotakiwa kuacha longo longo!! It's only the failure executive ndie ambae anaona the best way ya kuongeza mapato ni kuongeza bei!!

So, kama Muhongo anafanya siasa, basi TANESCO waje hadharani na data za kisomi za kuonesha ni asilimia ngapi ya mapato wanakusanya! Kama walitakiwa kukusanya sh.100 na sasa wanakusanya 70 and above, then Muhongo aache siasa na awaache TANESCO wafanye kazi yao. Lakini kama out of TZS 100, wao wanakusanya less or equal to TZS 40, then wao ndio waache professionalism politics!!
 
ebu tujiulize, kipindi kama hiki kabla ya muhongo hali ilikuaje? Ama kweli watanzania watu ambao tunasahau kirahii rahisi tu.
Alipowagomea TANESCO kupandisha bei ya umeme nadhan sote tulimpongeza sasa iweje leo mnamwona yeye ndiye mbaya kwa kujaribu kutetea watu wa kipato cha chini.
Sikatai kwamba mgao hakuna japo upo lakini si kwa kiwango kikubwa kama kabla ya Muhongo kuingia madarakani.
Kwa upande wangu mgao huo sijau experience kabisa nausikia kwa watu tu.
Huwezi mlinganisha ngeleja na muhongo, ngeleja alikuwa zaidi ya mchumia tumbo asiyekuwa na hata chembe ya huruma
 
Hayo ni majungu acha wafanye kazi . Wengi ni vibaraka wa akina Ngeleja
 
Waziri kutetea walalahoi imekuwa kosa? Fanyeni kazi kwa makini kusanyeni bill zenu kwa usahii. Sio kupandisha bei haitosaidia ni kumuumiza mlalahoi tuhuduma zenu ni takataka acha waziri awafukuze tu hamna lolote ufisadi tupu
 
Tunatakiwa kuwa more analytical and logical. Kwa ujumla ni kuwa TANESCO na serikali kwa ujumla wameshindwa kufanya kazi. Kinachotokea sasa siyo matokeo ya utendaji wa sasa wala siyo sababu ya Muhongo. Tatizo kubwa la sasa ni uwezo mdogo wa TANESCO kulipia gharama za umeme unaozalishwa na makampuni mbalimbali. Matatizo haya yanaanzia wapi? Matatizo yanaanzia kwenye mikataba:

  • Mikataba iliyofungwa kati ya TANESCO na wazalishaji wa umeme ni ya kifisadi na ya ajabu. Kuna mikataba ambayo inalazimisha TANESCO kuwalipa wazalishaji wa umeme hata kama TANESCO haikutumia umeme wao. Lipo pia suala la bei ya ununuzi kwa unit toka kwa wazalishaji kuwa juu mno. Bei unayonunulia ipo juu halafu usiponunua unaendelea kutozwa, uliona wapi mikataba ya kijinga kiasi hicho?

  • Mikataba hii imeandaliwa na nani? Kwa vyovyote siyo prof. Muhongo aliyeiandaa. Ipo iliyoandaliwa wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa pia. Ipo iliyoandaliwa wakati wa Jakaya, Ngeleja/Msabaha wakiwa mawaziri. Hakuna mkataba ulioandaliwa wakati wa Muhongo.

  • Nadhani Muhongo aliposema hakuna mgao aliangalia tu uwezo wa uzalishaji umeme kwa nchi nzima, hakuangalia kwa umakini uwezo wa TANESCO kuununua umeme huo.

  • Unaposema matatizo ya TANESCO yanasabaishwa na waziri/viongozi wa siasa kuingilia, je TANESCO imewahi kufanya vizuri wakati wowote ule wakati ambao haikuingiliwa na wanasiasa? Si vizuri wanasiasa kuingilia uendeshaji wa TANESCO lakini serikali itakosa vipi kuingilia TANESCO wakati kila siku TANESCO ipo mlangoni mwa serikali kuomba hela? Hii ni sawa na mtoto aliyekua akaamua kuwa na familia yake lakini kila siku yupo kwa baba yake kuomba hela ya chakula na matibabu kwaajili ya familia yake, ukifanya hivyo ni lazima Baba ataingilia maisha yako. Atapenda kukusimamia ili ajiridhishe kama kukosa kwako hela kila mara hakutokani na uvivu wa kufanya kazi, uzembe, uwezo na mbinu hafifu au matumizi mabaya ya mapato. Na hivyo ndivyo ilivyo TANESCO. TANESCO haijawahi hata mara moja kusimama kwa miguu yake

    Duru za kisiasa kutoka ndani ya shirika hilo, zinasema kuwa kumekuwa na msigano wa kimaamuzi kati ya shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini

    Hapa ndo tunapokosea kuingiza siasa hadi kwenye masuala ya msingi.
 
Kwa mfano tu: Unanunua unit 1 kwa sh. 70/- na wewe unaiuza sh. 50/- Unanunu jumla ya unit 100 lakini unauza 70 tu kwa sababu miundombinu ni mibovu hivyo zingine zinapotelea njiani.

Umeme unakatika katika mji mzima wa wilaya na inakuwa hivyo siku tatu. Wewe unanunua lakini huuzi kwa kuwa umeme umekatika na huikutengeneza.

Licha tu ya capacity charge unayowalipa hao unaonunua kwao lakini pia gharama zako za uendeshaji za ndani ni kubwa sana.

Ukichanganya na ufisadi wa tenda za manunuzi uliokithiri unaweza kudhani kuwa dawa ni kupandisha bei ya bidhaa yako.

Ndio maana mtu mmoja aliuliza hapa JF kuwa hivi TANESCO wanao wanauchumi au wanaendeshaje shirika lao? Tatizo sio bei ya umeme kuwa ndogo hata kidogo.

Ndo maana Ndg Maswi akapinga kuwa wasiruhusiwe kupandisha bei ila wayapatie ufumbuzi matatizo yao ya ndani yanayosababisha hasara.

Umeme ungekuwa haukatiki ovyo na kama ukikatika kama ungerudishwa kwa muda mfupi wangeokoa fedha nyingi mno!
 
Watanzania walivyo wanafiki,wanaoongoza kumshambulia Muongo sasa ni wale waliojipambanua kumpongeza wakati wa porojo zake bungeni just bcoz alimtuhumu mtu wanayepambana kumwangusha(Zitto).

Ilinishangaza hata wabunge wa upinzani kumpamba vile ktk mazingira tuliyonayo.ni upuuzi kuamini bila kuhoji itawezekana vipi kutokuwa na mgao wakati tunategemea mitambo inayolipiwa mabilioni kila mwezi pesa zinapatikana vipi.

Mtu kama Mnyika au Nasari wanakosa uhalali wa kumshambulia mtu waliyempamba kwa mbwembwe wakati ule.

.......

Mkuu bora umeliona hili... sisi watanzania wenyewe tuna matatizo makubwa sana ya ushabiki na kutokujitambua, ndio sababu viongozi wanatuchezea wanavyotaka. Yani akitokea mtu anayesema ukweli anashambuliwa na kuonekana mbaya na kila mtu...

Zitto aliendelea kuitwa yale majina ya mkurupukaji asiyejua analofanya, anatafuta sifa, ana bifu na prof and all that, lakini uzuri wa ukweli ndio huu, wala hauchukuwi muda kuonekana!!!

Saizi eti Mnyika ndie yuko mstari wa mbele kumsakama Muhongo, lakini Maswi na Muhongo waliposuka mbinu za kumchafua Zitto wote walimshangilia. Tanzania eeee, wana JF hapa walikuwa wanaimba kwamba Muhongo ni profesa wa ukweli, Zitto anataka kumzima... haya sasa endeleeni kushangilia.
 
Nashauri msiongee vitu msivyovijua jamanii....hakuna hata sababu moja ya kumlaumu mhongo....kuna watu nje na ndani ya tanesco wanajaribu kumchafua..

Naomba mjiulize swali moja tu mramba wa tanesco anasema zaidi ya bil 5 zinatumika kulipia maafuta kwa siku wakati mapato ni bil 2.

Naomba mjiulize maswali yafuatayo:-

1. Hizo bil.5 kwa nini zinapigiwa debe zilipwe kwenye mafuta wakati kuna mambo mengine mengi ya kuliendeleza shirika?

2. Ni kina nani ndani ya serikali (sio prof.muhongo) ambao wanafanya biashara hii ya mafuta na tanesco?

3. Kwa nini uzalishaji wa umeme kwa kutumia mitambo inayotumia mafuta inapigiwa debe sana kuliko njia
zingine za unafuu sana za kuzalisha umemem kama kwa kutumia maji na gesi? Kuna mikono ya watu
wengi sana inanufaika na biashara hii ya mafuta na tanesco.

Hii imepelekea mpaka zisambazwe propaganda kwamba umeme wa maji sio reliable na haututoshi....kuna miradi mingi sana ndani ya tanesco inayohusu kuzalisha umeme kwa maji kama stigler gauge n.k inafunikwa na kupotezewa kabisa kwa sababu tu itahatarisha biashara zao za kuizia mafuta tanesco.

Wananchi tuamke tuache kujazwa ujinga....tanesco haistahili kuwa maskini wala kufilisika...ila hawa watu wanaofanya biashara na tanesco ya mafuta (wengi wao ni viongozi wa serikali) wako tayari hata wafanyakazi wa tanesco wasilipwe mishahara au vifaa muhimu visinunuliwe ili wa;ipwe pesa zao za mafuta...na wanafnya viongozi wa tanesco wanavyotaka...

Ndio maana ni rahisi sana kumuona hata mkurugenzi mkuu wa tanesco anatetea kuwalipa makampuni za mafuta kwa hasara..

Watanzania tuamke sasa...prof. Muhongo hana hatia wanajaribu kumchafua sana hasa kupitia vyombo vya habari....na na baadhi yenu bila kujijua mnajiunga kumlaumu kwa pamoja

hitimiso lanhu ni kama ifuatavyo:

1. Hasara na matatizo yote ya kifedha yanayoikumba tanesco yanatokana na kupeleka makusanyo yote wanayoyapata kwenda kuwalipa makampuni ya mafuta yanayosambaza mafuta katika mitambo feki ya kuzalisha umeme...

2. Taarifa zinazosambazwa za kuponda uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni za uongo na badili ili waalalishe uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta na wachache wao waendelee kunufaika....nawaomba watanzania tuepukane na huu mkumbo..narudia...miradi mingi ya kuzalisha umeme kwa njia zenye faida kama maji zinapigia chapuo zionekane hazifai...lakini ukweli ni kwamba tanzania tuna maji ya kutosha kuzalisha umeme na ni njia nafuu kuliko zote....jiulize kwa nini mradi wa stiglers gauge wa mto ruaha ambao haukauki mwaka mzima...chonde chonde watanzania itakuwa tumefanya dhambi isiyosameheka kwa kumsemea maneno mabaya prof.mhongo.
 
]Ni kawaida kabisa ya binadamu anapokuwa kwenye "confort zone", hatopenda kupata changamoto zinakazo hatarisha mazingira aliyonayo.

Waziri Profesa Muhongo anapambana na mtandao wa watu ndani ya TANESCO ambao wanadhani/wanaamini yuko pale kuhatarisha mazingira na maslahi waliyonayo. Kelele kama hizi siyo ajabu kuzisikia kutoka kwao kwa vile wanatumaini zitapata wateja ambao wako tayari ku-emplifier kama Tanzania Daima ili zipokelewe na watu waliobarikiwa fikra finyu.

Ni cha kushangaza kama siyo kuchekesha kufahamu kama kuna watu wanaamini TANESCO kabla ya profesa Muhongo ilikuwa kama maraika na kwa sasa imeingiliwa na jinamizi ( shetani) na linataka kuiua.

.......

Ni uwendawazimu wa hali ya juu sana kutaka vyombo vya habari viwe vinaandika habari za kusifia serikali tu na sio kukosoa. Kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuunga mkono biashara inayofanywa na Tanesco ya kununua umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo.

Nyie CCM ndio mmetuingiza kwenye huu mkenge na makampuni yote yanazalisha umeme ni ya kwenu vigogo wa CCM (Ingawa wewe N'mapalala ni maskini tu).

Kitanzi ambacho viongozi wa CCM na mafisadi partners wenu mmeiingiza Tanesco haiwezi kutoka. Either bei ya umeme ipande mara dufu ili kuzuia tishio la Tanesco kufa au serikali hii maskini inayoshindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake iwe ina BAIL OUT Tanesco kila mwezi.

Cha kujiuliza: Wakati mnaingia hii mikataba ya uzalishaji umeme na haya makampuni ya mafisadi wa CCM hamkujiuliza kuhusu tofauti ya bei ya kununua na kuuza umeme. Kama maCCM mngekuwa na akili msingekubali kuingia mikataba ya kununua umeme kwa 1000 na kuuza kwa 500.

Ni heri mngeacha nchi ibakie gizani na kuiwezesha Tanesco kidogo kidogo kununua mitambo yake hadi kufikia kuzalisha umeme wa kutosha kuliko mlivyofanya kuiingiza Tanesco kwenye mikataba itakayofilisi shirika.

Hapa mtalaumu Mramba, Muhongo, sijui Maswi lakini chanzo cha tatizo ni Kikwete siku ile anaileta Richmond[/SIZE]
 
Hapo umenena, kuincrease sales wawakabe wateja Wao ( wakusanye 90%+ ya bili)
Waongeze efficiency katika mitambo Yao
Then ndo wafikilie kuongeza bei ya umeme.
Hata hivyo watuonyeshe hilo ongezeko litaongezaje ufanisi wa TANESCO na utekelezaji wa kuanzisha new source ya power owned by them sio tena mambo ya capacity charges
 
Ni uwendawazimu wa hali ya juu sana kutaka vyombo vya habari viwe vinaandika habari za kusifia serikali tu na sio kukosoa. Kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuunga mkono biashara inayofanywa na Tanesco ya kununua umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo.

Nyie CCM ndio mmetuingiza kwenye huu mkenge na makampuni yote yanazalisha umeme ni ya kwenu vigogo wa CCM (Ingawa wewe N'mapalala ni maskini tu).

Kitanzi ambacho viongozi wa CCM na mafisadi partners wenu mmeiingiza Tanesco haiwezi kutoka. Either bei ya umeme ipande mara dufu ili kuzuia tishio la Tanesco kufa au serikali hii maskini inayoshindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake iwe ina BAIL OUT Tanesco kila mwezi.

Cha kujiuliza: Wakati mnaingia hii mikataba ya uzalishaji umeme na haya makampuni ya mafisadi wa CCM hamkujiuliza kuhusu tofauti ya bei ya kununua na kuuza umeme. Kama maCCM mngekuwa na akili msingekubali kuingia mikataba ya kununua umeme kwa 1000 na kuuza kwa 500.

Ni heri mngeacha nchi ibakie gizani na kuiwezesha Tanesco kidogo kidogo kununua mitambo yake hadi kufikia kuzalisha umeme wa kutosha kuliko mlivyofanya kuiingiza Tanesco kwenye mikataba itakayofilisi shirika.

Hapa mtalaumu Mramba, Muhongo, sijui Maswi lakini chanzo cha tatizo ni Kikwete siku ile anaileta Richmond[/SIZE]
Ninafikiri hili bandiko lako umeliunganisha na bandiko langu kimakosa kwa sababu unachoongea ni nje ya kile nilichoongea.

Soma kwanza bandiko langu ili uelewe nini nimeandika ili kama ukipenda ujenge hoja kuhusiana na hilo na hilo siyo generalization.

By the way, take a note, Mimi siyo CCM na sijawahi kukuambia kama mimi ni CCM. Kwani wewe ni nani?. Ninachokiandika hakiusiani na CCM bali kinahusiana na fikra na mtizamo wangu.
 
TANESCO inakabiliwa na matatizo ya ndani kwa maana ya muundo na utendaji wake na ya nje kwa maana ya mikataba mibovu ambayo serikali iliingia na makampuni ya kimataifa.
  1. TANESCO wanapaswa kuimarisha kitengo chake cha kukusanya ankara. Walinganishe uzalishaji wao na mapato.
  2. TANESCO wanapaswa kudhibiti matumizi yao ikiwa ni pamoja na kuwafichua watumishi wanaolihujumu shirika kwa kufanya malipo hewa.
  3. TANESCO wapime utendaji wao (efficiency) kulinganisha na idadi yao.
Kwa upande wa serikali embu fanya yafuatayo:
  1. Pitia upya mikataba yenu kwa niaba ya TANESCO. Hivi kweli TANESCO ikifa leo hizo capacity charges zitaendelea kulipwa na serikali au makampuni hayo ya kimataifa yatahama na kutafuta biashara sehemu nyingine?!
  2. Wekeza zaidi katika miundombinu ya TANESCO.
 
Ninafikiri hili bandiko lako umeliunganisha na bandiko langu kimakosa kwa sababu unachoongea ni nje ya kile nilichoongea.

Soma kwanza bandiko langu ili uelewe nini nimeandika ili kama ukipenda ujenge hoja kuhusiana na hilo na hilo siyo generalization.

By the way, take a note, Mimi siyo CCM na sijawahi kukuambia kama mimi ni CCM. Kwani wewe ni nani?. Ninachokiandika hakiusiani na CCM bali kinahusiana na fikra na mtizamo wangu.

.......

Ni sahihi kwa kuwa unahisi Tanzania Daima wana smear campaign against Muhongo kwa kuwa mmiliki wake anahusishwa na chama cha upinzani. Na nyie masalia huwa hamuoni kizuri kutoka Tanzania Daima.

Pia huyo Muhongo unayesema sio malaika hana uwezo wa kumaliza matatizo ya sekta ya umeme Tanzania ambayo chanzo chake ni Kikwete kuileta IPTL wakati waziri enzi za Mwinyi na alipokuwa Rais ameileta Richmond.

Tatizo la umeme linasababisha umaskini na maisha duni kwa vijana wengi wa kitanzania na msipoangalia siku wakiingia mtaani nchi itashindwa kutawalika. Mnawanyima elimu bora hadi wanapata sifuri kwa wingi na mnawanyima umeme ambao wangeutumia hata kujiajiri kwa welding au ukinyozi
 
ebu tujiulize, kipindi kama hiki kabla ya muhongo hali ilikuaje? Ama kweli watanzania watu ambao tunasahau kirahii rahisi tu.
Alipowagomea TANESCO kupandisha bei ya umeme nadhan sote tulimpongeza sasa iweje leo mnamwona yeye ndiye mbaya kwa kujaribu kutetea watu wa kipato cha chini.
Sikatai kwamba mgao hakuna japo upo lakini si kwa kiwango kikubwa kama kabla ya Muhongo kuingia madarakani.
Kwa upande wangu mgao huo sijau experience kabisa nausikia kwa watu tu.
Huwezi mlinganisha ngeleja na muhongo, ngeleja alikuwa zaidi ya mchumia tumbo asiyekuwa na hata chembe ya huruma

Kaka uko maeneo gani ambayo huu mgao haufiki.?
 
Back
Top Bottom