Prof muhongo huu si uongo?

Awaulize Watanzania watumiaji wa umeme badala ya kukurupuka na kutoa kauli fyongo. Afuatilie habari katika vyombo mbali mbali vya habari nchini vikiwemo TV, Radio, Magazeti n.k.

kama mgao haupo nyumbani kwake na ofisini kwake atasemaje kuna mgao?
 
Huyu Profesa nimemuhogopa aisee yaani hata aibu haoni kweli ukiwa na ujasiri wa huyu jamaa unaweza kusema chochote bila hata kupepesa macho huku ukijua kuwa ni uongo jamaa kiboko huyu
 
tatizo maprofesa ccm hutumika ndivyo sivyo, hulazimishwa watende wasiyoamini na waamini wasiyoyatenda1
mfano alikuwepo profesa sarungi wengi wanafahamu alivyoiongoza vyema muhimbili akiwa mkurugenzi lakini alipohamia kwenye siasa utafikiri aliukana uprofesa wake kwa jinsi kuboronga kulivyokuwa kila kona!
 
...Ngeleja mwingine huyu, tuliambiwa kichwa sana hana hata ukichwa wowote. Utakuwaje kichwa halafu uendelee kusema uongo kwamba hakuna mgao wakati kuna mgao katika maeneo mengi nchini na watumiaji wa umeme wanaweza kuthibitisha hilo.
Tulipofika watanzania sasa ni kila kitu kulaumu. Hatuna muda wa kufikirisha akili zetu. Hivi ni nani aliyesema kwamba maadam mgawo haupo basi kukatika kwa umeme ndiyo mwisho wake? Nadhani kuna tatizo la uelewa kuhusu mgawo wa umeme. Prof. Muhongo is and will remain to be a hero in this important Ministry. He has done a lot within thia short period since his appointment as the Minister.
 
Ushasahau kuwa huyu Muhongo ni katika list ya wana CCM wanaopendwa hapa JF?

Wengine ni:
Magufuli
Mwakyembe

Ukitaka ugomvi na wana JF ambao husema kuwa CCM ni mafisadi bas wewe waguse hao waheshimiwa

Typical JF double standards

Double standard kivipi? yani mtu akilifanyia taifa jambo jema asisifiwe?
 
Labda anahujumiwa na watendaji wa chini yake.
Huku Mwanza maeneo ya Nyakato upande wa Nundu mchana ulikuwa na umeme na maeneo ya Florida Hotel hayakuwa na umeme. Usiku huu, maeneo ya Florida hotel yana umeme na maeneo ya Nundu hayana. Huu ni mgao kweli wala asidanganye Watanzania.
 
...hakuna "mgao" jamani hamuelewi, nchi inaongozwa kwa imani sasa...ukisema hakuna mgao inatakiwa wananchi waamini hata kama umeme hakuna...

...nahisi kuna haja ya waziri kuulizwa maana ya mgao..labda kuna tafsiri mpya ambayo watu hatujaipata...
 
...hakuna "mgao" jamani hamuelewi, nchi inaongozwa kwa imani sasa...ukisema hakuna mgao inatakiwa wananchi waamini hata kama umeme hakuna...

...nahisi kuna haja ya waziri kuulizwa maana ya mgao..labda kuna tafsiri mpya ambayo watu hatujaipata...

dhana ya mgao kwake inamaanisha walionacho hawatakuwa na mgao na wasionacho mgao ndio maisha yao!
 
Alikuwa anashughulikia mafuta kwanza bandarini amemaliza sasa mpeni muda kidogo anakuja kwenye umeme! Tuvumilieni.
 
huku ubungo,kimara hadi mbezi umeme unakaa siku 2 ya 3 giza.hapa nilipo nipo gizani.mwenge nako juzi nilienda ni hivyo hivyo!
 
Chezea Muhongo nyie!
Ninapoandika 80% ya daa hakuna umeme!
Chezea ccm nyie

mkuu nipo kwenye sherehe ya graduation ya jirani yangu hp mbezi. tunatumia taa za gari kwa ajili ya mwanga na mc anatumia koromeo lake. simlaumu muhongo ni system yote imeoza. kick ccm out of tanzania.
 
huko dodoma pamoja na kwamba kipindi cha bunge umeme nao unakatikakatika sanaaa tuu, halafu bila taarifa yeyote, afadhalini nyie wa dsm badra anawakumbukakumbuka kuwataarifu ingawaje sio mara zote kwamba watakata.
Huku mikoani hatukuswagi kabisa na hayo matangazo yao ya kwenye magazeti kwamba watakata mita fulani na fulani.
Yaani kunajamaa yngu jana kanunua umeme wa luku wa buku 20 ili leo afanye kazi zake vizuri,asubuh tu saa 2 wakakata jamaa akabaki kulalamika na luku yake nikamwambia hazitatumika akabakia naalalmika alikuwa anakazi ya deadline leoleo.
 
....that is your opinion but to most Tanzanians he has done nothing so far, he is a replica of fisadi Ngeleja.

 
Mgao wa umeme upo Prof Muhongo acha uhongo.
 

yes he has done a lot....

Kugeuza jina mgao wa umeme toka 'mgao hadi 'hitilafu'

ninapoishi tushazoea, tusipokatiwa saa tatu subuhi hadi saa kumi tutakatiwa saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri.......

Hitilafu za jumatatu hadi jumapili for sure he is a hero....
 

Inaitwa KICHONGEO au kwa kiswahili fasaha KIFILIO.
 
Jeshi la mtu mmoja ( profesa ) limezungukwa na Majeshi ya Mafisadi yanayopanga kila kukicha hujuma...

dhidi ya utendaji wake makini..ili hali tu wamuwangushe kimikakati na mpango wake wa kutetea watanzania...

unategemea nini.??!..Unafikili Mafisadi wanapata usingizi dhidi ya profesa.?!!..,hata kidogo, vita ni kubwa sana...

ndani ya Bunge ( kamati ya Ngwilizi ) na hata Nje ya ofisi yake....

Hatari sana Nchi hii.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…