Prof. Mlambiti wa SUA - Jiwe lililosahaulika

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,341
Reaction score
15,829
Leo nimekua nikitafakari mambo mbalimbali yanayoikabili nchi hii na nikajikuta namkumbuka prof.Mlambiti kwa mambo mbalimbali na jinsi alivyokua anaonesha hisia zake anavyoumizwa na mustakabali wa nchi hii.

Kwanza hajawahi kuamini kama CCM inania ya dhati ya kuikwamua nchi hii kiuchumi na kimaendeleo japo anaamini kuna watu ndani ya CCM wangeweza kujilipua na kuifikisha TZ mbali sana na hawakuwahi kufanya hivyo na hawatofanya hivyo... Akiwemo Raisi wa sasa na aliyepita kabla yake (Mkapa).

Prof. Mlambiti (a.k.a Babu) alitufundisha pale SUA miaka ya 2000 mwanzoni ni mtu aliyethubutu mara kadhaa kupingana na Mwalimu Nyerere juu ya Sera za kilimo za nchi hii akiamini ubunifu juu ya kilimo ungekomboa zaidi 80% ya wananchi wa TZ kama serikali ikiamua kuwekeza katika tafiti na rasilimali zingine pamoja na ukuzaji wa viwanda na masoko ndani na nje ya nchi.

Prof. Mlambiti daima fikra zake haziwezi kufa kichwani mwa mtu yeyote aliyemfundisha kwa kuwa aliongea maono, ukweli, na hali halisi bila kujali itikadi zozote na alisema ni kizazi kingine ndicho kitaibadilisha Tanzania na ni kizazi kitakachokuja kuishangaa sana historia ya kizazi hiki cha sasa kwa uzembe na uvivu mkubwa wa kufikiri.

Prof. Mlambiti ambaye alitufundisha sana elimu ya ujasiriamali (japo ilikua kama kitu kigeni sana kwa jamii ya TZ) ni mzee aliyetuhamasisha sana vijana kuumiza akili na kujitengenezea ajira kuondokana na utumwa wa fikra ambao vijana wote wa wakati ule tulikua nao.. Na waliofuata aliyoyafundisha na kuthubutu si wenzetu tena leo hii kiuchumi.

Ni mtu pekee ambaye huja mara nyingi kichwani mwangu kila linapotokea vuguvugu la uchaguzi, scandal za kifisadi,migogoro ya ardhi, migogoro ya kidini na hata migogoro ya kiuchumi kwa sababu ya maono na mafundisho yake na mara zote huwa natamani nijue ni nini anafikiria kwa wakati huo.

Kiufupi mzee yule ni hazina kubwa iliyosahaulika..na yeyote aliyewahi kuhudhuria darasa lake hawezi kusahau maishani mwake mafundisho ya yule mzee.
 
Yuko vizuri huyo prof nilishwahi kuona kitabu chake "yellow book" kinachozungumzia uchumi kilimo kwa east Africa

Hizi hazina zimesahaulika kabisa
 
Alipaswa tu kueleza kile kinachatakiwa kufanyika bila kutaja Nyerere maana iko shida kwa watanzania wengi ukishampinga Nyerere wanasahau hoja. kumbuka mfumo wetu wa elimu unatuongoza kushindana nani anamzidi mwenzake kuliko kuangalia uhalisia wa kitu kinachozungumzwa. Ukimpinga Nyerere watu wanafikiri unataka kuwa maarufu kuliko yeye hoja yako haitafuatwa. Inapaswa sasa ninyi mlioona uzuri muuonyeshe kwa vitendo
 
Namkumbuka sana huyu Professor.

Aliwahi kutuambia anajisikia vibaya sana kufahamu mambo mengi maovu ya serikali hii na kila akijaribu kutoa ushauri watu wanaendekeza kuingiza siasa tu..
 
yupo saut mwanza siku hizi, amechoka sana pia umri umesogea sana. Kuna tetesi kuwa alishawahi kunyang'anywa vyeti vyake kwa kukosoa utawala wa ccm, kuna mwenye kujua hili atufunue kidogo macho
 
namkumbuka kama mgombea ubunge jimbo la ulanga magharibu kipindi kile cha t.l.p inawika alichakachuliwa kula karibu mara 3 mpaka akakata tamaa kwenye siasa
 
Prof. Pereka yuko wapi jamani. Physiologist wa kutisha. Amenijengea foundation ambayo haisahauliki kichwani kwangu. Nikienda hosp sipati shida na nikidanganywa naelewa
 
Wao wenyewe ndio hawajataka kumuongezea mkataba.

Kuna kipindi alikuwa anaogopwa kwamba anatema sumu.. Labda SUA waliogopa hilo... Maana ingekua enzi hzo chadema iko moto lazima angehusishwa nao
 
Leo nimekua nikitafakari mambo mbalimbali yanayoikabili nchi hii na nikajikuta namkumbuka prof.Mlambiti kwa mambo mbalimbali na jinsi alivyokua anaonesha hisia zake anavyoumizwa na mustakabali wa nchi hii.

Kwanza hajawahi kuamini kama CCM inania ya dhati ya kuikwamua nchi hii kiuchumi na kimaendeleo japo anaamini kuna watu ndani ya CCM wangeweza kujilipua na kuifikisha TZ mbali sana na hawakuwahi kufanya hivyo na hawatofanya hivyo... Akiwemo Raisi wa sasa na aliyepita kabla yake (Mkapa).

Prof. Mlambiti (a.k.a Babu) alitufundisha pale SUA miaka ya 2000 mwanzoni ni mtu aliyethubutu mara kadhaa kupingana na Mwalimu Nyerere juu ya Sera za kilimo za nchi hii akiamini ubunifu juu ya kilimo ungekomboa zaidi 80% ya wananchi wa TZ kama serikali ikiamua kuwekeza katika tafiti na rasilimali zingine pamoja na ukuzaji wa viwanda na masoko ndani na nje ya nchi.

Prof. Mlambiti daima fikra zake haziwezi kufa kichwani mwa mtu yeyote aliyemfundisha kwa kuwa aliongea maono, ukweli, na hali halisi bila kujali itikadi zozote na alisema ni kizazi kingine ndicho kitaibadilisha Tanzania na ni kizazi kitakachokuja kuishangaa sana historia ya kizazi hiki cha sasa kwa uzembe na uvivu mkubwa wa kufikiri.

Prof. Mlambiti ambaye alitufundisha sana elimu ya ujasiriamali (japo ilikua kama kitu kigeni sana kwa jamii ya TZ) ni mzee aliyetuhamasisha sana vijana kuumiza akili na kujitengenezea ajira kuondokana na utumwa wa fikra ambao vijana wote wa wakati ule tulikua nao.. Na waliofuata aliyoyafundisha na kuthubutu si wenzetu tena leo hii kiuchumi.

Ni mtu pekee ambaye huja mara nyingi kichwani mwangu kila linapotokea vuguvugu la uchaguzi, scandal za kifisadi,migogoro ya ardhi, migogoro ya kidini na hata migogoro ya kiuchumi kwa sababu ya maono na mafundisho yake na mara zote huwa natamani nijue ni nini anafikiria kwa wakati huo.

Kiufupi mzee yule ni hazina kubwa iliyosahaulika..na yeyote aliyewahi kuhudhuria darasa lake hawezi kusahau maishani mwake mafundisho ya yule mzee.
Angekuwa amekula kichwa chako ukashindwa kugraduate hiyo Agribusiness yako ungemsifia hivyo hivyo? Kwa nini usiwasifie akina Sembuche wa Statistics?
 
Sembuche kwa sasa yuko kwao kigugu turian kastaafu hili n gwiji la mathematics sijawah ona alikua UDSM miaka ya 70s na akaenda Zimbabwe miaka ya 80s na baadae kwenda sua 1998 na sasa kastaafu
 
Umenikumbusha hisia alizo nazo prof. Tarimo.
Katika Dept ya Eng. Pale sua. Inamuuma sana wanasiasa wanapoongea kuhusu miradi mbali mbali ya maji.ambayo mingi imekufa kwa uzembe wa hawa watu.
 
Angekuwa amekula kichwa chako ukashindwa kugraduate hiyo Agribusiness yako ungemsifia hivyo hivyo? Kwa nini usiwasifie akina Sembuche wa Statistics?

Mkuu kwanza tambua mi sikusoma Agribusiness.. Pili hilo la kudisco halihusiani kabisa na kusudi la mada.. Nilishindwa kukamatwa PS 100 nije nikamatwe wapi tena mkuu.. PS 100 ilikua inawadisco watu mwaka wa kwanza tu na haikushangaza
 
Prof. Pereka yuko wapi jamani. Physiologist wa kutisha. Amenijengea foundation ambayo haisahauliki kichwani kwangu. Nikienda hosp sipati shida na nikidanganywa naelewa

Bibi yupo bado anakimbiza cardiovascular kinoma! Alishastaafu ila kwa sasa anapiga kwa mkataba!!
 
Back
Top Bottom