Prof Mbilinyi amsugua Mkapa na sabuni ya Geisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Mbilinyi amsugua Mkapa na sabuni ya Geisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Giro, Feb 12, 2009.

 1. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Katika mahojiano yake yaliochapishwa katika gazeti la RAI alhamisi iliyopita,Waziri wa fedha wa zamani katika serilikali ya awamu ya tatu,Profesa Simoni Mbilinyi amejitosa katika mjadala unaomhusisha rais mstaafu Benjamini Mkapa,
  Profesa Mbilinyi anasema aneyestahili kuchunguzwa ni Anna Mkapa wala si mumewe Benjamini Mkapa.Mbilinyi anasema hatua ya kumpeleka Mkapa mahakamani inaweza kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.
  ***************************************************************
  Wakati hayo yakijiri,serikali imebanwa na Bunge kiasi cha kulazimika kuanza kufikiria uamuzi wa kisheria na hata kutafakari fursa ya kumwondolea kinga Raisi Mkapa, au kumuhoji kuhusu mgodi wa makaa ya mawe kupitia kampuni ya ANBEN.Habari za kuaminika zina sema umiliki wa mgodi huo ulifanyia mabadiliko kutokana na mwenendo wa mambo na hasa baada ya suala hilo kuonekana kumuweka pabaya kisiasa na kisheria Mkapa.Katika mabadiliko hayo nyaraka za sasa zinabainisha kuwa mgodi huo unamilikiwa na kampuni ya Tanpower Resource Ltd,ambayo ni muungano wa kampuni nne tofauti
  (1)Fosnick Ltd..ambayo wanahisa wake ni Nick Mkapa,Foster Mkapa na mwingine anayetambulika kama B.Mahembe
  (2)Choice Industries--ambayo wanahisa wake ni Joe Mbuna na Goodyear Francis
  (3)Devconsult Ltd--wanahisa wake ni D.Yona na Dan Yona jr
  (4)Technologies Ltd--wanahisa wake ni Wilfred Malekia na Evans Mapundi
  Habari za kuaminika zinasema tayari nyaraka za awali (original) zenye kuonyesha kuwa mgodi wa Kiwira unamilikiwa na kampuni ya ANBEN ambayo ni ya Mkapa,zimefikishwa katika uongozi wa juu wa Bunge nyaraka hizo zimejitosheleza kiushahidi kwamba Mkapa ni mmiliki wa ANBEN.

  Mkapa si msafi ana kutu hivyo hata kama kina Mbilinyi na wenzake watamuogesha na kumsugua na sabuni ya mbuni mara tano kwa siku.Mkapa katu hato kuwa msafi ,labda tumpake rangi(afikishwe mahakani akajibu)
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama Prof Mbilinyi anasema Mama Mkapa ndio wa kumkazia macho...basi ni vema kumsikiliza..japo kwa sasa..!! Prof atakuwa anajua anachokisema.
   
 3. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  The fact is huyu jamaa hasafishiki kwa sasa. Either unatumia mbuni au geisha, its too late for that. Doa limeshakuwa kubwa sana. Kibaya zaidi, doa lenyewe limeshaonekana na Watanzania karibu wote. Kumsafisha sasa hivi hakutaondoa taswira ambayo imeshajengeka miongoni mwa watanzania kwamba Ben na Anna walifuja kodi za watanzania na kujinufaisha binafsi. Suala la Kiwira ni moja tu. Lakini yako mengi yalifoanyika chini ya utawala wake ambao yeye moja kwa moja kama Rais wa nchi anapaswa kuwajibika. Suala la mikataba mibovu ya madini, radar, ndege ya rais, EPA etc yamefanyika kwa baraka zake. Huyu bwana anapaswa kuwajibishwa!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,704
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Wote ni mafisadi tu ambao wanastahili kuchunguzwa, wapandishwe kizimbani na kama kuna mali waliyojipatia kwa njia za haramu basi wafilisiwe. Mama Mkapa hakuwa na ubavu wowote wa kuamua Kiwira iuzwe kwa bei karibu na bure, Mama Mkapa hakuwa na ubavu wa kuamua nyumba za serikali ziuzwe kwa bei ya kutupa na Mama Mkapa hakuwa na ubavu wa kuamua rada inunuliwe pamoja na kuwa Watanzania tulio wengi tulipinga ununuzi wa rada hiyo.

  Halafu bila woga wala aibu anathubutu kusema kumpandisha Mkapa kizimbani kama ataonekana anastahili kujibu tuhuma dhidi yake ni kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa!!!! Kwa maana nyingine mafisadi wakiachiwa kuendelea kupeta basi ni maendeleo kwa Taifa!!!! Na huyu ni professor lakini kauli yake haionyeshi kama anastahili kuwa professor!!!
   
  Last edited: Feb 12, 2009
 5. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Prof Mbilinyi asidhani tumemsahau. Huyu si ndiyo laijiuzuru serikali ya Mkapa kwa kashfa ya rushwa????
  Au ni Mbilinyi mwingine?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,704
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Ndiyo huyo huyo fisadi mwingine anamtetea fisadi mwenziye
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  If it backs like a dog ....
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu hajawahi kusikia vigogo wa nchi nyengine wakepelekwa mahabusu na baadae kupandishwa mahakamani ? Hawa maporofesa wengine waache kujipendekezza ni aibu kwa mtu mzima kumtetea fisadi au huenda na yeye alishauri katika njia za kupita sa ndo anaogopa yasije yakamwangukia ogopa sana watu wanapenda kuteteatetea.
   
Loading...