Prof. Mbarawa: Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya SGR maeneo ya Tanga - Arusha, Mtwara - Mbamba bay

mulisaaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
6,958
6,989
Updates kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa reli tanzania. Standard Gauge Railway (SGR).
sgr.jpg


Amesema; Gati namba 2 zinaendelea kujengwa ili kuboresha bandari hiyo Serikali inaendelea kuboresha miundombinu katika maeneo mbali mbali na kwa ukanda wa Mtwara.

Sio bandari pekee hata kwenye reli tenda za mradi wa SGR kwa Mtwara - Mbamba bay na matawi ya Mchuchuma - Liganga KM 1000, iko kwenye hatua za mwisho ili kuitangaza,kwa hiyo tunaenda spidi kuelekea 2020 tutakuwa mbali.

Serikali inamipango mikubwa kuimarisha miundombinu kwa SGR Tanga - Arusha tenda ya kumtafuta 'Transaction Advisor' imeshatangazwa, kwenye vya ndege pia Serikali itaboresha kwa bandari Tanzania port wanaweza eleza kidogo nini kinafanywa pale kuboresha

Nashukuru changamoto hizi za masuali zinatufanya nasi tukimbie kimbie kutekeleza miradi hii mikubwa, bado tunasisitiza Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu.

Hii ni habari njema kwa SGR Tanzania kwa ujumla!.
 
Ni hatua za kutia moyo sana. Tukikaza mikanda kwa pamoja, tukafanya kazi, tukalipa kodi stahiki na serikali ikapata mapato tutafika mbali sana kabla ya 2025. Kwa sasa kwa kweli serikali inatekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya mawasiliano mingi sana.
 
Hakuna hasiependa maendeleo tutanufaika sana raia wa kawaida na wale wa kati kwa kweli. Rai yangu tu wajitahidi umeme usije ukakwamisha maana linaonekana ni tatizo la kudumu.. laasivyo tutalala giza sana
 
Back
Top Bottom