mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,771
- 7,138
Mh. Waziri muda mrefu abiria tunaopenda kutumia mwendo kasi tunaumia sana, umbali kutoka m2000 mpaka ubungo stand kufuata mwendo kasi mkubwa, kupitia wakala wa barabara badilisha hizi stand, ya ubungo iwe ya daladala na simu 2000 yawe ya mabasi ya mikoani, hapo utakuwa umeondoa usumbufu. Mfano ukitoka Tegeta au kawe kama unawahi mjini ukitumia mabasi ya mwendokasi inaturahiaishia. Hatujui aliyebuni kituo hiki alifikiria nini mpaka tukapata adhabu hii. Leo hii barabara ya kuingia huko simu 2000 haitamamaniki. Abiria tunachelewa makazini tukiangaika na mabasi yanayoruka matuta.