comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mh Prof Jumanne Maghembe amesema kuna maneno yanaendelea mitandaoni na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Tanzania haichukui na kutumia ipasavyo nafasi za safari za watu mashuhuri duniani kutangaza utalii wanapokuja nchini, Prof Maghembe ameongea leo katika viwanja vya maonesho ya kibiashara jijini Tanga wakati akifunga maonesho, Waziri Maghembe ameyasema hayo alipokuwa anaongea na baadhi ya watumishi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA ) katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Mh Prof Maghembe amesema" Msikae kimya wajibuni hao wanaosema watu mashuhuri wakija nchini kutembelea vivutio vyetu hatuwatangazi, ukweli ni kwamba wengi wao hawapendi ujio wao ufahamike mpaka watakapoondoka tuna mfano wa wengi waliotembelea juzi juzi " Prof maghembe aliwataja wageni hao baada ya kuondoka ni David Beckham, Bill na Melinda gates, Willy smith na familia za kadhaa za kifalme, Aidha Prof Maghembe amesema watu mashuhuri waliotembelea karibuni kama Waziri Mkuu mstaafu wa Israel Ehud Barak kwa kuwa wao walikua watu wa seriakali hivyo ndio maana vyombo vya habari vilipewa taarifa na kumtangaza, Vilevile Prof Maghembe amesema watu mashuhuri wasiopenda kujulikana ujio wao nchini kuna utaratibu wao wa jinsi ya kufika nchini wengi wanakuja kwa kufanya ' booking' kwenye makampuni makubwa kwa malipo maalumu kwa masharti mengi ikiwemo ya kutotangazwa safari zao.