Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nitasimamia maendeleo ya kiuchumi nchini

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Screenshot_20201015-163901.png

NJOMBE- WANGING'OMBE
Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itajenga uchumi wa kisasa wenye ushindani wa kitaifa na kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi, unaokuwa kwa kasi bila kuharibu mazingira na ambao utakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Kukua kwa uchumi kunahitaji uongozi imara na utawala makini, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji mzuri wa mikakati na mpango hiyo. Kujenga mazingira mazuri ya kuwekeza, kufanya biashara na ushirikiano wa kimataifa bila kuathiri uhuru wa nchi yetu.

Kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 8 – 10 kila mwaka kwa miaka kumi ijayo na kufanikisha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu mwaka 2030.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom