Prof Lipumba ni Rasilimali ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Lipumba ni Rasilimali ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkigoma, Mar 13, 2012.

 1. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huu ni ukweli usiopingika ukibisha utaonekana una matatizo katika chako, huyu jamaa kweli ni prof wa ukweli mungu amempa akili na uwezo mkubwa, leo kuwa ni mtu mweusi pekee kutoka afrika aliyeshughulikia mtikisiko wa uchumi duniani akiwa ni mwenyekiti wao, akiongea kuhusu tanzania anasema yupo tayari kufanya tafiti juu ya tanzania ila tu wakubaliane kutekeleza utafiti huo na uchumi wa tanzania utapanda haraka na watanzania tutakuwa kwenye neema, ni professor pekee mwenye uchungu wa nchi yake, watanzania wameitupa almasi wazungu wameiokota. tusubiri 2015 labda watanzania wanaweza kuiona almasi.
   
 2. m

  mzee wa mawe Senior Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli huyu jamaa ni genius wa ukweli
   
 3. i

  in and out Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nampa big up lipumba awasaidie hawa manyang".au wa ccm.
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  lipumba yuko kazini huko USA. ameajiriwea na anapewa mshahara! tumbo linakuwashia nini wewe kabwela mwenzangu? hata hizo habari chache unazosikia juu yake, ni kwa kuwa mwajiri wake ana jukwaa kubwa na pana la kusikika dunia nzima. ya ngoswe tumwachie ngoswe!

  kama mngenitemebelea na mimi hapa kazini kwangu hapa TZ na kunifanyia tathmini, huenda na mimi ningemfunika lipumba! kwa nini?

  kwa sababu mimi ndiye "kichwa" cha wizara nzima hapa wizarani kwangu. kwa kuwa UN hawajaanzisha jukwaa la fani yetu, ndio maana watu hawanitambui. siku wakiazisha, baaasi! nitamfunika hata lipumba, dambisa moyo, ali mazrui etc!

  NB:
  nampongeza lipumba kwa alipofikia, lakini bado hajapata tiketi ya kueleweka na kuaminiwa na watanzania!

  mbarikiwe sana

  Glory to God!
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Rasilimali pekee iliyoshindwa uchaguzi mara tatu na alivyo king'ang'anizi 2015 yumo tena. Kule US anapiga deiwaka tu but nyie wenzetu mlioishia ngumbalu mnajua anafanya wandaz. Arudi bongo kufundisha tu deiwaka ikiisha siasa imemshinda
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..akishaingia kwenye system ya CCM basi kwisha habari yake.

  ..Dr.Ndullu naye alikuwa akisifika World Bank, lakini aliporudi Tz ameanza mauza-uza ikiwa ni pamoja na kujenga kasiri la mabilioni kwa ajili ya gavana wa bot.

  ..Daudi Balali was very humble alipokuwa IMF. hata kuitwa doctor alikuwa hataki, lakini alipojiunga na serikali ya CCM akaruhusu wizi wa EPA.
   
 7. j

  jani Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ki ukweli lipumba ni professor wa kuaminika....ingependeza xana kama tungemshirikisha kwene michakato ya kukuza uchumi wetu na inaezekana tungefika mbali....ila ndio hivyo tena siasa zetu.....kwa upande wa kupata uraisi na kuunda serikal....wel.....''no comments''
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red wewe ndio unaonekana una matatizo katika kichwa chako kwa kujaribu kuzuia critical thinking. Staili ya "ndiyo mzee" is definitely not the jamii forums' way. Next time wee mwaga mada jamvini halafu subiri kuona watu wanavyoidadavua.

  Kwenye blue hebu jaza nyama kidogo, alishughulikia vipi mtikisiko wa uchumi duniani na alikuwa mwenyekiti "wao" akina nani? Hebu shusha data zaidi mkuu nasi tunufaike.
   
 9. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwendawazimu si lazima aokote makopo! hata wewe kwa upuuzi huu uliouweka hapa ni uwandazimu tosha.
  Yaani mtu kagombea urais mara 4 tofauti alafu eti unadai yeye ni rasilimali ya Tanzania!!? my foot!
  Nakuhakikishia haitakuja kutokea Lipumba kuwa Rais wa nchi hii....yaani sahau hicho kitu kabisa! Ni rahisi mtoto wa Lipumba siku moja anaweza kuja kuwa Rais lakini si Lipumba mwenyewe....RIP CUF
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Heshima zimuendee prof lipumba!
   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  yaani chama chenye wabunge 2 tu huku bara,alafu unasema 2015 kitachukua nchi? my foot!
   
 12. Josephine

  Josephine Verified User

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa mtizamo wako unaweza kusema hayo,inawezekana pia hujui unazungumza nini,hivyo naomba nikukumbushe tu.

  Miaka ya 1985 wakati wa utawala wa Mhe Rais Mwinyi,Lipumba alikuwa mshahuri wa uchumi wa Rais Ikulu,uliza waliokuwepo nini kilitokea kwa uchumi wetu baada ya kila kitu kuwa ruksa..

  Kwa zaidi ya miaka 10 sasa,tumeshuhudia sera za uchumi za IMF na WORLD Bank zikishindwa kutekelezeka huku Lipumba akiwa Consultant wao..
  wa mda mrefu.

  Sassa tuambie lipi hasa tujivunie leo?
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Dada Josephine heshima yako kwanza, mimi huwa naamini kitu kimoja mfano mimi ni chama cha kijamii lakini wewe Chadema una sifa fulani siwezi kukunyima sifa yako kwa kuwa tunatofautiana itikadi. Naamini Dr W. Slaa anamfahamu vizuri Lipumba na ni mshirika mwenzie katika siasa za Tanzania. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuwapinga wale wote wanaowavunjia heshima viongozi wa kisiasa hata pale Wabe alipokukosea adabu nilimkemea kwani hukustahili maneno ya chuki aliyokuwa akiyaelekeza kwako.

  Lipumba ni kweli alikuwa mshauri wa maswala ya uchumi enzi zile za mzee Mwinyi enzi tulizoanza kuvaa mashati ya "tomato" enzi tulizo anza kununua Television enzi ile ndio enzi tuliovaa suruali za mchelemchele maisha hayakuwa magumu kama sasa watu walimudu kula yao.

  Profesa amewahi kuwa mshauri wa maswala ya uchumi nchini Uganda nadhani umeona na unaona sasa hivi Uganda wapo wapi na shilingi yao ipo vipi.

  Ukimpa mtu sifa yake huwezi kupungukiwa kitu dada yangu Mungu ni mwema anaona yaliyo kwenye vifua vyetu na atuepushe na chuki katika mioyo yetu Amin.
   
 14. j

  joeprince Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  aanze na zanzibar na cuf kwa vitendo tuone miradi
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280

  huo utafiti alishaufanya wakati akiwa mshauri wa mwinyi na ukaproof failure hana lolote akafanyie huko kwenye fellowship zake yeye ni mwalimu na si vinginevyo
   
 16. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Lipumba hana mtoto, sijui unaongelea mtoto gani?
   
 17. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yap! ni kweli prof. lipumba ni genius....but he's not a politician......aachane na siasa hawezi....siasa sio uchumi tu.
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Josephine,

  Mie mara nyingi when it comes to comparison between our president huwa sipendi kulijadili kwa kuwa nawaheshimu ila nimeona nikujibu kwani hujui unalolisema. Kwanza katika marais waliokuwa poor katika kiuchumi Nyerere was a failed president. He was given a country with an immense amount of wealth but left within a brink of bankruptcy kama hujui jiuliza kwanini tulilazimika kukubali ERP 1 and 2 za World Bank and IMF. Economic Reform Policy 1 and 2 Rais Mwinyi alibidi azikubali kwani nchi ilikuwa haina kitu. Kama ungelikuwa na umri kidogo basi ungelikuwa unakumbuka enzi za unga wa dona (rangi ya njano) na foleni za sukari guru miaka 70. Kwakuwa nchi ilikuwa imefilisika data zipo nakushauri ukazisome usiwe unaropoka.

  Rais Mwinyi alipoikuta ile hali na kwa kumuheshimu Nyerere ndipo alipokubali masharti ya nyanja ya uchumi kulegezwa. Leo hii hatuvai tena mashati ya mchele mchele, tunaweza kukosoana na tunakuwa kiuchumi ni matokeo ya policy formula za Rais Mwinyi na Lipumba ndio alikuwa mshauri wake.

  Hivyo nakushauri look carefully around you what you have including these forums is as result of macro economic policy relaxation ambazo ziliasisiwa na Mwinyi na chini ya ushauri wa Lipumba je hilo si la kujivunia? Kama hukumbuki muulize mchumba wako enzi za Nyerere tulikuwa hata kuzungumzia seirkali katika vijiwe vya mtaani tulikuwa tunaogopa leo hii tunaikosoa wazi mbele ya jamii sio mafanikio hayo? Ukuaji wa sekta mbali mbali mfano sekta ya benki sio mafanikio? Kama ulikuwa hujui zamani ulikuwa ukilipwa cheque na serikali inachukua siku 28-14 kulipwa leo hii inachukua siku 4 tu je hayo si mafanikio.

  Kuna mwanafalsafa mmoja alisema kuwa kama huna jambo zuri la kusema dhidi ya mtu ni bora ukae kimya otherwise utajiabisha especially kwa mtu kama wewe unayeheshimiwa na jamii.
   
 19. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tatizo la Tanzania ni uchumi, huwezi ukawa unaumwa kichwa ukaenda kwa fundi seremala akutibu itakuwa ni vichekesho, tatizo la uchumi mfuate mwanauchumi, Dj, mkabidhi vyombo vya muziki, ukitaka kupata neno la mungu nenda kwa Padri, huu ndio utaratibu. sasa leo tunalazimisha Padri awe kiongozi wa nchi tutachekwa.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo anaingia kwenye kundi la madini, zahabu, makaa ya mawe, misitu etc!
  Kazi ipo,mmmmh!
   
Loading...