Prof. Lipumba: Kikwete kujiongezea muda wa urais hadi 2017

Mbona mnatokwa na povu wakuu?! Mtoa habari mwenyewe kasema ni tetesi tu!...tusubiri tuone, wakati ukifika kama ni kweli uwanja utakua wetu kuchangia! Mwarobaini mchungu lakini Dawa, tustahamiliane!
 
apewe muda bado tuna mpenda na kumkubari kama vip hata 2025. chadema na slaa wakae pembeni

Aliyesema hayo ni Lipumba, Dr Slaa na Chadema wakae pembeni vp, nyie CCM vp kila kitu chadema......JK aondoke hata kesho kama unampenda sana mchukue nyumbani kwako.
 
hebu tujikumbushe shughuli za chama na serikali

wanataka kuendeleza haya,mwee hata mie ctaogopa kujitoa kuokoa taifa hli hata kama nitaishia kwe risasi za policcm
 
Kwa mujibu wa Prof Ibrahim Lipumba kupitia kituo cha ITV, anasema kuna habari kazipata kuwa mawaziri wanapanga kupeleka hoja bungeni ili Kikwete aongezewe muda hadi 2017!! Sababu ni kuwa asimamie zoezi zima la katiba mpya kupatikana! Lipumba kamwonya asithubutu, maalim Seif Sharrif Hamad alikuwa pembeni. Si bure hapa kuna kitu. Una maoni yapi mwana JF?

Mzee dhaifu hata kuwa mrafi kuongeza miaka yake miwili,kulngana na katiba huyo jamaa ataona aibu na ataiacha tz.
 
Written by Mwandishi wetu
Dar es Salaam,Tanzania

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi inadaiwa
kuandaa mazingira ya kumwongezea
Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Rais Jakaya
Mrisho Kikwete muda wa kuongoza nchini.
Taarifa za kuwepo kwa maandalizi hayo
yalifichuliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha
Wananchi (CUF) Profesa Haruna Ibrahim
Lipumba ambaye alisema kwamba Serikali
inajiandaa kupeleka hoja hiyo Bungeni ili
wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi Bungeni
waipitishe kwa kauli moja.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha
Baraza jijini Dar es Salaam Profesa Ibrahimu
Lipumba alidai kuwa amenasa taarifa za siri za
kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa
Serikali ili iendelee kudumu kukaa madarakani.
Profesa Lipumba alisema hatua hiyo ya Serikali
inakuja baada ya wasiwasi wa mchakato wa
Katiba Mpya kutokamilika mwaka 2014 kama
ilivyokuwa imepangwa awali na kufanya
uchaguzi mwaka 2015 kushindika chini ya
Katiba Mpya kama ilivyopangwa.
Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka
kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa
miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya
Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete
itakaa madarakani hadi mwaka 2017 itakapo
kamilisha mchakato wa katiba hiyo..
 
jamani hii taarifa si ya kweli lipumba hakusema kuwa rais ana nia ya kufanya hivi,nimemsikia mimi mwenyewe akisema kuwa rais hajawahi kutamka maneno haya bali alisema kuwa ni tetesi tu anazisikia hivyo si vema kumshambulia kikwete kwa kitu asichokisema
 
jamani hii taarifa si ya kweli lipumba hakusema kuwa rais ana nia ya kufanya hivi,nimemsikia mimi mwenyewe akisema kuwa rais hajawahi kutamka maneno haya bali alisema kuwa ni tetesi tu anazisikia hivyo si vema kumshambulia kikwete kwa kitu asichokisema

ujanja huo mkuu! Pevuka dogo, ndo mbinu za wanasiasa. Kashasoma upepo yule dogo wake Riz1 mwenye dili zake mgodi wa Buzwagi kule Kahama kitamnukia
 
Kama kuikubali ili kuwa kimbembe, leo aongezewe muda ili iweje? ...lakini ni sawa, aongezewe ili tupate sababu ya kulianzisha, ajue namna gani tumemchoka,
 
apewe muda bado tuna mpenda na kumkubari kama vip hata 2025. chadema na slaa wakae pembeni
Aje kwenye familia yako akuongoze wewe kwa miaka hiyo miwili na sio Tanzania,hata aliokaa ni mingi sana,kama watanzania tungekuwa na umoja angekuwa ameshakimbia ikulu
 
Inawezekana ni kweli kwani Lipumba kazipata hizo habari kutoka kwa Maalim Seif,CUF wana ndoa na Magamba.
 
Back
Top Bottom