Prof Lipumba azidi kumshambulia Mengi

Kweli RA payroll yake ni kubwa mpaka Lipumba....!


Hivi macho yangu yameona hii kitu sawasawa kweli naomba mnifumbue macho kama kweli hata Proffesor yupo kwenye payrol ya RA Mhh makubwa may be....!!!
Lakini si ajabu Maprofesa wetu kuwa namna hii labda ni mfumo wetu wa kimaisha kwa sababu nchi nyingine Maprofesa ni watu wanaotunza sana heshima zao lakini hapa home baadhi yao wengi wanaiaibisha taaluma yao.
 
Nimeamini watu iwa hamsomi habari yote mnaishia kutoa hukumu.
Lipumba kamwomba JK awashughulikie wote wawili nyie mmelala upende mmoja someni tena habari hiyo hapo juu,mnao hukumu bila kusoma yaliyomo ndo vilaza.
 
Jamani wakuu, hata mie Lipumba huwa ananitia mashaka sana na upeo wake katika mambo mengi. unajua wenzetu hawa "Profs" wakisaha pata hizo tittle zao wanajiona kama wanajua kila kitu duniani! kumbe yeye kabobea kwenye KA-area kake tu.
Pia anatabia ya kujibu vitu nje ya maada.
 
Nimeamini watu iwa hamsomi habari yote mnaishia kutoa hukumu.
Lipumba kamwomba JK awashughulikie wote wawili nyie mmelala upende mmoja someni tena habari hiyo hapo juu,mnao hukumu bila kusoma yaliyomo ndo vilaza.
mbona hakumtaja na slaa ashughulikiwe? kwa kuwa naye aliwataja tena kwa mapana na kina kama alivyowataja Mengi.
mkuu nomba ku-differ hapo
 
Prof. Lipumba angerudi tu UDSM! Maana tangu aanze kugombea Urais kura zake zinashuka kila kipindi. Kwa kuropoka kwake this time, nadhani mwaka 2010 ataambulia kura yake tu pengine na ya familia yake kama anayo!
 
Nimeamini watu iwa hamsomi habari yote mnaishia kutoa hukumu.
Lipumba kamwomba JK awashughulikie wote wawili nyie mmelala upende mmoja someni tena habari hiyo hapo juu,mnao hukumu bila kusoma yaliyomo ndo vilaza.

Hata kama kamwomba JK awashughulikie,ni uzushi tu...JK msanii hawezi kuwafanya lolote... na pia tujiulize why now?! mbona alipowataja slaa hakuna alichosema?
 
Too political, I am starting to believe that this is inside job!! Cha dhahiri ni kwamba wote ni mafisadi na wanajaribu kujikosha kwa umma.
 
kela72 said:
Hivi prof Lip alioa? nasikia alikuwa hataki kabisa?

kela72,

..mara ya mwisho nilisikia Prof ameoa mwanamke toka lile kabila linalochukiwa kabisa hapa jamii forums.

..pia mwanamke huyo ni alikuwa muumini wa dini inayochukiwa na chama cha CUF.
 
Huyu Lipumba naye yumo mifukoni mwa mapapa mafisadi akitafuna mapesa yao taratibu. Ama kweli viongozi wetu wa nchi yetu ni mandumila kuwili wa hali ya juu na pia ni viongozi uchwara.
 
Kwani alichosema Lipumba kina ubaya gani? Sijaona ubaya wowote na hoja anazotoa ni nzito.

Alichouliza kinapaswa kuulizwa na mtu yoyote yule. Toka nchi yetu ianze, umeshasikia malumbano ya wafanyabiashara kwa manufaa ya taifa :confused:

OK, tuachane na Tanzania. Je kuna nchi gani wafanyabiashara wanaingia kwa manufaa ya taifa :confused: Au ndio mwanzo wa Warlords :confused:

Kaka tatizo no vita kati ya Chadema na CUF na nani ni Political giant! Mengi au Lipumba?. Kaazi ipo hapa. Wanataka kumtia maneno mdomoni ili kukidhi haja za kisisiasa. Ama kweli Chadema kazi ipo. Endeleeni Kudema dema tu..mtafika.

Prof alichozungumza kawalaumu woote RA na RM... tatizo CHADEMA hawataki mfadhili wa Helicopter akaguswa wao ni kusifia tuuuuu.

Kazi ipo.
 
Kosa la Lipumba ni lipi ? kuweni wa wazi na msionekane wenye kubabaika au kuogopa ,ila ikiwa mnafaidika na mmoja wa mafisadi hapo itakuwa sina haja ya kuona sababu.
 
hivi huyu lipumba anatafuta nini kwa watanzanianau kwa sababu yupo kwenye payroll ya RA anataka kutufanya tusahau vita ya ufisadi
 
Nimeamini watu iwa hamsomi habari yote mnaishia kutoa hukumu.
Lipumba kamwomba JK awashughulikie wote wawili nyie mmelala upende mmoja someni tena habari hiyo hapo juu,mnao hukumu bila kusoma yaliyomo ndo vilaza.

wewe ndio hauchambui mada vizuri, lazima ujue lipumba alisema nini mara ya kwanza juu ya mengi

RA, manji na wenzake wanamatatizo siku nyingi mbona huyo Lipumba hajawahi kumuhimiza JK awachukulie hatua, DR Slaa amekuwa akilia peke yake utasema yeye ndio yuko kwenye chama cha upinzani peke yake

Lipumba amesema huo ugomvi hauna tija kwa taifa, alafu baadae akasema RA amesema mambo ya maana juu ya NBC kuhusu mengi. Mengi alivoongea juu RA, manji et al LIPUMBA AKAMWAMBIA MENGI ANASABABISHA UBAGUZI NA ANAJIPENDEKEZA KWA RAIS WALA AKUMWOMBA RAIS AYASHUHULIKIE YALE ALIYOSEMA MENGI, LAKINI RA ALIVYOONGEA YA MIKOPO YEYE AMEYAONA YA MAANA, JE KWA NINI?????????
LIPUMBA NI KAMA VILE SOFIA SIMBA ALIVYOMUAMBIA MENGI KACHEMSHA NA RA ALIVYOONGEA AMEKUA BUBU, "BUBU AMBAYE ATAKI KUSEMA" ANGALAU WA JF ANASEMA
 
kela72,

..mara ya mwisho nilisikia prof ameoa mwanamke toka lile kabila linalochukiwa kabisa hapa jamii forums.

..pia mwanamke huyo ni alikuwa muumini wa dini inayochukiwa na chama cha cuf.

m_h_g_ ????

jOKA KUU Kwani kabila la mke wa lipumba lina matatizo gani mpaka lina chukiwa jf??
 
semilong said:
jOKA KUU Kwani kabila la mke wa lipumba lina matatizo gani mpaka lina chukiwa jf??

semilong,

..kwa mtizamo wangu, watu wa kabila hilo hufanya kazi kwa bidii sana. sasa wanapopata "ka-ahueni" ka namna yoyote ile wale wa makabila mengine wanaanza chuki zisizo na msingi.
 
Ndio Lipumba yupo kwenye mstari na anaposema aliyosema Rostam ni mazito ,hivi tatizo lipo wapi ? wewe unaejua kuwa Mengi yupo katika haki ni wewe tu .ila waTz walio wengi wanamuona Mengi kuwa ni mwizi aliekubuhu au jambazi sugu ,sasa alichofanya Lipumba ni sawa na kumwambia Mengi jisafishe ? Na tumeona ametokeza kwa mara ya pili kukanusha kwa vielelezo huku ni kujisafisha , Inaionyesha mna matatizo ya kufahamu Lecture jamani kwenye vyuo vikuu hakuandikwi ubaoni ,yaani mnaonekana kama mnaazima magazeti na kusoma tu na halafu mnakurupukia hapa JF.

Kumfahamu Lipumba kunataka mtu msomi ambae amezoea kusikiliza Lecture na kuondoka na kina cha yaliyozungumzwa ,kuna watu wanapata tabu sana wafikapo vyuo vikuu vya nchi za ughaibuni ,jamani wanaotoa lecture huko ni maprofesor ambao humwambii kukamata chaki akaujazia notice kwenye ubao ,just anaingia na kukufahamisha mawili matatu ,na saa ingine anawapa kurasa za kitabu mkasome siku ya pili akiingia anauliza kama kuna mtu hajafahamu ,na akitokea anakwambia mfuate ofisini na wiki ijayo mtihani.
Lipumba ni mmoja ya mtu ambae inataka umfahamu kwa kina na kama una muda uyaangalie mazungumzo yake mstari kwa mstari ,ila kama ni wasomaji mnaokimbilia na kufukuzana na njaa mtapata tabu sana.
 
hivi huyu lipumba anatafuta nini kwa watanzanianau kwa sababu yupo kwenye payroll ya RA anataka kutufanya tusahau vita ya ufisadi

Kwa kweli kwenye hiyo payroll wapo wengi....na hapo bado mzee wa Dowans hajaingia bado, kazi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom