Prof Lipumba azidi kumshambulia Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Lipumba azidi kumshambulia Mengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Semilong, May 5, 2009.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kutoka mwananchi

  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema malumbano ya wafanyabiashara yanayoendelea kushika kasi nchini kuhusiana na ufisadi, hayana tija kwa taifa badala yake yanalitoa katika harakati zake ya kukabiliana na changamoto za maendeleo.

  Profesa Lipumba alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusiana na kauli ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz aliyemtuhumu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ni ‘nyangumi wa ufisadi'.

  Alisema malumbano hayo yanawafanya Watanzania wengi kuacha kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo na kubaki kwenye fitina zinazosambazwa na wafanyabiashara hao.

  Aliitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukomesha tabia ya wafanyabiashara kukamiana kupitia vyombo vya habari, kwa lengo la kuwashirikisha wananchi kwenye chuki zao ambazo zinaotesha mbegu za rangi na ukabila, hivyo kutishia amani ya nchi.

  "Tanzania ni nchi maskini ingawa tuna rasilimali nyingi. Tumekuwa na tatizo kubwa la kushindwa kujipanga vizuri katika kuzitumia. Kwa jinsi suala hili la ufisadi linavyokwenda, linazidi kutuvuruga," alisema Lipumba na kufafanua: "Mijadala (malumbano) hii inazidi kututoa kwenye mstari."

  Hata hivyo, alisema katika maelezo ya Rostam, ambaye pia ni Mbunge wa Igunga, kuna hoja nzito alizozitoa na ambazo zimewafumbua macho Watanzania, hivyo Rais Kikwete hana budi kuzishughulikia kikamilifu.

  Alitaja miongoni mambo hayo kuwa ni tuhuma kuwa Mengi alikopa mabilioni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kabla haijabinafsishwa na hakurejesha na vile vile alichukua mabilioni mengine kwenye mfuko unaochangiwa na wahisani; Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (CIS) ambazo pia hakuzirudisha serikalini kama ilivyo utaratibu wa mfuko huo.

  Aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuutangazia umma wote waliokopa NBC na CIS na kuwaamuru walipe na kwamba, wachukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa mafisadi wengine waliochota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Profesa Lipumba, alisema kama nyaraka zinazohusu fedha za CIS zitakosekana Hazina, serikali iwasiliane na nchi wahisani wa mfuko huo, kwa sababu wana kumbukumbu za kampuni zote zilizokopa.

  Alimtaka Rais Kikwete kuonyesha dhahiri nia yake ya kupambana na ufisadi kwa kutowaonea huruma wafanyabiashara wote wawili ambao kila mmoja anaonekana yuko karibu naye (rais).

  Profesa Lipumba alisema anamtambua Rostam kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mengi ni mwanachama wa CCM ambaye amekuwa akijinadi kuwa anamsaidia Rais Kikwete kwenye vita dhidi ya mafisadi; hivyo akasisitiza wote wako karibu na Rais Kikwete.

  Alisema fedha za Mfuko wa CIS hutolewa na wahisani ili kuwasaidia wafanyabiashara kuagiza bidhaa nje na hutakiwa kurejeshwa serikalini kwa shughuli nyingine za maendeleo, hivyo kama hazikurudishwa, huo utakuwa ni wizi wa mali ya Watanzania.

  Kuhusu EPA, Profesa Lipumba aliendelea kusisitiza kuwa ripoti ya awali ya ukaguzi ilionyesha kampuni ya Kagoda ilighushi nyaraka ili kuzichota hizo fedha, hivyo haoni sababu ya serikali kutowapeleka mahakamani wahusika au wamiliki wake ambao mpaka sasa wanafichwa.  lipumba unataka kikwete amshughulikie mengi je marafiki zako RA, manji(nssf). tanil, jetu et al vipi.

  Mengi ameshamaliza hizo kesi zote mahakamani!

  Kweli RA payroll yake ni kubwa mpaka Lipumba....!
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimesoma post huku nimebana pumzi, siamini Lipumba kama anakuja na mashambulizi namna hii dhidi ya mtu aliyejitoa mhanga kuwataja mafilisi wa nchi hii!

  Sasa naanza kuamini kuwa Lipumba si tu kwamba yupo ktk payroll ya mafilisi bali pia zile kelele zake alizokuwa anapiga dhidi ya mafisadi ni kwamba alijua hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yao na alikuwa tu anatimiza wajibu ili kupata reputation ya kisiasa. Wanasiasa bwana ni kama upepo vile.

  Anyway sasa naamini kuwa CUF si chama makini kama alivyosema Prof. Safari na wanajua wanachokifanya, they just stir in order to survive and who knows, may be wanasiasa wa kulipwa.
   
 3. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Msiumize vichwa sana, kama alivyofanya nyakati za DOWANS ndivyo anavyofanya nyakati hizi.

  Inabidi hawa wanasiasa uchwara na wapenda hela bila kuangalia maslahi ya taifa wawe wanaangalia timing. Si kila jambo kubwa utie domo ili kutafuta umaarufu, tumeni makanjanja wenu waboronge tutaacha lakini kwa mwendo huu nazidi kumwona Lipumba kilaza tu, anajaribu kutafuta jinsi ya kusikika upya.

  Nonesense!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #4
  May 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lipumba is the fake politician< kibaraka > wa ufisadi. Labda baada ya kuona nyaraka za mengi anaweza kuongea lingine.
   
 5. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa nimetambua kwamba Prof. Lipumba ambaye ni mwalimu wangu chuo kikuu amekuwa mwanasiasa kweli kweli! Nimjuavyo huyu bwana ni mtu mwerevu na makini but I wonder what he has been eating lately! Kwa nini asirudi UDSM?

  Hivi Prof. Lipumba anatambua kwamba pamoja na kuongoza chama kikubwa kama CUF chama hiki hakina kiti hata kimoja bugeni Tanzania Bara? Hivi anatambua kwamba ushindi wa CCM wa kishindo 2005 ulitokana na ufisadi na pesa za ufisadi wa kuvuruga uchaguzi zilipitia mikononi mwa hawa hawa watuhumiwa "papa"? Hivi haoni kelele za Mengi hatimaye zitamsaidia yeye uchaguzi 2010 kwa vile serikali itabidi ifikirie mara mbili mbili kabla haijarudia Mchezo mchafu kama 2005. Hivi Prof. Lipumba yuko makini na anataka CUF inyakue madaraka 2010? Kwa mtindo huu ndio maana CUFwalidanganywa "toto" katika kuigia mazungumzo ya muafaka na CCM. Kiko wapi? Wengi wetu tulijua kwamba mazungumzo haya ilikuwa ni kupoteza muda na sijui watu kama yeye akuliona hili. With leaders like him who needs perpetual opposition leaders? Muacheni Mengi! Afterall the man is foresighted and no wonder he is a multi millonaire.
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ktk Mwananchi ya Leo kuna taarifa Mbili...sometimes ni vema kuepuka kaka/dada zetu ambao hukopy news na kuweka Bold maeneo wanayoyapenda...tunachowaomba muweke link ili mtu binafsi aweze kusoma aamue mwenyewe.Unaposema mwananchi bila kuweka link inawapa tabu watafiti kuanza kusearch date ya andiko lako.

  Lipumba kawalaumu wote wawili na ndio kichwa cha mwananchi ya Leo.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=11730

  Habari ingine ni juu ya Hii vita namna CUF na Chadema wanavyogonganishwa au kujigonganisha au kutoa maoni yao..

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=11727
  Ktk Hili Msimamo wa Lipumba ni huu...ukisoma hio habari chini kabisa..
  "Profesa Lipumba aliliambia Mwananchi Ofisini kwake Buguruni jijini hapa kuwa, hajabadilisha wala kuusaliti misimamo kuhusu vita dhidi ya ufisadi nchini, lakini vita hiyo lazima ilenge katika kungÂ’oa mzizi ambao mfumo mbovu wa serikali."
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Lipumba ni mojawapo wa mzizi wa kifisadi na nibudi ung'olewe mapema pia.
   
 8. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kweli tupu unachozungumza kuhusu huyu Professor.Sina doubt credentials zake,huyu bwana alisikika sana pale mlimani kwa kupendelea mfumo huria wa uchumi akishirikiana na Professor Benno Ndullu.Ni mtu mahili kuelea mada za uchumi na uwezo mkubwa kuzisimamia.Bahati mbaya kwenye siasa namuona yuko tofauti kabisa naona zaidi anazidi kujimaliza mbele ya watu walio wengi mabao wamechoka utawala mbaya wa CCM.Huyu Prof asione aibu kumconsult Maalim Seif ambaye ana ouzoefu kwenye uwanja wa siasa.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Lipumba si Mnyamwezi? Chuma usimtetee. Hajaanza leo wala jana.

  Alikuwa mshauri wa Mwinyi wa Uchumi. Matokeo yake mnayakumbuka.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tuta watambuaje... matendo.. jamani matendo.. tuta watambua. kama ni wapinga fisadi ama wakumbatia fisadi.

  Lipumba mwe!
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hizi ni habari za kutungwa washkaji! Au wamemnukuu vibaya?
  HAIWEZEKANI!

  Ameanza kwa kusema haya ni malumbano yasiyo na TIJA. Halafu baadae inakuwaje tena aone kuja hoja NZITO?

  HAIWEKANI wandugu....
  Hizi sio habari za kweli....
  Maana.....
  No-no-no! This can't be!

   
 12. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Lipumba sio MNYAMWEZI, ni MTUSI...
   
 13. T

  Thobius New Member

  #13
  May 5, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lipumba prof mzima umekuwa mtu wa kukurupuka na kushutumu mzalendo mwenye uchungu. Mitaani mpaka wameamua kukuita ''Lipumba wa pumba". Acha izo bwana unaaibisha chama.
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unafahamu watusi wewe? hebu ona sura na Mpua, na ongeza na unene hapo hapo. Mtusi gani ana pua kama donge la Sabuni? Huyo lazima awe mbantu. Pia dini ya Uislam na jina la LIPUMBA, labda angelikuwa RIPUMBA ningeliamini unayosema.

  Nina rafiki yangu anatoka kijiji hicho na pia kwenye mikutano ya Wanyamwezi wa basi pia huwekwa meza moja na Kapuya (Kwa shingo upande).
   
 15. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Prof Lipumba is not serious!!! Anahisi nayeye yatamkuta, si mnajua uchumi ulivyokuwa wa hovyo enzi za mzee mwinyi na yeye alikuwa mshauri wake wa uchumi???!!! Si ajabu ktk lile alilosema Inv. kuna data za kuanzia '90s huyu jamaa akawemo. Lets wait and see...
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  haste haste mkuu
  hehehe.
  nadhani tumkogeshe kwanza (mzizi wa kifisadi) kisha akishatakata ndipo wenye kumbagua waendeleze libeneke.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Prof Lipumba, Prof Kapuya hawa wote wanatokea Tabora...kuna shida na gani na maprof wenu!?
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  connecting the dot.. na Prof RA wa ufisadi nae anatokea tabora
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwani alichosema Lipumba kina ubaya gani? Sijaona ubaya wowote na hoja anazotoa ni nzito.

  Alichouliza kinapaswa kuulizwa na mtu yoyote yule. Toka nchi yetu ianze, umeshasikia malumbano ya wafanyabiashara kwa manufaa ya taifa :confused:

  OK, tuachane na Tanzania. Je kuna nchi gani wafanyabiashara wanaingia kwa manufaa ya taifa :confused: Au ndio mwanzo wa Warlords :confused:
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  My friend, allow me to say that Hii habari imekaa kisanii....

  Lakini pamoja na hayo, nothing surprising comes out of politicians--; Mwanasiasa aweza kufanya chochote kile kupata umaarufu na cheo, na kama walivyo "social/community prostitutes" the only thing matters to them is "elevated profile"!!!!

  But wait!!! Lipumba kwa sasa ni insignificant and chochote anachosema hakina uzito kama miaka saba nyuma, he needs to revisit his objectives in this world

  HEBU TUSIKIE LABDA HADI AKINA MIGIRO NAO WATAONGEA SIKU MOJA
   
Loading...