Prof. Lipumba awasilisha bajeti mbadala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba awasilisha bajeti mbadala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.


  Chama cha Wananchi (CUF) kimesema serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ni wavivu wa kufikiri, hali ambayo kila mwaka inawafanya washindwe kupata vyanzo vingine vya mapato.

  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema serikali imeg'ang'ania kuongeza kodi katika sigara, pombe, mvinyo, na ushuru wa magari.

  Jana Lipumba aliainisha vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo alisema kama serikali ingeviwekea kipaumbele vingeweza kuwakwamua wananchi kutoka katika umaskini.

  Kadhalika, alisema mapato ya ndani ya serikali yaliyotangazwa kukusanywa kwenye bajeti ya mwaka huu 20010/2011 yanayofikia trilioni sita hayawezi kufikiwa.

  Lipumba alisema kama wao wangepewa fursa ya kuandaa bajeti wangejikita katika kukusanya mapato kutoka sekta ya madini.

  Sekta nyingine ambazo alisema zinatoa mapato mengi ni magogo yanayouzwa nje ya nchi na kuondoa misamaha ya kodi mbalimbali ikiwemo ya wafanyakazi wa serikali kutolipa ushuru wanapoagiza magari.

  Eneo lingine ni kudhibiti matumizi mabovu ya fedha za serikali ambapo alisema asilimia 30 ya fedha hizo zinaliwa na watu wachache.

  Alisema makampuni ya madini amekuwa yakisingizia kuwa hayapati faida wakati katika soko la dunia bidhaa hiyo inaonekana kupanda bei kila kukicha.

  Upande wa magogo yanayouzwa China, alisema wao wana takwimu sahihi na wanajua wananunua kiasi gani kuliko serikali ya Tanzania ambayo inawauzia hatua ambayo alisema ni hatari.

  Alitoa mfano kuwa takwimu inazojua serikali ya Tanzania ni ndogo mara 10 ya zile wanazojua China.

  Alisema serikali kuendelea kuongeza kodi katika sigara na vinywaji mbalimbali hakuwezi kuongeza mapato ambayo yatatumika kulikwamua taifa kiuchumi pamoja na kuondoa umaskini wa kipato kwa Watanzania.

  Kuhusu kilimo, alisema bado serikali haijatenga bajeti ya kutosha na hivyo inaonyesha wakulima wataendelea kuteseka kwa muda mrefu.

  Alitoa mfano kuwa nchi za Afrika zilikubaliana kuwa bajeti ya kilimo ifikie asilimia 10, lakini Tanzania imetenga asilimia 7.8 tu.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yaani ingekuwa watanzania wanachagua ubora na si bora tu...huyu jamaa anafaa kupewa ikulu ndani ya siku 100 Tanzania inakuwa nchi ya asali na maziwa...tatizo Mitanzania mishabiki tu na kelelee nyiiiiiiiiiiiiiiiiiingi hawajuwi kuchaguwa kati ya makapi na mpunga wamo wamo tu...nimeshangaa mpaka wanaitwa wasomi wa chuo Dodoma sijuwi uko...wamemchangia Kikwete fedha za upuuzi gani sujuwi...wakati wao kila siku wanaandama na kugoma wakigombana na serikali hiyo hiyo inawapa mikopo kiduchu...huku wanataka serikali hiyo hiyo indelee kuwapo na kuwahangaisha na vijimikopo kiduchu....Mitanzania bana...!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Junius,
  Mkuu tatizo sio ukusanyaji fedha ila zinatumika vipi?.. tutauza magogo China kwa bei yoyote ile lakini hizo fedha hazitafika serikalini., Anachofahamu Lipumba ni bei inayoandikwa serikalini lakini hajui kwamba ile mara 9 asiyojua inakwenda wapi inakwenda mifukoni mwa watu..Hii ndio Bongo mkuu wangu..

  katika Matumizi ya serikali, Tender itaonyesha millioni 10 supplier hupewa 5 na 5 za kiongozi,Katika mapato itaonyesha millioni 10 lakini ziolizokusanywa haswa ni millioni 20. kila kitu is almost 100% faida tupu yaye anajua asilimia 30 tu..

  Magari yanaingia nchini pasipo kodi ni kwa sababu hii ndio biashara yao..isiyokuwa na liseni wala ushahidi. Mkulu akijingiza Range Vogue la wizi akaliuza anaingiza kitu over Usd 40,000 za haraka kwa kibali cha msamaha wa kodi tu na gari litasajiriwa kwa jina la hata mnunuzi wa ndani na kwa gharama kidogo sana..

  Misamaha ndio imejenga majumba yooote unayoyaona kwenye mitandano yakiuzwa na ndio ya viongozi wenyewe kwa hiyo anachosema Lipumba sio elimu ila ni yeye kutofahamu kwamba CCM wanayafanya haya kwa makusudi kabisa na sii kwamba hawafahamu vyanzo vya fedha..Kumbukeni tu kwamba kila Kiongozi wa serikali yetu is a businessman/woman...wao wanajiita Wajasiriamali - na sii dhambi misahafu inaruhusu..

  Na siku zote as a businessman/woman ni lazima utafute kuegemea kama wanavyotufanya haoyo mashirika ya madini.. Hivi kweli Lipumba alitegemea mashirika ya mafuta yapewe msamaha lakini viongozi wajisahau wenyewe (wafanya biashara)...tulowakabidhi madaraka ya kutunga sheria against themselves (Mbunge ndiye Waziri).
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Naona proffesa anawapigia mbuzi gita.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Mkandara,
  Ni kweli kabisa unayosema hujaenda mbali sana na Prof. Lipumba, ndiyo maana nikasema hawa jamaa inafaa waondoke tu, tatizo wananchi hawapo tayari chama kipo ndani ya damu yao, hawajali njaa zao na shida, wao bendera na shina la chama vinawatosha, hawajali zahanati, shule bora kwa watoto wao wala vipi. Ndiyo nasikitika Watanzania wanajitakia wenyewe kuwa masikini.

  Mkuu, Republican wameondoka madarakani baada ya miaka kumi tu ya utawala wa Bush, na sikuwa hawajajenga bara bara, madaraja na vyuo vikuu...la hasha, watu wanataka mabadiliko tu na mitazamo mipya ya kimaendeleo. Imagine hawa ni watu wenye maendeleo makubwa kabisa, how come sisi tunakaa na chama miaka zaidi ya 40 plus na matatizo yote uliyoyasema mkuu, wananchi wapo taabani....bado chama hicho hicho kina guarantee ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao....Mkuu mi hapa naganda nashindwa kushangaa.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli mnafikiria hakuna mtu ndani ya CCM anayeweza kuyaona haya aliyoyasema Lipumba? Tatizo ni kuwa wakifanya anayopendekeza Lipumba wao watakula wapi?
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yap spot on mzee
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu ndio maana nikasema Itikadi haiwezi kusaidia kitu kwani hawa CCM wanaamini kabisa kwamba wanayoyafanya ni mabaya na kinyume cha Utawala bora.

  Sawa na Muumini wa dini aliyeamua kuwa shoga...Hivyo ni chaguo lako kumpa wanao kuwalea ukitegemea watakuwa straight au atawafundisha dini na kulaani ushoga! Hakika makosa ni yetu sisi sio ya JK wala CCM kwani wao tayari wamekwisha uhalalisha Ushoga.

  Na bahati mbaya Tanzania nzima sasa hivi mwendo ni Ufisadi, Hiyo corruption imefika matawini ktk serikali za mitaa na hakuna njia nyingine isipokuwa kubadilisha Utawala. Hizi juhudi zooote za vyama vya Upinzani kugombea viti vya Bunge nina hakika ni juhudi za kutafuta Ulaji wao, hakuna true patroit anayeweza kugombea Ubunge ktk Utawala mbaya - for he become part of it!
   
 9. C

  Calipso JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [QUOTE=Mzee Mwanakijiji;952323]Hivi kweli mnafikiria hakuna mtu ndani ya CCM anayeweza kuyaona haya aliyoyasema Lipumba? Tatizo ni kuwa wakifanya anayopendekeza Lipumba wao watakula wapi?[/QUOTE]

  Jaribu kuunganisha vyama vya upinzani ili viwe na dhamira moja tu ya kuing'oa ccm madarakani,tumechoka na hawa mafisadi.. ukimtegemea Mwakiembe kwa hilo,utamkuta ana jengine,si huyu mwakiembe ndie alokuwemo kwenye ile kamati ya muafaka wa kwanza wa znz,waznz wanauchungu nae huyu,tunakumbuka maneno yake machafu. ukimwangalia sitta, duh! nakumbuka kuna wakati tuliona kwenye magazeti wenye wake zao wabunge walikua na utata na wake zao kwenda bungeni.. la yaani CCMijambazi
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuunganisha vyama vya upinzani ili viwe na dhamira moja tu ya kuing'oa ccm madarakani,tumechoka na hawa mafisadi.. ukimtegemea Mwakiembe kwa hilo,utamkuta ana jengine,si huyu mwakiembe ndie alokuwemo kwenye ile kamati ya muafaka wa kwanza wa znz,waznz wanauchungu nae huyu,tunakumbuka maneno yake machafu. ukimwangalia sitta, duh! nakumbuka kuna wakati tuliona kwenye magazeti wenye wake zao wabunge walikua na utata na wake zao kwenda bungeni.. la yaani CCMijambazi[/QUOTE]

  Hilo wazo lako lipo Akilini Mwangu nashangaa hapo kwetu bongo kuwa na vyama vingi vya Upinzani, wakati wa uchaguzi ukifika CCM inavishinda vyama vyote vya Upinzani kwa kupata kura nyingi. Kma vyama vya Upinzani havita ungana kuwa chama kimoja basi kila baada ya miaka 5 tusubiri CCm kuwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu. Hatujifunzi Nchi kubwa kam amerika kuna vyama vikuu 2 Vikubwa katika Nchi yenye majimbo zaidi 50 na kuna upinzani wa kimaendeleo mkubwa tofauti na nchi yetu yenye vyama vingi kisha hakuna Maendeleo yoyote. kula kukicha kulaumu kiongozi fulani amefanya hiv,i kiongozi fulani ameharibu hichi nashauri vyama vya Upinzani kuwa kitu kimoja kukiondowa CCM Madarakani asante.
   
Loading...