Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,269
- 25,310
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ametoa ya moyoni kufuatia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kushindwa katika uchaguzi wa Umeya wa Kinondoni.
Akizungumzia uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumapili ambapo Diwani wa CCM Benjamini Sitta alishinda, Prof Lipumba alisema CHADEMA wameshindwa kupata kiti hicho unatokana na ubinafsi mkubwa.
Alisema tokea awali alishauri mgombea wa umeya angetokana na chama cha CUF na sio CHADEMA.
“Kama sio ubinafsi na umangimeza wa rafiki zangu CHADEMA, upinzani tungeshinda hicho kiti” Lipumba.
Prof. Lipumba aliongeza kuwa kuwa CUF ndio chama pekee kinachokubalika kwa Kinondoni ndio maana hata mbunge wake ni wa CUF.
“Sasa hawa ndugu zangu wameleta ubinafsi mkubwa mpaka wameshindwa.”Alisisitiza Prof.Lipumba.
Chanzo: Hivi Sasa