Prof. Lipumba atoa maelezo ya CAG kuhusu CUF chama cha wananchi

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Tarehe 26 March 2020, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere aliwasilisha ripoti ya ukaguzi wake ya 2018/19 kwa Rais John Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dodoma.Pamoja na Mambo mengine CAG Charles Kichere alisema:

"Mheshimiwa Rais, nilibaini Chama cha Wananchi CUF kilipokea ruzuku toka Serikalini ya Kiasi cha Shilingi milioni 369.38 Lakini Chama hicho kilihamisha kiasi cha shilingi milioni 300 kutoka akaunti ya Chama kwenda akaunti binafsi ya mwanachama na kiasi cha shilingi milioni 69 kilitolewa kama fedha taslimu.

Hata hivyo nyaraka za matumizi ya fedha hizo hazikuwasilishwa kwangu kwa ajili ya ukaguzi."

Kauli hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeleta mtafaruku na sintofahamu kubwa kuhusu usimamizi wa fedha za Chama cha CUF.Ni vema tukaweka sawa kumbukumbu zetu kwamba tukio hili lilitokea Januari 2017. Wakati huo Chama chetu kilikuwa katika mgogoro wa uongozi na akaunti za Chama katika Benki ya NMB zilikuwa na tishio la kuzuwiwa.

Naomba nikumbushe kuwa tarehe 2 Desemba 2016,Tume ya Taifa ya Uchauzi ilitangaza uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata 22 za Tanzania Bara.Nikumbushe kuwa baadaye Time ilifanya masahihisho na kueleza kuwa ni kata 20 ndizo zitakazohusika na uchaguzi mdogo.Pia CUF iliamua kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani,Zanzibar.

Hatimaye Chama kilisimamisha wagombea 14 kati ya kata 20 zilizotangazwa kurejesha uchaguzi.Upande wa Zanzibar CUF iliweka Mgombea Ubungo Jimbo la Diwani
Naomba nikumbushe kuwa wakati uchaguzi mdogo unatangazwa,Chama kilikuwa hakipewi ruzuku ya serikali.Kwa sababu tulitaka kushiriki uchaguzi na hatukuwa na fedha,mnamo tarehe 28 Desemba 2016 nilimuandikia Msajili wa vyama vya Siasa kuiomba Ofisi yake ikipatie Chama chetu fedha zitokanazo na ruzuku ya kila mwezi ya chama toka Serikalini ili kiweze kishiriki kikamilifu katika chaguzi ndogo zilizotangazwa kurejewa hapa nchini na kutekeleza Mpango Mkakati wa Ujenzi wa Chama chetu.

Msajili wa Vyama vya Siasa aliridhia Chama kipate sehemu ya ruzuku ili kishiriki katika uchaguzi na kutekeleza shughuli za Chama.Fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Chama ya Benki ya NMB,tawi la Temeke.

Katika kipindi kulikuwa na tishio la aliyekuwa Katibu Mkuu kuzuia akaunti zetu zote za Chama upande wa Tanzania Bara zisifanye kazi.Katika hali hiyo Kamati ya Utendaji iliamua shilingi 300 tulizoomba kwa ajili ya kugharamia uchaguzi zihamishwe akaunti ya Benki.Mwanachama huyo ni Masoud Mhina Omari,aliyekuwa Naibu Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na sasa Naibu Mkurugenzi wa Mafunzo,Itifaki na Udhibiti.

Shilingi milioni 69 zilitolewa kama fedha taslimu kuanzia kugharamia shughuli za kampeni za uchaguzi zikiwemo ziara za viongozi kwenda kwenye kata zenye uchaguzi mdogo.

Fedha zote zilizowekwa kwenye akaunti ya Masoud Mhina Omari zilitumiwa na Chama katika masuala ya Uchaguzi na uendeshaji wa shughuli za chama.Wakaguzi wa CAG waliokuja kutukagua walipewa maelezo haya na nyaraka za matumizi ya Chama ya Mwaka2016/17.

Chama kinamshukuru Masoud Mhina Omari kwa Uaminifu wake.Hatua ya kuweka fedha kwenye akaunti yake ilitusaidia kukamilisha shughuli za chama kwani baadaye Benki ya NMB ilizuwia kutoa fedha kwenye akaunti zetu zote za Tanzania Bara.

Naomba nisisitize tukio hili la kuhamisha fedha kwenda akaunti ya Masoud Mhina Omari lilitokea Januari 2017 kwa sababu ya tishio la kuzuia kutoa fedha toka akaunti za Chama.

Mgogoro wa Chama umemalizika na taratibu za fedha zinazingatia kanuni za fedha za Chama.

Tunakubaliana na Ushauri wa CAG kuwa mifumo ya udhibiti wa fedha ndani ya chama iimarishwe kwa kufuata sheria na Katiba ya Chama .Hivi sasa Mhasibu anaandaa mfumo imara wa udhibiti wa fedha ndani ya chama.

Prof.Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti waTaifa,27 March 2020.
 
Kwa iyo Mkaguzi alipopita huko mulishindwa kumueleza haya maelezo na kumpatia uthihitisho wa matumizi ya hizo fedha. Condom hii imeshatumika sasa nadhani inataka kutupwa kwenye doo la taka.
 
:D:D:D:Dngoja nijaribu kucheka kifaranza, Le professor Le-Pumba....

Namie nimefeli ka yeye...

Everyday is Saturday......................:cool:
 
maelezo ya kimtaa mtaa na kihuni hapo ndiyo mh. husema mbona we we in mpumbafu sana? Nitakufunga!!! kitaalamu huo ni wizi na ubadhirifu mnafaa mnyimwe ruzuku mpaka mtaporudisha pesa zote mlizozichezea kihuni,kodi yetu wananchi sio ya kuchezea chezea kihuni hasa wakati huu ambapo vyuma vimekaza
 
Mode hebu pigeni Ban hii Akaunti isiendelee kutujazia ujinga humu.

Hapa ↓↓ ulidai hizi Fedha zilitumika kununulia magari enzi za Maalim Seif.
Then unakuja tena na Stori tofauti!

Pumbavu zako.

RIPOTI YA CAG: Miaka mitatu nyuma CUF ilikuwa chini ya Maalim Seif si Prof. Lipumba - JamiiForums
RUZUKU YA CUF.png
 
Back
Top Bottom