Prof. Lipumba arejea nchini

Prof. Lipumba arejea nchini

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,868
Reaction score
5,753
Asema haungi mkono UKAWA.
attachment.php


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda jana. Picha na Said Khamis

Kwa ufupi

Asisitiza kutokubaliana na uamuzi wa Ukawa kumsimamisha Lowassa kugombea urais.

By Goodluck Eliona, MwananchiDar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita.

Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.

Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

"Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao," alisema.

Akizungumzia hatima yake kisiasa, licha ya kusema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, alisema hatashiriki kufanya kampeni kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuwa umoja huo umemsimamisha mwanachana wa CCM, Edward Lowassa.

"Kisiasa hatima yangu ni kama ya Mtanzania mwingine yeyote, Ukawa tuna mgombea kutoka CCM, amehama juzi tu, pia mle ndani ya Bunge la Katiba hakuunga mkongo Rasimu ya Katiba na ndiyo maana nikasema dhamira yangu inanisuta," alisema Profesa Lipumba.

Alisema wanachama wa CUF hawana sababu ya kuona kama amewaacha kwa kuwa bado yupo nchini.

Awali, akitangaza kujiuzulu, nguli huyo wa uchumi, alisema alifikia uamuzi huo kutokana na Ukawa kumkaribisha Lowassa kugombea urais kupitia umoja huo, hivyo dhamira yake inamsuta.


Chanzo;
Mwananchi

 

Attachments

  • FB_IMG_1439531993871.jpg
    FB_IMG_1439531993871.jpg
    41.8 KB · Views: 17,420
Huyu Prof Kajifuta Mwenyewe Kwenye Ramani Ya Siasa
Wenzake Wanaingia Ukawa Maana Neema Iko Jirani
Yeye Anakimbia
 
Mnakomboa nini?

watanzania wasiojielewa na ambao wanalazimishwa kuandamana hovyo huku wakisababisha uvunjifu mkubwa wa amani na kufanya uhalifu mitaani a.k.a panya road wa kisiasa wa chadema na ukawa.
 
Back
Top Bottom