Prof. Lipumba ana uhusiano gani Ponda?

Prof. Lipumba ana uhusiano gani Ponda?

Status
Not open for further replies.
Kumbe udini ni uislamu!!!!!! Leo ndio nimejua.

Sijawahi kumuona au kumsikia Lowassa amekwenda kufanya harambee ya kujenga msikiti au shule ya kiislamu lakini sidhani kama ameshawahi kuitwa mdini.

Acheni upumbavu mtakuja kuchinjana siku moja.

wewe umemuona lowasa anaandamana pamoja na wachungaji type ya mtikila???

Ponda ni sheiiii.twaann mtu
 
Ni masikitiko makubwa kuona Mheshimiwa msomi mwenye hadhi ya Profesa kushindwa kujiepusha na uchochezi, wakati viongozi wa madhehebu yote wakifanya jitihada kubwa kuondoa mpasuko katika jamii yetu, juzi Profesa alisema kuwa

“
tuache unafiki, tuungane na kumsikiliza Ponda kwa kauli zake, matendo yake ili kufikia kile ambacho Waislamu wanakitaka,” alinena Profesa Lipumba”

kauli hii inatupa ujumbe gani? Kwa wadhifa wake na heshima yake katika jamii, kauli yake ina mwangwi mkubwa kwa jamii hasa ya waislamu na kuwafanya waamini wakristu wanawaonea waisalamu. Au serikali inawapendelea waislamu.

Akizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alielezea kusikitishwa kwake juu ya kauli kwamba Sheikh Ponda asingeweza kupata dhamana katika kesi iliyokuwa ikimkabili.

“Vyombo vyetu haviko makini, tuliambiwa Ponda hawezi kupata dhamana lakini leo hii amefungwa kifungo cha nje, hii inatia shaka na uamuzi uliokuwa ukiendelea,” alisema Profesa Lipumba.

Mtaalamu huyo wa uchumi, alitumia nafasi hiyo kuwataka Waislamu kuungana na kuhakikisha kuwa wanatetea haki zao.


“Tuache unafiki, tuungane na kumsikiliza Ponda kwa kauli zake, matendo yake ili kufikia kile ambacho Waislamu wanakitaka,” alinena Profesa Lipumba.

Umati mkubwa wa waumini wa Kiislamu walimiminika kutaka kusikia mawaidha ya katibu huyo kwa mara ya kwanza baada ya kutoka gerezani juzi. Katika tukio hilo, waumini pia walichanga fedha kwa ajili kumwezesha Sheikh Ponda kugharimia matibabu ya afya yake na sehemu ya fedha hizo walipewa mawakili wake ili wafanye maandalizi ya kukata rufaa.

Pia Mei 18 mwaka huu, waumini hao wamepanga kufanya dua (Itikafu) itakayofanyika katika msikiti huo kwa ajili ya kumwombea Sheikh Ponda na wenzake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom