Prof. Lipumba ana uhusiano gani Ponda?

Prof. Lipumba ana uhusiano gani Ponda?

Status
Not open for further replies.

Kamura

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
508
Reaction score
52
Ninefungua gazeti la Mwananchi nikakutana na kichwa cha habari "Ponda bado ngangari" mbele ya hiyo headline kuna picha ya Lipumba na ndani ya hiyo habari kuna maoni ya Lipumba baada ya maelezo ya Ponda.

*Asema mkakati wa kukamatwa kwake uliandaliwa

Sheikh Ponda Issa Ponda
SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dares Salaam, kumwachia na kumweka chini ya uangalizi wa mwaka mmoja Katibu Mkuuwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda,jana aliibuka na kusema umefika wakati wa Waislamu kufanya uamuzi mzito.

Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya swalaya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam, Sheikh Ponda, alisema hatua ya yeye kuwekwa ndani kamwe haitamkatisha tamaa na kurudi nyuma katika mapambano ya madai ya Waislamu nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa kinyume cha sheria, wakati wana madai ya msingi ndani yataifa lao.

Alisema hatua yeye kukamatwa, ni wazi ilikuwa ni mkakati maalum unaoratibiwa na Serikali, wenye lengo la kuwafunga midomo masheikh waKiislamu ili wasiseme jambo lolote ambalo ni manyanyaso kwa jamii yao.

"Ni wazi hivi sasa, hawa wenzetu wanapigana nasi kitaalamu kwa kutunyamazisha midomo, kamwe hatuwezi kurudi nyuma. Hali ya Waislamu ni nzitona tunahitaji kufanya maamuzi mazito.

"Ni wazi kabisa, ninataka kulisema hili lieleweke kuwaUislamu wetu hauko kwa ajili ya Katiba, wala Utanzania wetu, bali ni kwa ajiliya asili ya dini yetu tu.

"Kwa muda mrefu, walikuwa wakifanya mikakati ya kunishughulikia eti sio raia wa Tanzania,niliwajibu wazi pale Mtoni kuwa hakuna mtu yeyote wa kuniweza kuninyang'anya.Na sasa wamebadili mfumo wa kutushughulikia masheikh kwa kesi za uongo.

"Ninataka kuwaambieni ndugu zangu, Waislamu hatutarudi nyuma, iwe katika amani au mapambano, ili mradi tu tuweze kuisongesha mbeledini ya Allah (Mwenyezi Mungu)," alisema Sheikh Ponda.


Maisha yagerezani
Alitumia mkusanyiko huo, kusimulia maisha aliyokumbana nayokatika gereza la Segerea.

Alisema aliweza kushuhudia mambo mengi, yakiwamo ya watu wengi kuwekwa mahabusu bila kesi zao kushughulikiwa.

"Walipo nikamata walinipeleka katika gereza la Segerea nakuniweka selo ya watoto, ambapo alikuja mtoto mdogo ambaye nilimuhoji na kusemaana umri wa miaka 10.

"Katika hali ya kushangaza, mtoto yule alisema amewekwa ndani kwa sababu ya tuhuma za kuiba pochi iliyokuwa na Sh 40,000.

"Kama iliwezekana kwa mtoto huyo kukamatwa, imekuwaje kwa mtoto aliye kojolea Koran pale Mbagala Oktoba 10,mwaka jana, hadi leo hajakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

"Leo hii, kwa mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha magereza mengi na makaburi nchini yamejaa masheikh ambao kila mara wamekuwa wakifikwa namadhila ya kesi za kusingiziwa.

"Leo kina Sheikh Farid, Mselem hadi leo hii maskini ya Mungu wamewekwa ndani kwa kesi za kusingizia tu, ila Mbeya yametokea machafuko katiya Wakristo ambao walichoma msikiti, lakini hadi leo hii hakuna hata kiongozi aliyefikishwa mahakamani."

Wakati akiyasema hayo, waumini wa dini ya Kiislam kila marawalikuwa wakikubaliana na maelezo yake kwa kutamka ‘Takbir ... Takbir' neno lenye maana kwa lugha ya Kiarabu ‘Mungu mkubwa'.

Juzi Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtia hatiani Sheikh Ponda na wenzake 49, ambao waliachiwa huru katika kesi iliyo kuwa ikiwakabili.

Washtakiwa hao, waliachiwa huru na Hakimu Mkazi wa Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakiliwa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na upande wa utetezi uliwakilishwa naWakili Yahya Njama.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Nongwa alisema: "Jamhuri imeshindwa kuthibitisha mashtaka kuanzia shtaka la kwanza, tatu, nne na la tanokwa washtakiwa wote, katika mashtaka hayo washtakiwa wote kuanzia wa kwanzahadi 50 hawana hatia.

"Katika shtaka la pili la kuingia kwa nguvu katika Uwanja waMarkaz Chang'ombe, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kwamba Pondaaliingia kwa nguvu, hivyo anatiwa hatiani kwa kosa hilo.

"Shtaka la kuingia kwa nguvu halielezi adhabu inayostahili kutolewa, lakini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au faini au vyote kwa pamoja.

"Kwa mshtakiwa wa kwanza (Ponda) hakuna kumbukumbu kwamba nimkosaji wa makosa mengine… mahakama inazingatia pia mshtakiwa alikaa rumande kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 18 mwaka jana hadi leo, hivyo inamwachiwa kwamasharti.

Alisema mahakama inamwachia Ponda kwa masharti ya kulindaamani, awe mwenye tabia njema kwa miezi 12 na endapo atashindwa atarudi mahakamani apewe adhabu nyingine inayostahili.


SOURCE MTANZANIA
 
wewe ulishaonaga wapi mtu anagombania urais tangu mwaka 1995 mpaka sasa bado anasema atagombea tena!
 
Ninefungua gazeti la Mwananchi nikakutana na kichwa cha habari "Ponda bado ngangari" mbele ya hiyo headline kuna picha ya Lipumba na ndani ya hiyo habari kuna maoni ya Lipumba baada ya maelezo ya Ponda.

huenda mwandishi kachanganya habari..
 
jamaa ana akili sana za kwenye vitabu, lakini akili za kuwa strategic ili awe rais hakubarikiwa nazo kabisa, hata mtoto mdogo anamzidi. isingekuwa udini, jamaa yule alifaa kuwa rais wetu na tungeshamchagua, lakini kwasababu akili yake iko obsessed na udini na ungunguli, na kusambaza chuki kwa waislam kuwa wanaonewa na wakristo (haki sawa kwa wote slogan), basi hana maana yeyote hapa tz. kwanza akatafute mke aoe wazeeke pemoja, ndo maana kikwete alimtania kule jangwani kuwa watu wanataka kuingia ikulu bila mke (slaa nae alipata dongo lake kuwa angeingia ikuulu na mke wa kuazima)...
 
Ninefungua gazeti la Mwananchi nikakutana na kichwa cha habari "Ponda bado ngangari" mbele ya hiyo headline kuna picha ya Lipumba na ndani ya hiyo habari kuna maoni ya Lipumba baada ya maelezo ya Ponda.
Labda nitatizo gani unalohisi ktk hiyo habari? Tumezichoka hizi hisia za kidini kila kukicha. Mods piga pini hii nyanga maana hauta fika mbali bila kuingia hisia za udini.
 
Prof lipumba amepotea kisiasa just leave him
Nanusa halafu ya udini hapo kwa sababu masuala anayohubiri Sheikh Ponda si ya kuungwa mkono na kiongozi mkubwa wa kisiasa kama Prof Lipumba. Halafu ngangari ndio slogan ya CUF inatumikaje kwa Sheikh Ponda au ndio waliomutuma? Najiuliza maswali mengi.
 
Labda nitatizo gani unalohisi ktk hiyo habari? Tumezichoka hizi hisia za kidini kila kukicha. Mods piga pini hii nyanga maana hauta fika mbali bila kuingia hisia za udini.

Mbona hakuna udini hapo mkuu?
 
Nanusa halafu ya udini hapo kwa sababu masuala anayohubiri Sheikh Ponda si ya kuungwa mkono na kiongozi mkubwa wa kisiasa kama Prof Lipumba. Halafu ngangari ndio slogan ya CUF inatumikaje kwa Sheikh Ponda au ndio waliomutuma? Najiuliza maswali mengi.

Hujui kuwa sera ya KAFU ya HAKI SAWA ilitungwa na kuasisiwa na jopo la MAULAMAA?
 
Ni kiongozi wa dini na muumini wake baasi
 
Al Shababu huyo.
Vipi na yule Al shababu wa Chadema (Lwakatare) bado yuko Jela? au nae kahukumiwa kifungo cha nje? mwaka huu tunashuhudia ma al shababu ktk kila sekta hata huko Arusha nasikia wamekamatwa ma alshababu 3 kwa kutupa bomu Kanisani wenye majina ya Kikristo kama ifuatavyo:Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)Al Shababu kwa kubadilisha majina bana! mara wajiite Lwakatare, mara Ambrose nk!
 
Mimi naona ni kama Pengo na Membe.
Au kama Lowasa na Malasusa
Au kama Slaa na Lema.

Kuna shida hapo? au kwa vile wako katika imani usioipenda?

Au shida za waislamu sio shida za wananchi? au shida za watanzania? Suala la baraza kuchakachua matokeo sio tatizo la nchi? Hivi Ponda akisema na Lipumba akilisemea, na au Mbowe akilisema inabadilisha maana?

Au tatizo ni mtindio wetu wa ubongo usioona haki?
1+1+1 = 1 does it make sense???
 
kinachowasumbuwa ni udini wenu,mbona slaa anashinda kanisani hamjamsema,lipumba mwislaam na anasali msikitini,nini kimekukera au ulitaka asali kanisani ndio aonekane si mdini,tatizo ni umbumbumbu wa kifikra mbashindwa kujuwa maana ya udini.ponda ni kiongozi wa kitaifa wa waislaam.pia tambuwa kuwa lipumba ni mfuasi wa dini ya kiislam,hivyo shekh ponda ni kiongozi wake kama ambavyo mbowe na slaa ni wafuasi wa uroma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom