Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

DAMU MPYA

Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
7
Reaction score
15
Prof. Lipumba ambaye ni wenyekiti wa chama cha wananchi Cuf amekerwa na tabia isiyo ya kinidhamu wala staha iliyofanywa na mbunge wa kigoma kasikazini Bwana Zitto Kabwe,


Katika kikao cha dharula alichokiitisha usiku ule wa mkutano baada ya kumaliza kuhutubia, alitufokea viongozi wa Mtwara kuhusu alichokiona katika mkutano, alisema aliwaona wanachama wa ACT-Tanzania wakiwa na mavazi yao na bendera zao akahoji kwanini tuliwaalika wakaja wakiwa na bendera zao na kuzichomeka hewani?

Mmoja wetu aliinuka na kujibu vizuri kuwa wale vijana tuliwakamata baada ya kuwaona na bendera hizo katika viwanja vyetu, tulipotaka kuwapeleka polisi mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Kaila alisema yeye ni afsa habari wa chama chao taifa,

Akadai kuwa walialikwa na zitto kuhudhuria mkutano ule,na wamekuja kwa gari lake alilowapatia waje nalo, ''Mh Mwenyekiti tunakuomba radhi sana kwa uliyoyaona pale uwanjani, wale vijana hatukuwaita sie, aliyewaleta toka dar es salaam ni swahiba wako uliyeongozana nae Zitto Kabwe, hata gari walilokuja nalo ni lake kawapatia''

Lakini pia prof. lipumba alidai kuwa ''zitto hana heshima hata kidogo kwa sababu tumemwalika sisi katika jukwaa la chama chetu, amekosa jukwaa la kuhutubia siku nyingi, leo tumempa fadhila lakini ametufanyia vitimbi, amekodi mpaka waandishi wa habri wake bila hata kuniambia, kumbe hata wafuasi wake amewagharamikia waje wakiwa na bendera na mavazi ya chama kingine katika mkutano wetu"?alihoji Prof. Lipumba

‘Mbona asitumie jukwaa la hicho chama cha wapambe wake? ikiwa ana unafiki wa namana hii basi hafai kupewa hifadhi kabisa' alimalizia Prof. Lipumba

Tarehe 31/12/2014 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano wake katika viwanja vya mashujaa hapa mjini Mtwara ambapo zitto kabwe alikuwa mgeni mwalikwa, pia watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa zitto walivamia mkutano huo wakiwa na bendera na mashati yenye chama kingine ambacho hakikuwa na makubaliano ya kufanya mkutano pamoja na cuf..
 
zito anaona akijitokeza waziwazi ni ACT atapoteza ubunge kabla hajafaudu posho za mwishomwisho
 
ACT Tanzania kumbe waligogea kwenye mkutano CUF mtwara duuh!!
 

Kwanini? Huwezi kufukuzwa Chadema ukakubalika mahali pengine popote. Kwa uvumilivu wa Chadema, kwa malezi bora ya Chadema kisiasa hususan kwa vijana; labda mwanasiasa ahame mwenyewe kistaarabu ila ukifukuzwa maana yake tabia yako is so abnormal to fit anywhere politically. Tumbili the Sisimizi mwenyewe chupu chupu atimuliwe huko alikokimbilia.
 
Mmmh!! Ebu nirudie kusoma tena kwa mara ya pili maana sijui cjaelewa au siamini,,, bt kama kweli kayafanya hayo, basi zitto anawakati mgumu sana kisiasa
 
Nilidhani ZZK yupo makini hasa baada ya misukosuko katika safar yake ya kisiasa iliyompata kumbe bado utot na kutaka sifa binafsi kuamuandama
 
Mmmh!! Ebu nirudie kusoma tena kwa mara ya pili maana sijui cjaelewa au siamini,,, bt kama kweli kayafanya hayo, basi zitto anawakati mgumu sana kisiasa

Anataka afanane na mshauri wa ACT
 
Hawa vijana wetu wa mwisho wa Reli ni shiida,hata kigoma wametuvuluga hakuna siasa tena kama enzi zile,wewe umeshaona wapi watu wanajenga sehemu ya kufungua tawi alafu wanasubiri chama chochote kiwapelekee hela ya Rushwa alafu ndio liwe tawi lao?.Kama haumini hilo njoo kigoma utaona aibu hii
 
Baada ya kazi nzuri ya ESCROW nilijua tumemrudisha Zitto kundini. kumbe dogo bado hajaeleweka!

Ana umimi sana huyu dogo!
 
Back
Top Bottom