Prof. Lipumba aiapia CHADEMA kutotawala nchi

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema anayeamini kuwa Chadema, kitatawala nchi hii atambue ni mgonjwa na anatakiwa kwenda kwa Mchungaji Mwasapile Ambilikile, maarufu kama Babu kupata kikombe cha dawa.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha soko la Mitumba, wilayani Muheza hivi karibuni, Profesa Lipumba alisema viongozi wa Chadema ni wafanyabiashara hawawezi kuongoza nchi.

"Kama kuna mwananchi yoyote Wilaya ya Muheza anaamini Chadema inaweza kuongoza nchi hii, basi huyo akanywe kikombe kwa Babu huko Loliondo", alisema Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro, alisema CCM imewafikisha wananchi wanakula mlo mmoja kwa siku, huku watoto wakienda shuleni na njaa. Mtatiro alisema hali inazidi kuwa ngumu, lakini CCM ambayo imesababisha ugumu huo inaona kawaida vyakula kupanda bei.


Source:
Mwananchi Machi 26, 2011
 
anaitetea CCM na mwafaka ndio maana huwa tunasema CUF ni CCM B mnabisha sasa jioneeni wenyewe
 
Unategemea mchumba wa CCM aseme Chadema watatawala nchi?! Han lolote huyo professa bwabwaja....wacha waendelee kuolewa na CCM
 
Ana punguza siku za kuishi bure kwa kuichukia chadema,...bora mda huu angeoa atulie
 
Unategemea mchumba wa CCM aseme Chadema watatawala nchi?! Han lolote huyo professa bwabwaja....wacha waendelee kuolewa na CCM
Kwa masikitiko makubwa namshuhudia Profesor Lipumba akibakwa ndani ya 'NDOA YA MKEKA' ya CCM/CUF na kupoteza taswira ya hali halisi ya Tanzania ya Leo. Tumebaki na Chama kimoja tu cha upinzani Tanzania .
 
......kula laki sita alizopata 2010 zinazidi kupungua nafikiri 2015 zitakuwa 200,000 za Bakwata na wazenji waishio bara. Bye bye poor CUF!!!! Zenji wanasema mkono mmoja "Mapinduzi daimaaaa!!" na mkono mwingine "Haki saawaaaa!!!"
 
Maskini lipumba!!! Ameshapotea, amesahau ccm walivyomvunja mkono pale kigambon akiwa anahutubia na frank magoba.
 
Nimekosa kabisa jina la kumwita huyu Lipumba. Ngoja niache tuu.
 
Ndugu waungwana,Hivi Cuf BILA KUITAJA CHADEMA mkutano wao haunogi?
Kiongozi wa cuf maneno matano ni chadema kati ya saba,
AU CHADEMA NDO WANAOTAWALA NCHI.?
Mbona TAMKO la kamati kuu ya CDM akuna sehemu yeyote katajwa Cuf kwanini?
Nini tatizo pale?.
CUF wamefanya mkutano Tanga mbona watu awajasema?
NCCR walifanya mkutano Kigoma yaliomkuta Mwenyekiti wake huko mbona CHADEMA aiseme.?
 
Kwa masikitiko makubwa namshuhudia Profesor Lipumba akibakwa ndani ya 'NDOA YA MKEKA' ya CCM/CUF na kupoteza taswira ya hali halisi ya Tanzania ya Leo. Tumebaki na Chama kimoja tu cha upinzani Tanzania .

Tusijidanganye wala kudanganyana!

....HAKUNA CHAMA HATA KIMOJA CHA UPINZANI TANZANIA!
 
ndugu waungwana,hivi cuf bila kuitaja chadema mkutano wao haunogi?
Kiongozi wa cuf maneno matano ni chadema kati ya saba,
au chadema ndo wanaotawala nchi.?
Mbona tamko la kamati kuu ya cdm akuna sehemu yeyote katajwa cuf kwanini?
Nini tatizo pale?.
Cuf wamefanya mkutano tanga mbona watu awajasema?
Nccr walifanya mkutano kigoma yaliomkuta mwenyekiti wake huko mbona chadema aiseme.?
woooote wanasiasa wa tanzania hawana jipya... Wanasemana na kupigana vita kila wanakoenda...

Kwa mtu yeyote mwenye kufikiri mbali.. Yanayoonekana kwenye vyama vya upinzani...

Ni uoza mtupu.
 
Lipumba amekuwa pumba sasa, hana maana kama kiongozi aliyepigania kambi ya upinzani kwa muda mrefu. Shida yake hapa ni ubinafsi, sasa wivu unamsumbua baada ya chama chake kupigwa bao na Chadema. Huyu profesa ni mbinafsi wa hali ya juu, ndiyo maana hataki kuwaachia wenzeka ndani ya CUF kugombea uraisi, amegombea mara nne na anatoka kapa.
 
Mwaka huu tutajionea mengi mno, hivi kumbe mkuki kwa nguruwe.........

Majuzi Mwanza, Geita na Bukoba Mbowe na Slaa walikuwa wakiisema waziwazi CUF majukwaani? CUF ni CCM B, CUF siyo chama cha upinzani, CUF wanaibeba CCM, CUF wanadhoofisha upinzani n.k. Hatu juzi wakati Dr (PhD) Slaa yuko kigoma amesema bila kubwabwaja kuwa CUF ni wakala wa CCM na kamwe hakiwezi kuwa chama cha upinzani, nadhani hayo ni matusi na kejeli na dharau za kutosha dhidi ya CUF kwa mtizamo huo ni muhimu CUF waseme wanayoyajua kuhusu CHADEMA, kama ni muda wa kuumbuana ndio huu, waumbuane weeeeee, sie yetu macho na masikio and i strongly recommend to cuf to move on shouting about CHADEMA as long as CHADEMA started it and is moving on with it.

Namaanisha b'se katika majukwaa ya cdm ajenda yao na adui yao mkubwa hivi sasa ni CUF na CCM then ni lazima ktk majukwaa ya CUF pia ajenda yao na adui yao mkubwa awe CCM na CHADEMA and that is how politics is.

Vijana wa UVCCM walivyomshambulia sumaye kisiasa lazima awajibu,kama walimponda naye awaponde na kama walimtukana naye amtukane, ndivyo siasa ilivyo the game of tit for tat, ktk mazingira hayo mashabiki wa CHADEMA mliojazana humu lazima muwe wavumilivu mno
 
SLAA-CUF inafadhiliwa na ccm kufanya mikutano ya kuishutumu cdm,cuf haiwezi kuwa chama cha upinzani,cuf ni chama popo,cuf haina uwezo wa kuongoza dola,


MBOWE- CUF ni mke wa ccm,cuf siyo chama cha upinzani,cuf ni ccm b, cuf ni wanafiki, cuf hawana mwelekeo,

LIPUMBA-Chadema ni chama cha wafanyabiashara na mafisadi nyangumi,chama cha wapiga disco,chama kisicho na uwezo wa kuwatoa watz kwenye umasikini,anayedhani cdm inaweza kuongoza nchi akanywe dawa ya babu loliondo,anaumwa.

Mtatiro- Tutajibu kila propaganda wanayosema cdm dhidi yetu, chama kinachotafuta dola hakiwezi kudhaminiwa na mafisadi(nyangumi) -sabodo,mengi na wenzie- siku kikipata dola kitawatumikia waliokifadhili,tutajibu hoja kwa kielelezo,propaganda kwa ukweli , mwisho wa siku ukweli utasimama,
MANENO YA VIONGOZI WENU HAYO,KATI YA HAO WOTE NANI MJINGA NO 1,2,3,4,
NANI MJINGA KULIKO WOTE,NANI TAAHIRA, NANI MJANJA?




.
 
mwaka huu tutajionea mengi mno, hivi kumbe mkuki kwa nguruwe......... Majuzi mwanza,geita na bukoba mbowe na slaa walikuwa wakiisema waziwazi cuf majukwaani? Cuf ni ccm b, cuf siyo chama cha upinzani, cuf wanaibeba ccm, cuf wanadhoofisha upinzani n.k. Hatu juzi wakati dr(phd) slaa yuko kigoma amesema bila kubwabwaja kuwa cuf ni wakala wa ccm na kamwe hakiwezi kuwa chama cha upinzani,nadhani hayo ni matusi na kejeli na dharau za kutosha dhidi ya cuf kwa mtizamo huo ni muhimu cuf waseme wanayoyajua kuhusu cdm, kama ni muda wa kuumbuana ndio huu,waumbuane weeeeee, sie yetu macho na masikio and i strongly recommend to cuf to move on shouting about chadema as long as cdm started it and is moving on with it.
Namaanisha bse katika majukwaa ya cdm ajenda yao na adui yao mkubwa hivi sasa ni cuf na ccm then ni lazima ktk majukwaa ya cuf pia ajenda yao na adui yao mkubwa awe ccm na cdm and that is how politics is.
Vijana wa uvccm walivyomshambulia sumaye kisiasa lazima awajibu,kama walimponda naye awaponde na kama walimtukana naye amtukane,ndivyo siasa ilivyo the game of tit for tat, ktk mazingira hayo mashabiki wa cdm mliojazana humu lazima muwe wavumilivu mno

yessir!!!
 
Ndugu waungwana,Hivi Cuf BILA KUITAJA CHADEMA mkutano wao haunogi?
Kiongozi wa cuf maneno matano ni chadema kati ya saba,.?
Mkuu, ndiyo dunia kila mtu ana mnyonge wake. Kama CCM ni wanyonge wa CDM. Basi CDM nao wamepata mbabe wao CUF ambaye kila saa yupo nyuma yao tu hapo. Najua inavyokukera, basi na kwa wengine ni hivyo pia.
Napita tu wakuu.
 
Back
Top Bottom