Prof. Lipumba aiapia CHADEMA kutotawala nchi

Prof. Lipumba aiapia CHADEMA kutotawala nchi

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema anayeamini kuwa Chadema, kitatawala nchi hii atambue ni mgonjwa na anatakiwa kwenda kwa Mchungaji Mwasapile Ambilikile, maarufu kama Babu kupata kikombe cha dawa.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha soko la Mitumba, wilayani Muheza hivi karibuni, Profesa Lipumba alisema viongozi wa Chadema ni wafanyabiashara hawawezi kuongoza nchi.

"Kama kuna mwananchi yoyote Wilaya ya Muheza anaamini Chadema inaweza kuongoza nchi hii, basi huyo akanywe kikombe kwa Babu huko Loliondo", alisema Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro, alisema CCM imewafikisha wananchi wanakula mlo mmoja kwa siku, huku watoto wakienda shuleni na njaa. Mtatiro alisema hali inazidi kuwa ngumu, lakini CCM ambayo imesababisha ugumu huo inaona kawaida vyakula kupanda bei.

Source:
Mwananchi Machi 26, 2011

Hii siri bado anabaki nayo moyoni.....kumpata mgombea Uraisi UKAWA itakuwa mbinde kweli kweli.....ila siasa bila unafiki haiendi.
 
Mtoa mada ni wakupuuzwa(mpuuzi) siamini kama kasema hayo,thibitisha weka audio yake. Na kama kasema haya bac amekopi kutoka ccm miaka yote walisha sema Cuf kuja kutawala tz ni ndoto za mchana, kama kweli aliongea maneno hyo je unajifunza nini kwa kiongozi kama huyu?
 
Mbona kuna threads na habari nyingi tu humu huwa huulizi kama ni za kweli au is za kweli na unachangia,
 
Nadhani JF mmetumwa kufanikisha hujuma flani. Mbona mnaibua mavi ya kale. Very sad ukizingatia hapa ndo tuliamini ni forum ya ukombozi. Mbele ya pesa, .................
 
Mkuu hutaki historia? Hii ndio JF mkuu kila kitu kinabaki kama kumbukumbu. Mkiambiwa wekeni akiba ya maneno hamtaki. Siasa siku zote haina rafiki ama adui wa kudumu.

Teh teh teh teh teh teh teh! Hamkumbushi yaliyopita nyie. Mnafanya tu propaganda ili muone kama ushirikiano wa UKAWA utatingishika. Lakini hiyo haitawasaidia sana. Nadhani mnajisumbua tu. Tafuteni gia nyingine! Propaganda hizo zimepitwa na wakati. Halafu zamani mbona kulikuwa na Chuo Kigamboni cha kufundisha propaganda, au siku hizi hawafundishi nini? This is nosense!
 
Nadhani JF mmetumwa kufanikisha hujuma flani. Mbona mnaibua mavi ya kale. Very sad ukizingatia hapa ndo tuliamini ni forum ya ukombozi. Mbele ya pesa, .................

Nafikiri lengo lao ni kutuonesha sisi wananchi jinsi hawa viongozi wetu wa upinzani walivyo wanafiki,wawe ni akiba ya maneno la sivyo kila siku watakua wanaumbuka.
 
STORY MFU YA MACHI 2011 KABLA YA UKAWA. MAMBO YAMEBADILIKA SANA TANGU WAKTI HUO!:rockon:
 
STORY MFU YA MACHI 2011 KABLA YA UKAWA. MAMBO YAMEBADILIKA SANA TANGU WAKTI HUO!:rockon:

Kumbe mnajua kuwa mambo huwa yanabadirika ila memory haibadiriki wote wanafiki tu,Lipumba mnafiki,Mbowe mnafiki wote wezi tu
 
Mnarudia hizi stori za zamani il I iweje mbona hamuweki TUMAINI la watanzania ukawa?au mkisikia hill neno ukawa mioyo yenu inajipiga shoti
 
Back
Top Bottom