Prof. Lipumba aendelea kudai Katiba Mpya kwa Rais Magufuli

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
TAARIFA KWA UMMA

PROF. LIPUMBA AENDELEZA ALICHOAHIDI NOVEMBA 2, 2020: AMPA MAKAVU RAIS MAGUFULI KUHUSU KATIBA MPYA:

Mwenyekiti wa CUF-Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim H. Lipumba ametoa wito kwa Rais John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake ya Kukamilisha kazi ya Kupata Katiba Mpya inayotokana na Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ambayo ni zao la Maoni ya Wananchi.

Prof. Lipumba aliongea hayo kwenye Sherehe za Siku ya Mahakama iliyofanyika leo Februari 1, 2021 huko Dodoma. Akimkumbusha Rais ahadi aliyoitoa kwenye hotuba yake ya Novemba 2015, Mwenyekiti wa Chama aliweka bayana kwamba kukamilisha kazi ya Kupata Katiba Mpya yenye maridhiano ni kiporo ambacho kinapaswa kushughulikiwa katika kuenzi kazi nzuri inayofanywa na Majaji nchini.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa Chama Prof. Lipumba ni sehemu ya muendelezo wa kutekeleza Maazimio ya Chama aliyoyafikisha kwa Umma Novemba 2, 2020 kwenye Ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo. Chama kimeazimia kuanzisha na kuendeleza vuguvugu la Kudai Katiba mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi kwa njia mbalimbali.

Katiba Mpya inayotokana na Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba iliyofikishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba inaaminika kuwa itakuwa Muarobaini wa Changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za Kidemokrasia.

Kifungu cha 28 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sheria Na. 83 ya 2011 kinampa Mamlaka Rais kuitisha Bunge Maalum la Katiba ( BMK) kwa Mara ya pili ili kuondoa dosari zilizopelekea kushindwa kupatikana Maridhiano kwenye Bunge la Katiba lililotangulia.

Tunaendelea kutoa wito kwa wadau wote kushikamana katika Mapambano ya Kudai Katiba mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Februari 1, 2021
 
Hongera sana Prof. Lipumba kwa kuthubutu kumkumbusha Mh. Raisi ahadi yake ya Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom