Prof. Lipumba aahidi utawala wake kuongozwa na tafitii kabla ya utekelezaji..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba aahidi utawala wake kuongozwa na tafitii kabla ya utekelezaji.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Jana kwenye mdahalo wake pale Movenpick, Prof. Lipumba alionekana kukerwa na utawala wa bora liende wa JK na CCM yake kwa kufanya maamuzi makubwa bila ya kuongozwa na tafiti.

  Akitoa mfano wa shule za kata alisema utawala wa JK ulikurupuka na kuanzisha shule za kata bila kufanya utafiri wa kina na matokeo yake fedha nyingi zimeteketea na huko shule hizo hazina matunda yoyote ya kujivunia. Kabla ya hapo kwenye mkutano wake wa hadhara jana, Prof. Lipumba alizitupia madongo shule za kata na kusema hata JK hilo analifahamu kuwa ubora wake ni wa chini na ndiyo maana hajapeleka mtoto wake kwenda kusomea kwenya shule hizo za kata.

  Prof. Lipumba aliutoa mfano wa Uchina ambako alisema kabla hawajaanzisha mradi wowote mkubwa wa kitaifa huanza kwa kufanya tafiti za aina ya "pilot studies" yaani kutenga maeneo machache ya majaribio ili kuona kama kuna mafanikio kabla ya nchi nzima kufuata miradi hiyo...Hivyo aliahidi ya kuwa utawala wa CUF atakaoungoza yeye utafanya tafiti za kutosha kabla ya kuanzisha mradi wowote mkubwa wa kitaifa........

  Tatizo kwa Prof. Lipumba hakuonyesha tafiti nyingi ambazo nchi hii tumekuwa tukizifanya zina mapungufu gani hata yeye utawala wake kujikita kwenye tafiti nyingi mpya kabla ya kuanzisha miradi mikubwa ya kitaifa na hivyo kukwepa mapungufu yaliyojitokeza kwenye tawala ya JK inayomalizia muda wake.

  Vile vile wakati kinadharia asemayo Prof. Lipumba yanaonekana yana maana lakini kiutekelezaji wake utamaanisha tafiti nyingi zitaishia kukusanya takwimu ambazo utamaduni wetu ni kuwa watendaji wala hawazisomi na huchukua muda mrefu na hivyo zaweza kuwa ni kikwazo cha watu kuwa wabunifu na kufanya maamuzi mazito kwa wakati mwafaka wakiogopa lawama za kufungwa na minyororo ya kusubiri matokeo ya tafiti.

  Wakati mwingine tafiti huchukua muda mrefu na mpaka matokeo yake yafahamike utakuta hata mahitaji halisi yanayopendekezwa yanakuwa yamepitwa na wakati na hivyo kutokuwa na manufaa hata chembe.

  Majibu siyo mepesi kama prof. Lipumba alivyoyaweka na kwa kutumia mfano mmoja tu wa shule za kata ambao ni kweli CCM na Jk walizitumia kama ni mtaji wa kisiasa na wala siyo kwa minajili ya kuboresha elimu yetu.........
   
Loading...