Jiongeze : kwani hujui kuwa magufuli kaanzisha mikwara ili na yy kama wenzake, Kumbuka mkapa akula kwa njia zake akaja Kikwete akajidai kurekebisha mikataba kwa hati ya dharula akapiga zake akaondoka na sasa yupo Canada kuangalia jinsi ya kulinda masilahi yake tokea zamani, kwa sasa Magufuli na yy yupo anaandaa njia zake za kula hiyo pesa ndiyo hiyo kaleta waziri , wameshajua watanzania wengi hawajui chochote juu ya madini wameamua kuja na mbinu zao ili na wao waambilie chochote kabla ya 2020.Kwa msimamo Wa Huyu Kabudi inatosha kumuambia atupishe katika kiti alichokalia maana anaonyesha kuwa na msimamo sawa na ule Wa akina Tundu lissu ambao kwa namna Moja ama nyingine wanaelekea kuwa wamhongwa na acacia.
Rais chukua hatua kwa huyu mtu
Prof. Kabudi: Sheria mpya za madini hazitahusu migodi inayoendelea
makinikia ni 5% ya madini lakini kule migodini kuna 95% bado inapigwa juu kwa juu yaani wale Wajanja wa CCM tokea kipindi hicho bado wanakula pesa bila kwele, Magufuli kaja na mbinu zake apate kula na yy hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyoUkimtumbua Kabudi basi ukamtumbue na Magufuli pia as it seems he shares the same thoughts.
Wewe hujiulizi kwa nini hawa BARRICK/ACACIA mpaka dakika hii wapo wanakwangua madini huko migodini kwa raha zao huku wakilindwa kwa mitutu ilhali Osoro kamuaminisha Magufuli na Umma kwamba wale jamaa ni fake na wanaoperate hapa illegally?
Hata mimi nakubaliana na wewe kabisa. Serekali yetu 'ikiamua' (asante kwa kunipa hii vocabulary) inaweza. Si waliamua kuwaingiza mawaziri wakuu kwenye mafao yasiyowahusu!!!, si waliamua kukamata watu then kuwaundia sheria ya uhujumu uchumi!!!. Waliamua na imefanyika. Kwa kuamua, serekali zetu ziko mbele sana. Mchana kweupeeee, wanaamua kuisigina katiba na maisha yanaendelea. Kwahiyo tuko pamoja mkuu, mi nakukubali...ulichoeleza ni utaratibu ambao unatumika kwenye sheria nyingi.
..mimi nimejaribu kujazia tu ktk hoja yako kwamba yapo mazingira maalum ambapo sheria hushughulika na makosa/masuala yaliyotokea kabla sheria haijatungwa.
..kwa mfano sikubaliani na hoja yako kwamba tukiondoa kinga ya Maraisi hatuwezi kuwagusa Maraisi waliopita.
..Bunge la Tz lilipitisha sheria ya mafao ya viongozi wakuu wakati Waziri Mkuu ni Salim Ahmed Salim. Sheria hiyo ilielekeza kwamba hata Mawaziri Wakuu[kawawa, msuya] waliotumikia kabla ya Salim Salim nao watapata mafao ya viongozi wakuu.
..mfano huo unathibitisha hoja yangu kwamba wakati mwingine sheria inaweza kurudi nyuma. Mfano mwingine ni sheria ya Uhujumu uchumi ya wakati wa utawala wa Baba wa Taifa.
..Ila lazima NIKIRI kwamba watetezi wa haki za binaadamu wanapinga sheria zinazorudi nyuma haswa ktk masuala yanayohusu jinai.
Wino wa damu you mean wale watu alikuwa anasemaje lisu wamefukiwa. Damu haituachi tuombee hao wadhalimu walipishwe na vizazi vyaoMikataba ya uwekezeaji kwenye madini ccm waliipitisha kwa wino wa damu kwa hiyo si rahisi kufutika hadi kizazi kichafu cha chama hiki kitakapopita
Nenda Syria mkuuSasa kama sheria hazihusu mikataba ya nyuma, na ndipo raslimali nyingi zilipo, hii sheria wamemtungia nani?? Na kwa nini ziwe za hati ya dharura? Nimechoka na hii serikali. Sjui niende nchi gani
Pole dada! Wanamchokonoa dingiAta akitumbuliwa hana chochote cha kupoteza atarudi idarani lakini pia mwenzako ni LEARNED BROTHER kitambo kwa siku anaweza kuingiza 20k usd per day kwa kusuka MoU. Maskini tunashida sana.
Yako ndiyo imeanzia hapo?
Ni kweli tumeshuhudia Rais akilishwa matango pori Mara nyingi na yeye anayatapika hadaharani, halafu ikigundulika ni tofauti anamute kama siyo yeye.Tukubali na mawazo tofauti, sio anachosema rais ndio lazima kiwe
mpongeze pia na tundu lisu kwa kutoa tahadhari mapema ambayo kabudi ameitumiaMimi nampongeza Professor,kaitendea haki taaluma yake. Kama kwa mtazamo wa kisheria tungeweza kuingia kwenye matatizo,basi kwa kuepuka kama nchi ikaonekana inafaa At First,tuanze upya,kwa wale waliotayari na makubaliano,waombwe angalau amendments ziwaguse katika ile tuiitayo Win-Win situation,tukiwaendea kidoplomasia,naamini watatuelewa. Sheria iko hivyo. Nampongeza Mh Waziri wa Sheria na Katiba kwa kufuata professionalism ili kwanza nchi inufaike na rasilimali zake lakini pia kuiondolea kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia ya kiuchumi.
Kuna mchangiaji kawaomba Mods waifute thread hii kwa madai kuwa ni ya chuki. Nafikiri kweli kichwa cha habari kina udhi,japo maudhui yaliyopo ndani hayaudhi.
ha ha ha... hata mimi nilijaza blanks na picha tu. hapo ndo tulipokosea na kuwapa loophole ya kufanya wanavyotaka. Kuna mtu alinionesha kipengele hicho nilichoka kabisa. kama isingekuwa hivyo, kesi hiyo wangeshinda asbuhi kabisa. kwa grounds kwamba sharia hutumika pale ilipotungwa naa kutowagusa wa nyuma.Kusema kweli mimi sikuwahi kusoma popote zaidi ya kujaza blanks tu na picha
Maajabu ya Tanzania,sheria ya bodi ya mikopo imetungwa mwaka jana lkn inawahusu waliohitimu vyuo vikuu kuanzia mwaka 1994 na wanakatwa asilimia 15 badala ya 8 waliyosaini.Hii ya madini yenyewe inaanza kuanzia ilipotungwa kwenda mbele hairudi nyuma na haitayahusu makampuni ambayo yanaendelea na uchimbaji!Hivi inaingia akilini kweli?wanasheria humu jukwaani saidieni kunielewesha hapa
Wachangiaji hapo juu wote akili zenu za kushikiwa, mpaka kuamua kucomment inamaana unauhakika na ulicho kisoma tatizo lenu mmekurupuka nawashauri mngeomba kwanza awapatie hiyo crip ya prof. Kabudi kutoka kwayo ndo comments zianze otherwise nonsense.Uharaka wa nini kama sio makinikia. Kweli lisu anatetea majizi